Zijue mbinu wake zetu hutumia kuwasiliana na michepuko kwa simu bila sisi kujua

Zijue mbinu wake zetu hutumia kuwasiliana na michepuko kwa simu bila sisi kujua

kasulamkombe

JF-Expert Member
Joined
Oct 3, 2017
Posts
2,232
Reaction score
2,491
Unajua baada ya mwanamke kumpata mwenza wake wa raha na shida huwa mara moja moja wengine wanaendelea na zile tabia zao za zamani au mahusiano mengine yasiyo rasmi lakini huwa waangalifu sana kwani huwa wanaogopa sana kushikwa.

Wanaogopa Kutema big g kwa karanga za kuonjeshwa kwani huwa wanajua kuwa mwanaume akishakufumania tu hata mara moja anaweza akasema kuwa amekusamehe lakini mahausiano hayatarudi kabisa kama zamani.kuna vitu atakuwa hakuamini tena.

Mbinu Ambazo huwa wanatumia ni kama zifuatazo:

1. Kuwa na line mbili.line moja utakuwa unaijua na ndiyo itakuwa kwenye simu kila siku na hasa akiwa nyumbani na wewe na simu atakuwa anaiacha mezani au sehemu yeyote na hana presha kwani hiyo namba anakuwa hajampa jamaa yake.watakuwa wanapiga ndugu,marafiki na wafanyakazi wenzake.hii simu hata atakuambia angalia ni nani anapiga

2. Mbinu nyingine anakuwa na line tofauti ambayo huwa anaiweka kwenye simu wakati either haupo nyumbani au kwa usalama zaidi anaiweka anapokuwa kazini au siku ambazo huwa wanakubaliana kuwasiliana. kuna ambao huwa wanawasiliana wikendi tu, wengine jumapili tu na wengine siku au kipindi mme huwa nakuwa kazini. shambani au katika mizunguko mke huwa anajua ratiba nzima.hii line huwa wanaiweka mara nyingi kwenye pochi

3. Njia nyingine ni huwa wanakariri namba ya jamaa yake na anamwambia kuwa usinipigie wala kunitumia meseji mimi ndio nitakuwa nakupigia. anakuwa anatumia namba za simu za marafiki kumpigia simu na kupanga ratiba lakini hiyo namba haandiki jina sehemu yeyote ile

4. Njia nyingine anakutambulisha jamaa yake kama ni mtu wake wa karibu kikazi au biashara na atakuambia ni ndugu kwa hiyo hutakuwa na shida naye na atafanya huyo jamaa awe rafiki wa mme wake zaidi.anaweza kuwa ni fundi, biashara na kwahiyo mme utakuwa na rafiki mme mwenzako bila ya kujua.ratiba zako wote wawili wanakuwa wanazijua

5. Mbinu nyingine ni ya kwenda kwenye maombi kanisani.huko nusu ni maombi ya kutoa mashetani na pepo na nusu ni kutoa pepo za ngono.wanatafutana kumalizana kiu wewe ukijua kaenda kusali.au siku za mpira hasa wanaojua ratiba za ligi za ulaya wakati arsenal inafungwa kule na huku ndoa inagegeduliwa au wanawasiliana la line ya kificho

Naomba kuwakilisha.hizi mbinu na tuendelee kuishi kwa amani.Usimchunguze Sana unaweza jua nyingi mimi kwangu hizi zote nazijua ila najifanya sizijui ili ndoa iendelee tu!
 
Usiwaonee wanawake hata wanaume pia wananitumia
1.Mwanamke anaemchukulia bwana rafiki yake hupenda kujiita Twin mdada ukisikia hivyo stuka
2.Mwanaume ukitambulishwa mke au Manzi wako kidume chenzako eti Cousin yake Stuka fikiri mara 2 mbili
 
Usiwaonee wanawake hata wanaume pia wananitumia
1.Mwanamke anaemchukulia bwana rafiki yake hupenda kujiita Twin mdada ukisikia hivyo stuka
2.Mwanaume ukitambulishwa mke au Manzi wako kidume chenzako eti Cousin yake Stuka fikiri mara 2 mbili
ndio na nyie njooni na mbinu za wanaume mnazojua.hapa ni kubadirishana uzoefu kwa nia njema tu!! wote sio malaika ila inauma ile kitu kitamu kula peke yako aisee
 
kuwa na amani mama yupo kanisani salama.leo ni kubadirishana maujuzi tu wote ni binadamu na tusingependa kukwazana kwani ile kitu tamu sana sasa ukisikia kuna mtu anakula mwingine kunakuwa na kawivu kidogo
Unaharibu jumapili ya watu wewe.
 
wenzenu bado wapo kwenye hizi mbinu na wengine bado mazuzu eti anatembea na simu muda wote mpaka bafuni.akiwa anapika yupo nayo mpaka inatia shaka.simu nyingine anapokelea nje mara chooni au bafuni
Kwambinu hizo bado sana. Hapo mtu anakamatwa. Siku hizi tume Advance. Sio O level
 
Kiukweli mimi huwa nawaonea sana huruma wanawake wanavyofanya huwa wanaona wanatukomesha sana ila hakuna mtu mbaya kama mwanaume anaweza kulala hadi na mama Mkwe wake sema tu huwa tunawaonea huruma maana akili zao hazijasimama dede.
 
#3 kuna dame aliniambia hivyo nikaona huyu s anataka kunifanya mchepuko ngoja nimfundushe aisee
 
Hii ya kanisani ni kweli, kuna ndoa ya mshkaji wangu ilivunjika kiutani utani hivi hivi, jamaa alipata mwanamke wa kiislamu, mwanamke mzuri kwelikweli, chocolate colour na makinikia ya kutosha.

Wakafunga ndoa bomani, ila akaamua kua mkewe ni lazima awe mkristo, so akampeleka kanisani kwao akamtambulisha na harakati zikaanza, baada ya miaka miwili mtoto wa kike akawa kajiunga mpaka kwaya ya kanisa, jamaa akajua naaam dini imekolea Mkewangu.

Bahati mbaya sana jamaa kanisa anaenda pasaka au xmass baaasi.. Sasa jumapili moja mkewe katoka church, wamepata lunch mke kaingia kuoga, kajikoki fasta fasta kaaga anaenda kwao mara moja Bi'mkubwa'ke kamuita, kwao ni mbezi mwisho kule, jamaa kasema poa yeye akaendelea zake kucheck mpira.

Mara bibie akaaga akaondoka zake, hapo ilikua mida ya saa Tisa kuelekea kumi jioni, so alikua na haraka ili kubalance muda, baada ya kuondoka na haraka haraka zake akasahau simu mezani, kidogo ikaanza kuita, jamaa akaiona, akasema ngoja nitoke nimuwahi kabla hajafika mbali, ila katoka kakunja kona ya kwanza, ya pili, kama Mungu tu akamwambia "acha ubwege hebu chungulia humo kwenye simu kuna nini" LAHAULAH aliyoyakuta humo yalikua mazito!

Break ya kwanza akaenda kwa muinjilisti kumshtakia huyo "Mzee wa kanisa" aliyekua akimpakua mkewe..

Alipotoka huko kwa Muinjilisti akaja kwangu, alivyovaa na taharuki aliyokua nayo nikamuuliza vipi ndugu yangu? Akanipa "Samsung" ya mkewe nisome, Doh, ni aibu! Mtoto wa kike anausifia "mkuyenge" wa Mzee wa kanisa + mapicha picha kibao.

Jumatatu yake mapema sana tukaamkia kwenye kikao kizito ndani ya kanisa. Uliwaka moto wa hatari sana pale kanisani pembeni ya madhabahu ndiyo tulikaa.. Mzee wa kanisa aliitwa kwa tyming bila yeye kujua na mkewe akaitwa kutoka kazini akiambiwa afike kanisani haraka sana kuna dharula, mama wa watu kaja kapanic ile mbaya!

Basi bwana, mambo yakawekwa hadharani, hapo hapo mwanamke akaanza kulia na kuanza kulalamikia wanawake wengine wa hapo hapo kanisani, Mara muimba kwaya mwengine naye akataja wake, basi ikawa kizaa zaa pale. Wakati huo yule mke wa jamaa yangu alikua kakimbilia kwao, maana toka Jana yake ile aliposhtuka na kurudi home kufuata simu akukuta jamaa hayupo, wala simu Hamna, milango haijafungwa, TV iko on, akajua hapa ni kizaa zaa. Akakimbilia kwao.

Basi huku na huku ndoa ya mshkaji ikavunjika kiutani utani tu.

Jamaa akaapa hatokuja kukanyaga kanisani tena.
 
Nyingine ni hii
Anatumia habadilishi laini ila mchepuko ukimpigia simu mumewe akiwepo, atapokea simu vizuri na kuuliza naongea na nani?
Mchepuko ukishasikia hivyo utajua mwenye mali yupo, utajibu, hoo sorry nimekosea mamba.
Pia michepuko huwa inapeana majina feki.
 
Kiukweli mimi huwa nawaonea sana huruma wanawake wanavyofanya huwa wanaona wanatukomesha sana ila hakuna mtu mbaya kama mwanaume anaweza kulala hadi na mama Mkwe wake sema tu huwa tunawaonea huruma maana akili zao hazijasimama dede.
Dah ulivyotaj mam mkwe moyo ukalia paah nikadhan tayar ijumaa wikiendaaa...
 
Back
Top Bottom