Zijue nchi zenye waafrika wengi zaidi nje ya Afrika

aiseee sasa kizazi chao kikitoweka hao UN watanufaika na nanini !? kweli watu weusi tunachukiwa mnoo
 
Shida mademu wakiafrika ni vizinga na kutudharau sana sisi wanaume wa kiafrika
hahaaa njaa mkuu ..shida zimetamalaki mnoo Africa so usiwalaumu mnoo kuna ambapo tumekosea kuishi kimaadili kama taifa ..hili halipaswi kutazamwa kwa macho yakawaida
 
Kwa maisha hayo sioni kosa la Trump.
 
Hao walipelekwa wakati wa biashara ya utumwa mamia ya miaka iliyopita na siyo waafrika ni watu wa hizo nchi, kitu kingine usipende kuwaita watu wote weusi kuwa ni Waafrika
 
Brazili inamchanganyiko wa maraifa 11 mengine ni kama Italy, Spain, Japan, China, nk
 
Asikidanganye mtu, hao weusi wa marekani kwa kiasi fulani wanachukia sana kuhusishwa na bara la Africa. Ni kweli wapo very proud kuwa black. Wanaprefer kujiita blacks kuliko african americans. Halafu huwa wanabagua waafrika wanaoishi US.
Siyo kuwa wanabagua wao wamelelewa katika misingi ya kibepari we unapeleka ujamaa wako hauna nafasi kule
 
Wewe na wengine ndo mnakosea kuwaita Wao siyo Waafrika Bali ni weusi hivi wewe mtu akikuita Meuropean au Masia utamkubalia? Hata kama babu zako wanaasili ya huko?
 
Wewe na wengine ndo mnakosea kuwaita Wao siyo Waafrika Bali ni weusi hivi wewe mtu akikuita Meuropean au Masia utamkubalia? Hata kama babu zako wanaasili ya huko?
Hakuna sehemu niliyowaita waafrica sijui umenisoma wapi. Mstari wa kwanza wa paragraph uliyoninukuu nimesema "Hao ni watu weusi Basi sio waafrika"
 
Vipi kuhusu masuala ya elimu na teknolojia ya hawa waafrika wenzetu nje ya Africa. Naomba wenye kujuan vzuri suala la elimu yao watujuze hapa. Niliwahi kwenda Brazil na kuona huo ukweli kwamba ndiyo nchi yenye weusi wengi nje ya Africa i.e. ni nchi ya pili kuwa na weusi wengi baada ya Nigeria. Cha ajabu nilichoona ni kwamba weusi wamebaguliwa sana katika mfumo wao wa elimu kiasi kwamba ukiwa restaurant pale Rio, Brasilia utaona wahudumu wote ni weupe lakini ukipata mwanya wa kuangalia kule jikoni kwenye kazi ya sulba wote weusi. Ukienda benki humwoni mweusi. Subiri uende Copacabana jioni, wanaohangaika na mipira hadi ya mchangani ni weusi. Kwenye vyombo vya usalama utashangaa police wengi wa vyeo vya chini mitaani wanaotakiwa kupambana na magenge ya wahalifu hasa ya cocaine yaliyoenea kwenye 'Favelas" ( manzese za huko) ni weusi. Wale weipe wanakaa ofisini na tai zao kusubiri taarifa za matukio. Katika kiwanda cha kutengeneza ndege weusi hawaonekani kabisa.....orodha ni ndefu.
 

Mkuu Bufa,hawa wa kwenye msitu wa amazon si ndio red indians ama mayan ambao inasemekana kizazi chao kilipotea ingawa kabla idadi yao iliwahi kufikia hadi 13000.
 
Hali ya Brazil inasikitisha ila pia ni kwavile walichelewa sana kuacha utumwa. Ndio nchi ya mwisho kusitisha utumwa katika ukanda wa magharibi. Hii imewafanya watu weusi kuachwa nyuma sana hadi kuzaa hali waliyonayo leo.

Sent from my SM-J701F using JamiiForums mobile app
 
Brazili inamchanganyiko wa maraifa 11 mengine ni kama Italy, Spain, Japan, China, nk
huko SAHIHI kabisa. Mfano mzuri waliokuwa makocha was time ya Taifa Brazil Scolari anatrace asili yake Italy Na dunga anatrace asili yake Ujerumani
 
Kumbe wazungu wanaweza kumaliza kizazi cheusi kupitia intermarriage sasa tabu yanini? Wangekuja tuu wakazaa na sisi OVER!!!? KULIKO kutuletea Maebola na HIV yasiyo na mpango
 
Asikidanganye mtu, hao weusi wa marekani kwa kiasi fulani wanachukia sana kuhusishwa na bara la Africa. Ni kweli wapo very proud kuwa black. Wanaprefer kujiita blacks kuliko african americans. Halafu huwa wanabagua waafrika wanaoishi US.

Mkuu kwa Asilimia chache sana nakubaliana na wewe
 
Nikiwa Brazil Miaka ya 1940 kabla sijahamia Ufaransa Watu wenye Ngozi Nyeusi walikuwa wakipatikana zaidi ya asilimia 80 ya mitaa yote, kwa sasa nashangaa kuona idadi ikipungua kwa kasi.
 
Mimi nilidhani unazungumzia nchi za kiafrika zinazoongoza kwa kuwa na watu wengi nje ya nchi zao !
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…