Zijue MISSION 09 za KBG (FSB sasa) ambazo kama baadhi zingefanikiwa Dunia ingekuwa tofauti na leo

Zijue MISSION 09 za KBG (FSB sasa) ambazo kama baadhi zingefanikiwa Dunia ingekuwa tofauti na leo

Kama ilivyo CIA, KGB (imekuwa FSB kuanzia 1995)shirika la kijasusi la USSR sasa URUSI limewahi kuhusika katika operation hatari sana maeneo mbalimbali Duniani. Kilele cha operation hizo ilikuwa kipindi cha vita baridi. Taarifa nyingi zilijulika pale jasusi la KGB Vasili Mitrokhin lilipotorokea uingereza na Mafaili yenye siri nyingi maana alikuwa ni mtunza kumbukumbu wa shirika hizo.

1:MASHAMBULIO KWA MIUNDOMBINU YA MAREKANI
Hungry-Horse-Dam.png

kUANZIA 1957 Hadi 72 KGB walianza kupiga picha miundombinu ya marekani kwa siri. Mitambo ya umeme,Mafuta chochote kile ambacho kingeleta athari za kudumu kwa mmarekani kilipigwa picha.Mipango yote ilikuwa ni kuahakikisha ikitokea vita, wanapiga shambulio moja amerika hasa new york inakoswa umeme, na kuanza kushambuliwa na russia mtaa kwa mtaa.

2: MIKAKATI HATARI YA KUOKOA MATEKA RAIA WA URUSI.

Hostage-Retribution.jpg

Mwaka 74 walinda kikosi maalumu kiitwacho ALPHA GROUP. KBG waliunda kikosi hiki kutekeleza mission za siri sana na Za kikatili kupita kiasi ili kuwaokoa mateka wao. Mfano ni huu wa LEBANON.
Magaidi waliwateka wanadiplomasia wanne wa kirusi siria. Lengo ni kuizuia russia isiiunge mkono siria.Baada ya maridhiano kufeli na magaidi kuonyesha wamemuua mmoja wa mateka, ndipo kikosi hiki kikaingilia kati, waliperereza na kujua kundi hilo ni hesbula. Wakamteka ndugu wa karibu na kiongozi mkuu wa hesbula. wakawa wanamkata vipande vidogo vidogo vya mwili wakivituma kwa kiongozi huyo vikiambatana na ujumbe.Baadae walimuua na wakamtumia kiongozi huyo ujumbe kuwa wanajua pote walipo ndugu na familia yake na kinachofuata ni kuwafanya wote kama huyo ndugu yao akiwemo na yeye aliyedhani hajulikani. Haraka sana magaidi waliwaachia hao mateka bila masharti yoyote.

3:KUTUMIA WANAWAKE WAREMBO KUREKODI VIDEO ZA NGONO ZA VIONGOZI
Blackmail-Stewardess.jpg

KGB ilijumuisha wanawake warembo waliowaita "SWALLOWS", USSR walikuwa na mpango wa kutawala dunia, Mshirika wao Indonesia alipopata nguvu walipata hofu atawaasi na kujikita na uislamu. Raisi wa nchi hiyo SURKANO ndio alikuwa kikwazo. Baada ya kumfuatilia waligundua anaudhaifu mkubwa katika NGONO. Walipanga SwALLOWS wa kutosha hotelini alipofikia na kwenye ndege kama wahudumu. Bila kujua wakamrekodi akiwa anafanya mapenzi na wadada hao kwa mpigo. Walipomtishia na kumtumia hizo clip ili awe mpole aendelee kuwaunga mkono, majibu yakawa tofauti maana hakushtushwa na aliomba wamtumie nyingine zaidi maana zile zilikuwa ni chache. Jaribio likafeli.

4:KBG HACKERS (WADUKUZI WA KIMTANDAO) WALITEMBELEA ZAIDI YA COMPUTER 400 ZA WANAJESHI WA MAREKANI
Old-Computer.jpg

mwAKA 80 Walikuwa wanatafuta jinsi ya kuPATA siri za jeshi la marekani. Walimuajiri jamaa anayeitwa Markus Hess mtaalamu aliyebobea katika anga hizo. Shughuli nzima ilifanyikia UJERUMANi ambapo aliweza kuACCESS computer zaidi ya mianne za jeshi la US. Akifanikiwa kubashiri PASSWORD za computer muhimu kabisa PENTAGON na kupata taarifa za siri za wanajeshi lukuki.
Hadi pale mtaalamu wa US Cliford stoll siku moja katika pitapita zake akaona vitu asivyovielewa kwenye system yao. ilimchukua miezi 10 kujua nini kilikuwa kinaendelea na huyo jamaa aligundua ana SUPPERACCESS ya Deffensive system ikiwemo mitambo ya nyuklia marekani. Hadi alipowekewa mtego wa kimtandao na kunaswa huko hannover ujerumani. alikuwa anawauzia KBG hizo siri.

5:OPERATION RYAN
Spying-on-the-US.jpg

Miaka ya 80, ulizuka uvumi kuwa US wanajiandaa kuilipua russia muda wowote na makombora ya NYUKLIA. Ndio KGB na urusi wakaja na hii operation ambayo ni kubwa kuwahi kutokea.
Walipanga kuweka satelite zitakazopiga picha vituo vya kijeshi marekani nzima kila sekunde kuona kama kuna kombola linakuja,Pia kumonitor matumizi ya RADA amerika yote ili kuangalia uwezekano wa shambulio. Pia kuwachunguza raia na wanajeshi wa marekani wote wanapoondoka US, PIa kuiweka NATO chini ya uachunguzi wa hali ya juu. Walijaribu kuingilia mawasiliano ya simu yote nchini marekani na ulaya yote. Waliweka mtandao wa MAKACHERO duniani ambao wako tayari muda wote kushambulia wakiona urusi inavamiwa na marekani. Operation hii ya mabilioni ilihairishwa miaka mitatu baadae.

6:KUNUNUA BENKI ZA WAMAREKANI
6-us-bancorp.jpg

KBG hawakupanga kutumia mashushu wao kujua siri za selikali ya malekani, Badala yake walitumia BENKI.Wlipanga kununua BENKI TATU huko Northern California. Hawakukurupuka walijua benk hizi zilitumika na makampuni yaliyokuwa yanatengeneza TECHNOLOGY za jeshi la US, Wakaona kumiliki hizo benki watapata taarifa za siri za nini wanafanya jeshini kwa maana ya teknolojia.CIA walishtukia huu mchakato baada ya kugundua Mnunuzi kutoka Singapole aliingiziwa pesa kutoka RUSSIA.

7:OPERATION PANDORA
Watts-Riots.png

Waliendelea kuiandama marekani maana ndio alikuwa adui yao namba moja. Safari hii KBG wanapanga machafuko ndani ya US. Unakumbuka miaka ya 60 kulikuwa na vuguvugu la watu kupinga ubaguzi, kwa KGB hii ilikuwa ni fursa. Waliandaa vipeperushi NEW YORK na majarida feki yaliyoonyesha watu weusi wanawavamia wenye asili ya WAYAHUDI na kuwaibia vitu. Majarida haya yalionyesha kuwa walalamikaji ni kundi la waisrael JEWISH DEFENCE LEAGUE ambao kwa FBI walihesabiwa kama magaidi. Kisha wakayasmbaza kwa watu weusi waliokuwa wanamiliki silaa na mapolisi/wanajeshi weusi uchochezi huu wajiandae na mashambulizi ya wayahudi. Kuzidi kuchochea KGB walipanga kukilipua chuo kilichojaa wanafunzi weusi tu. Baada ya kulipuka chuo watume ujumbe kwa vyama vyote vya watu weusi kuwa ni WAYAHUDI ndio wanahusika.

8:SAKAFU YA KUSIKILIZIA
Hotel-Viru.png

KBG walikuwa wako vizuri sana ktk kuweka vinasa sauti kusikiliza mazungumzo katika maofisi na majengo mengi. Yaani waliwahi kuweka vinasa sauti katika hoteli maarufu kwa zaidi ya miaka 20 bia kujulikana. Mfano nchini ESTONIA jengo lenye ghorofa 22 lililokuwa linafikiwa na wafanya biashara wakubwa duniani, kulikuwa na floor ya 23 ya siri iliyokaliwa na KGB kwa muda wa miaka 20 hadi USSR ilipoanguka mwaka 1991. Mtoto mdogo aliyempa barozi wa Marekani Russia zawadi ambayo ilipachikwa kinasa sauti chenye uwezo wa hali ya juu. Kwa miaka saba KGB walikuwa wanasikiliza mawasiliano yote hadi kilipo gunduliwa ka bahati mbaya na mfanyakazi wa radio wa UK alipokosea mawimbi na kusikia mazungumzo asiyoyaelewa.

9:KUFADHILI UGAIDI
Terrorists.jpg

Jasusi la KGB Aleksandr Sakharovsky anajinasibu kuwa "Utekaji wa ndege ni UVUMBUZI WAKE".
Waliungana na YASSER Alafat na kumsaidia kuchukua madalaka ya PARESTINA. Walitengeneza magaidi wa kutosha na wapigania uhuru ili kuwadhoofisha maaduia wao. Mfano mwaka 69 tu ndege zaidi ya 82 zilitekwa sehemu mbalimbali duniani na hawa jamaa. Walichochea vita huko IRELAND kwa kuwasambazia Bunduki,bastola, mabomu wanajeshi kitu kilicholeta machafuko makubwa. Lengo lao lilikuwa ni kutengeneza mataifa mengi yenye kuunga mkono ukomunisti.

DUNIA INA MAMBO MENGI,
HII NI TAASISI MOJA TU LAKINI UKISOMA KUHUSU CIA(US), MOSSAD(UZAYUNI), MI6(UK), ISI (PAKISTANI),BND(ujerumani), RAW(INDIA), DGSE (UFARANSA),ASIS(AUSTRALIA) NA MSS(CHINA) UTAJUA GHARAMA YA KUILINDA NA KUITANGAZA NCHI KATIKATI YA MAADUI BILA VITA.

Vyema basi tuletee na visa vya UK na common wealth
 
Kgb na fsb ni vitu viwili tofauti.KGB ilikuwa dissolved na FSB wala haifanyi kazi zilizokuwa zinafanywa na KGB
 
Mkuu hao informer wanawapataje? na kuwaamini hivyo?
Ni kwa kutuma maombi.uwaeleze unataka kuwasaidia nini.na wala hawakuamini kiiivyo kukupa kazi nzito wakiona umewajua sana,mwisho wa siku ni.

Crush the bottle after using it.
 
Kgb na fsb ni vitu viwili tofauti.KGB ilikuwa dissolved na FSB wala haifanyi kazi
zilizokuwa zinafanywa na KGB

Safi, mamlaka ya kiutendaji yaliboreshwa mkuu, FSB ikapewa majukumu maalum nje ya nchi ya Urusi na yale matawi ya iliokua KGB yaani FSO na SVR yakawa na kazi za ndani ya nchi ,kuna mabadiliko yalifanywa na Rais kipindi hcho anaitwa Boris Yeltsin kubadili mfumo 1991-1993 kuimega kisheria KGB kuwa fSK iliongozwa na mtaalum Sergei stepashin ,polepole na mwaka 1995 fsk iikapewa mamlaka na kubadilishwa jina kuwa FSB, 1995 Rais akampa nafasi ya kwanza ya Ukurugenzi mkuu wao akawa askari mkakamvu mno General Mikhail ivanovich Barukov , hakutosha sana ndipo mwaka 1998 Mtaalamu wa mapigo ya karate na tai chi askari mtiifu mno Vladimir putin akawa Mkurugenzi Mkuu wa FSB akaleta mabadiliko makubwa kiutendaji na mfumo, nikosoe nilipoboronga mkuu
 
Ni kwa kutuma maombi.uwaeleze unataka kuwasaidia nini.na wala hawakuamini kiiivyo kukupa kazi nzito wakiona umewajua sana,mwisho wa siku ni.

Crush the bottle after using it.

Crush the bottle after using it, unamaanisha nn mkuu
 
Ni kwa kutuma maombi.uwaeleze unataka kuwasaidia nini.na wala hawakuamini kiiivyo kukupa kazi nzito wakiona umewajua sana,mwisho wa siku ni.

Crush the bottle after using it.

wanakupa mafunzo au vipi na maombi natuma wapi? nipe maelekezo mkuu
 
Crush the bottle after using it, unamaanisha nn mkuu
Hujaelewa nini hapa.ukiishatumika kwa suala flani wanakutelekeza au kukupoteza kabisa usijevujisha siri zao.rejea simulizi opp kamata osama.
wanakupa mafunzo au vipi na maombi natuma wapi? nipe maelekezo mkuu
Link katoa mdau huko post za nyuma, kwa sababu wewe ndiye umeona unalo la kuwasaidia, wewe ndiye utajua ujifunze kitu gani ili uhakikishe unawapa info zisizo na ukakasi, na pia informer sio lazima awe na mafunzo yoyote.

Na ukumbuke mafunzo ya hawa watu yanategemea anakwenda kufanya kazi gani.kama ni kudukua mifumo ya mawasiliano hawawezi peleka komandoo ataenda aliyebobea IT.
 
Hujaelewa nini hapa.ukiishatumika kwa suala flani wanakutelekeza au kukupoteza kabisa usijevujisha siri zao.rejea simulizi opp kamata osama.

Link katoa mdau huko post za nyuma, kwa sababu wewe ndiye umeona unalo la kuwasaidia, wewe ndiye utajua ujifunze kitu gani ili uhakikishe unawapa info zisizo na ukakasi, na pia informer sio lazima awe na mafunzo yoyote.

Na ukumbuke mafunzo ya hawa watu yanategemea anakwenda kufanya kazi gani.kama ni kudukua mifumo ya mawasiliano hawawezi peleka komandoo ataenda aliyebobea IT.
Mwambie akasome kitabu kinaitwa THE ART OF WAR by SUN TZU, atajifunza kuna aina kama Tano za SPY/Informer na Jinsi ya Kuwatumia.
(1) Local spies; (2) inward spies; (3) converted spies; (4) doomed spies; (5) surviving spies
LOCAL SPIES amsome huyu atapata mwanga.
 
Mmmaaa!!!, sifanyi kazi hizo, kazi gani hizo loooh si afadhali niendeleze biashara yangu niishi maisha bora na ya raha kabisa maana naona kama inatisha tisha looooh hata wakinifuata nakataa
 
Mmmaaa!!!, sifanyi kazi hizo, kazi gani hizo loooh si afadhali niendeleze biashara yangu niishi maisha bora na ya raha kabisa maana naona kama inatisha tisha looooh hata wakinifuata nakataa
Unaona sasa eh[emoji2]
 
Mwambie akasome kitabu kinaitwa THE ART OF WAR by SUN TZU, atajifunza kuna aina kama Tano za SPY/Informer na Jinsi ya Kuwatumia.
(1) Local spies; (2) inward spies; (3) converted spies; (4) doomed spies; (5) surviving spies
LOCAL SPIES amsome huyu atapata mwanga.
mkuu nifafanulie mmoja mmoja kati yao hao local ni nani na wanapatikanaje .God bless me i dont like dat job loooh
 
mkuu hivi hao watu wanajuana wote au wanaweza wasitambuane na kwann iwe hivyo kama hawajuani?.God bless me
[emoji2] kutokujuana ndio ufanisi wa kazi unayopewa.

Yaani unarudisha ripoti makao ya kitengo nchi uliyopo. unaambiwa urudi nchini kwako kwa rikizo ukaripoti ofisi flani,[emoji53] [emoji53] ghafla unakutana na jamaa ambaye alikupora begi stand ya basi likiwa na dokumenti zako ulizotumia kusafiria ile nchi ulikokuwepo[emoji2] ukamkimbiza bila mafanikio nayeye kaja kuripoti hapo.manabaki kushangaana.
 
Back
Top Bottom