Lord denning
JF-Expert Member
- Jun 3, 2015
- 15,819
- 33,255
1. Ni muumini mkubwa wa Katiba Mpya inayotengeneza mifumo imara na sio kuwapa nguvu Wanasiasa. Suala hili linaungwa mkono na idadi kubwa ya Watumishi wa Umma ikiwemo vyombo vya dola. Watendaji wengi Serikalini wamechoka kupelekeshwa na wanasiasa wanaofanya mambo kwa maslahi yao binafsi, hivyo wanataka mifumo imara ya kuwadhibiti wanasiasa.
2. Ni mtu anayechukia Rushwa sana na mkweli kupindukia. Kwa miongo kadhaa, CCM wamekuwa wakiendesha nchi kwa uongo hivyo ukweli wa Lissu unawatisha sana
3. Anakubalika na watu wa rika zote kutokana na uwezo wake kiakili na msimamo yake mizuri isiyoyumba. Wazee, Vijana na hadi watoto wadogo
4. Ni ushuhuda wa wazi wa uwepo wa nguvu za Mungu. Watanzania wengi wameanza kumjua Tundu Lissu akiwa sio mlemavu wa viungo. Ulemavu wa Lissu ulitokana na Shambulio alilofanyiwa na Uongozi wa Magufuli ambapo bila nguvu za Mungu asingepona. Leo hii wanavyomuona anatembea kwa kuchechemea huku akiwa na vyuma na risasi mwilini wanaamini kuwa huyu bila shaka ni mpakwa mafuta wa Mungu.
5. Lissu anakubalika na dini zote kuu nchini Tanzania yaani waislam na wakristo. Hii ni kwa sababu kwa uwazi kabisa Lissu amewatetea Wapalestina katika vita yao dhidi ya Israel na hii imefanya Waislam wengi kumuunga mkono. Kwa upande wa Wakristo Lissu ni Mkatoliki hasa.
6. Lissu ana amini sana kwenye soko huria na kutumia rasilimali tulizonazo kupata maendeleo kwa mfumo bora wa uwazi na haki. CCM hasa viongozi wake wanatumia vibaya sana rasilimali za Taifa kwa mambo ya ufisadi. Lissu anapinga haya na watu wengi wanamuunga mkono kwenye haya.
Mwisho Lissu ni muumini mahiri wa Tanganyika ambayo imefunikwa na koti la Muungano ambao kiukweli Watanzania wengi hawaupendi.