Zijue Injini 5 za Japan zilizopendwa sana na zenye nguvu sana

Zijue Injini 5 za Japan zilizopendwa sana na zenye nguvu sana

Cylinders - Koenigsegg 5.0-Liter V8

Nilivyo google nakutana na hili jini hapo juuu mzeiya, sio poaa.

nguvu ya anonymous [emoji185]
In terms of dispacement, Toyota ana 5.7 liter v8 nafikiri ni ur series iko kwenye landcruiser 200

Sent using Rocket Propelled Grenade
 
Kuna hii kitu 3UZ-FE V8 huu mzigo sauti yake tu inanenepesha masikio,achilia mbali ubabe wake ukiisikia jinsi inavyo pokea maelekezo kutoka Kwa gia box mwili lazima uchangamke
 
Japan ikiwa ni miongoni mwa nchi zenye kutengeneza magari kwa wingi duniani, na ikiwa inamiliki kampuni kubwa tatu za magari ambazo zipo kwenye top 10 ya makampuni makubwa ya magari dunian ambazo ni maarufu kama BIG THREE (TOYOTA, NISSAN na HONDA). Kampuni hizi pamoja na kampuni nyingine ndogo ndogo zimekuwa zikiunda magari yenye injini za technology tofauti tofauti.

Pamoja na hayo, inasemekana injini zifuatazo ndiyo injini bora kabisa na zenye nguvu sana zilizowahi kuundwa nchini Japan. Wale fans wa Mbio watazimis sana injini hizi..

1. 2JZ-GTE (TOYOTA)
Hii ni injini bora kabisa yenye nguvu kutoka kampuni ya Toyota.
Injini hii ina inline six cylinders, twin turbocharged na inauwezo wa kutoa 276hp (206kw)
Ilianza kuzalishwa mwaka 1991 mpaka 2002.

2.RB26DETT (NISSAN)
Hii ni miongoni mwa injini bora kabisa kutoka Nissan ni inline six cylinder, twin turbo charged. Ina uwezo wa 276hp (206kw)

Imetumika sana kwenye Nissan skyline na GTR

3.EJ20k. (SUBARU)
Hii ni injini kutoka kampuni ya Subaru. Ina four cylinders, boxer engine yenye turbo moja. Ina uwezo wa 295hp (219kw). Imetumika sana kwenye subaru impreza WRX na Impreza WRX STI.

4. 13B-REW (MAZDA)
Injini hii imetoka kampuni ya Mazda...Ni Wankel engine au maarufu kama Rotary engine. Ukubwa wake ni Lita 1.3 tu lakini ina uwezo wa 276hp (206kw)

Imekuwa ikitumika kutoka 1972 mpaka 2002 kutokana na ubora wake, imetumika takribani miaka 30. Weka mbali kabisa na watoto

5. K20A. (HONDA)
Hii ni injini kutoka kampuni ya Honda..Ilianza kuzalishwa mwka 2001 mpaka 2011.
Ina 212 hp(158kw)..Imetumika katika model tofauti tofauti za Honda ikiwemo Honda Civic

Nadhani wale fans wa mbio na sauti za kibabe za injini, watazimis sana hizi injini...[emoji39][emoji39][emoji39]..kwa sababu kwa sasa magari yanafungwa majenereta na si injini..







Sent using Jamii Forums mobile app
Kwenye List hii ya racing engine hujatenda haki kwa kutoweka Kampuni ya Mitsubishi Motors Corporation (MMC).

Ambapo Mitsubishi Lancer mpaka uzao wa Evolution engine zake zimetamba na zinawasumbua wakina Subaru na Toyota.

Mitsubishi injini zake zilizotamba ni 4G91,4G92,...... na 4B16 za kwenye evolution.
 
Hii mada inahusu injini bora za kijapani katika mbio ambazo nyingi zipo upande wa petrol.

Hizo 1hz,2L na nyinginezo hizo zinawekwa kwenye list ya injini bora za diesel.
 
Kuna hii kitu 3UZ-FE V8 huu mzigo sauti yake tu inanenepesha masikio,achilia mbali ubabe wake ukiisikia jinsi inavyo pokea maelekezo kutoka Kwa gia box mwili lazima uchangamke
Mkuu hii bado ni mtoto kwa injini ya 1VD-FTE imefungwa kwenye Land Cruiser series 200 na 79.

Hii ukiisikia inavyokohoa lazima ufurahi mpaka moyoni.
 
NISSAN SKYLINE.
Sikiliza mapigo ya RB engine ikitoa sauti yake halisi..

Wale wanyoa viduku wanaofunga vibuyu kwenye Alteza waje hapa....[emoji119][emoji119][emoji119][emoji119]



Sent using Jamii Forums mobile app
 
TOYOTA SUPRA..
Sikiliza 2JZ hapa na sauti yake halishi..

Wanyoa viduku wa Alteza na hivyo vibuyu mnavyofunga , mtupumzishe kidogo.[emoji119][emoji119][emoji119][emoji119][emoji23]



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom