Zijue mbinu za Kisasa za Kumkwepa kumlipa nauli Kondakta katika Daladala

Hizo mbinu huwa zinanifikaga mara nyingi, sio kuwa sina hela ila tu huwa ni mtu wa kuchezea simu muda mrefu napokuwa kwenye gari. So hio ya konda kupita na hatimae kusahaulika inatokeaga sana saingine nawapa nikiwa nashuka ila muda mwengine nawapotezeaga tu kulingana na mood yangu!
 
Fundisha kukwepa kodi nauli ya 400 nikwepe ya nini

Enzi nasoma mwanafunzi nauli 50 nime panda sana dala dala bure

Hadi makonda wa posta wakanikariri wakiniona wanaomba nauli mlangoni
 
hahahaa...
hizo enzi za uanafunzi konda akikuomba nauli unasema umekaa vibaya, alafu baadae unahama siti watu wakipungua kama sio muangalifu hapo kaishaliwa, au unahamia siti ya mbele kutoka kwenye bansenburner mtu akishuka (hiace). Hapo ndio kaisha sahau.
ila sio vizuri huo ujanjaujanja kwa kweli.
 
Umewashtua masela!
Makonda watakaba mpaka penalt.
Usishangae ukadaiwa nauli wakati wa kutinga kwenye daladala.
 
[emoji28] [emoji28] [emoji28] [emoji28] [emoji28] [emoji28]
 
Akya kya kya kya kya kya kya kya kya hizi mbinu zinafaa kwa wale wa mbagala na Gongo la mboto mida ya jioni na asubuhi
 


Na kwa nini ukwepe kulipa Nauli? Kwa nini unataka kula jasho la Binadamu mwingine anayejituma kujikwamua kila siku kama wewe unavyojituma kwenye kazi yako? Unaelewa hata maana ya neno ,,HAKI"? Kama hauna hela ya nauli kwa nini usiongee naye kwanza na kumuomba? Acha hizo konda anahitaji hela kama wewe na mimi hata yeye ana familia ya kuhudumia pia hivyo tuache mambo ya kurudishana nyuma, lipa nauli kwa faida ya wote!

Kila la Heri!
 
Nimeshawahi kufanya muda wa usiku.
Kuna abiria huwa wanakwepa nauli. Utakuta umechukua nauli kwa kuanzia mbele, ile unamaliza nyuma, gari linafika kituoni halafu kuna abiria labda watatu wanashuka na watano wanaingia.
Sasa kati ya wale walioingia, unakuta wote wamepata siti, sasa si inabidi urudi kwa kuchezesha sarafu! unakuta mwingine anajikausha kabisa halafu unajua kabisa huyu abiria amepanda sasa hivi na ana mwonekano wa kipekee ambao haukuwepo kabla kwenye gari wakati nachukua nauli. Huyo unamkomalia hadi anaona aibu na hafiki mwisho wa safari.
Hiyo tabia wanayo sana masharobaro, halafu abiria akisema amlipie eti wanajifanya kukataa.
 
ongezea na hii

atalipa mbele(kama wewe upo nyuma) ,au atalipa nyuma (kama wewe upo mbele.

njia hii nzuri kama mpo wawili mnafahamiana (wambele na wanyuma)

[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]

*Akifa shekhe kazi ya Mungu*
*Akifa mlevi sababu ya Pombe*
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…