Pre GE2025 Zijue sababu 5 za kwanini Lissu ni hatari kwa CCM

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
1. Ni muumini mkubwa wa Katiba Mpya inayotengeneza mifumo imara na sio kuwapa nguvu Wanasiasa. Suala hili linaungwa mkono na idadi kubwa ya Watumishi wa Umma ikiwemo vyombo vya dola. Watendaji wengi Serikalini wamechoka kupelekeshwa na wanasiasa wanaofanya mambo kwa maslahi yao binafsi, hivyo wanataka mifumo imara ya kuwadhibiti wanasiasa.

2. Ni mtu anayechukia Rushwa sana na mkweli kupindukia. Kwa miongo kadhaa, CCM wamekuwa wakiendesha nchi kwa uongo hivyo ukweli wa Lissu unawatisha sana

3. Anakubalika na watu wa rika zote kutokana na uwezo wake kiakili na msimamo yake mizuri isiyoyumba. Wazee, Vijana na hadi watoto wadogo

4. Ni ushuhuda wa wazi wa uwepo wa nguvu za Mungu. Watanzania wengi wameanza kumjua Tundu Lissu akiwa sio mlemavu wa viungo. Ulemavu wa Lissu ulitokana na Shambulio alilofanyiwa na Uongozi wa Magufuli ambapo bila nguvu za Mungu asingepona. Leo hii wanavyomuona anatembea kwa kuchechemea huku akiwa na vyuma na risasi mwilini wanaamini kuwa huyu bila shaka ni mpakwa mafuta wa Mungu.

5. Lissu anakubalika na dini zote kuu nchini Tanzania yaani waislam na wakristo. Hii ni kwa sababu kwa uwazi kabisa Lissu amewatetea Wapalestina katika vita yao dhidi ya Israel na hii imefanya Waislam wengi kumuunga mkono. Kwa upande wa Wakristo Lissu ni Mkatoliki hasa.

6. Lissu ana amini sana kwenye soko huria na kutumia rasilimali tulizonazo kupata maendeleo kwa mfumo bora wa uwazi na haki. CCM hasa viongozi wake wanatumia vibaya sana rasilimali za Taifa kwa mambo ya ufisadi. Lissu anapinga haya na watu wengi wanamuunga mkono kwenye haya.

Mwisho Lissu ni muumini mahiri wa Tanganyika ambayo imefunikwa na koti la Muungano ambao kiukweli Watanzania wengi hawaupendi.
CCM lidude likubwa litishwe na Lissu ni vichekesho kama vichekesho vingine,subiri baada ya matokeo mtakavyolia lia
 
LISU hoyeeee!
Bibi Kizimkazi ziiiiii!!!!
 
CCM lidude likubwa litishwe na Lissu ni vichekesho kama vichekesho vingine,subiri baada ya matokeo mtakavyolia lia
Udude mkubwa wa CCM unachangiwa na hao watumishi wa umma na wa vyombo vya dola ambao wameichoka CCM.

Kama unasoma kwa kuelewa inabidi uogope
 
1. Ni muumini mkubwa wa Katiba Mpya inayotengeneza mifumo imara na sio kuwapa nguvu Wanasiasa. Suala hili linaungwa mkono na idadi kubwa ya Watumishi wa Umma ikiwemo vyombo vya dola. Watendaji wengi Serikalini wamechoka kupelekeshwa na wanasiasa wanaofanya mambo kwa maslahi yao binafsi, hivyo wanataka mifumo imara ya kuwadhibiti wanasiasa.

2. Ni mtu anayechukia Rushwa sana na mkweli kupindukia. Kwa miongo kadhaa, CCM wamekuwa wakiendesha nchi kwa uongo hivyo ukweli wa Lissu unawatisha sana

3. Anakubalika na watu wa rika zote kutokana na uwezo wake kiakili na msimamo yake mizuri isiyoyumba. Wazee, Vijana na hadi watoto wadogo

4. Ni ushuhuda wa wazi wa uwepo wa nguvu za Mungu. Watanzania wengi wameanza kumjua Tundu Lissu akiwa sio mlemavu wa viungo. Ulemavu wa Lissu ulitokana na Shambulio alilofanyiwa na Uongozi wa Magufuli ambapo bila nguvu za Mungu asingepona. Leo hii wanavyomuona anatembea kwa kuchechemea huku akiwa na vyuma na risasi mwilini wanaamini kuwa huyu bila shaka ni mpakwa mafuta wa Mungu.

5. Lissu anakubalika na dini zote kuu nchini Tanzania yaani waislam na wakristo. Hii ni kwa sababu kwa uwazi kabisa Lissu amewatetea Wapalestina katika vita yao dhidi ya Israel na hii imefanya Waislam wengi kumuunga mkono. Kwa upande wa Wakristo Lissu ni Mkatoliki hasa.

6. Lissu ana amini sana kwenye soko huria na kutumia rasilimali tulizonazo kupata maendeleo kwa mfumo bora wa uwazi na haki. CCM hasa viongozi wake wanatumia vibaya sana rasilimali za Taifa kwa mambo ya ufisadi. Lissu anapinga haya na watu wengi wanamuunga mkono kwenye haya.

Mwisho Lissu ni muumini mahiri wa Tanganyika ambayo imefunikwa na koti la Muungano ambao kiukweli Watanzania wengi hawaupendi.
Pamoja na kwamba huo ni mtazamo wako hujawahi kuwa na akili
 
Kweli sio wajinga na ndo mana wameanza kuiona CHADEMA kama chama kinachoweza kukamata dola
Nyie kwl nyumbu na mazuzu Hamna akili ht kdg. Chadema haiwezi kuchukua Dola nchi hii mpk vilembwe vyenu. Upinzani utakaochukua Dola utatoka ndani ya CCM yenyewe siyo hao vibaraka vya wazungu
 
Mwisho Lissu ni muumini mahiri wa Tanganyika ambayo imefunikwa na koti la Muungano ambao kiukweli Watanzania wengi hawaupendi.
Umemlisha maneno mengi....kwa kinywa chake Antipasu alisema vipaumbele vyake ni : Katiba Mpya, Tume huru ya Uchaguzi, Demokrasia, na Haki.

Lakini najiuliza; mbona hayasemi masuala ya :-

1. Maendeleo ya Kiuchumi kwa Kila mwananchi-Upatikanaji wa masoko ya bidhaa na huduma tunazozalisha hapa nchini,

2. Kudhibiti Mmomonyoko wa maadili katika jamii ( corruption and "social decay") kwa ngazi na kada zote, na

3. Ukuaji wa Teknolojia muhimu za kusaidia maendeleo ya wananchi.?

Ukitumia jicho la Tatu utagundua Antipasu ameishajiweka barabara kutimiza malengo ya wanyonyaji wetu wa ndani na WA nchi za Magharibi na mashirika ya Makubwa waitayo ya kiulimwengu wakati ni ya kwao. Wanyonyaji hawa huwezi kusikia Wana himiza sisi tutimize mambo matatu niliyoeleza hapo juu. Tukitimiza hayo, watalia njaa.

Kwa ufupi, Antipasu ni "mlaghai kama wengine" watumiwao na wanyonyaji wetu ndani ya Afrika. Si wa kumchekea kwenye mambo ya msingi.
 
Hivyo vipaumbele vyake kwa kifupi vikifanyika hayo mengine yote unayosema yatakaa sawa.
 
Nyie kwl nyumbu na mazuzu Hamna akili ht kdg. Chadema haiwezi kuchukua Dola nchi hii mpk vilembwe vyenu. Upinzani utakaochukua Dola utatoka ndani ya CCM yenyewe siyo hao vibaraka vya wazungu
Kibaraka wa wazungu kivipi? Acha kuongea ma utopolo humu. This is a forum of great thinkers
 
Hivyo vipaumbele vyake kwa kifupi vikifanyika hayo mengine yote unayosema yatakaa sawa.
Ndugu yangu, lazima uanze na haya kuyajadili ndipo utaweze kupanga Katiba Mpya, demokrasia, Haki vitawekwaje ili kukidhi vigezo vya kubeba hayo matatu tajwa.
Utatungaje Katiba Mpya bila kujua ni mazingira gani yatafaa kuimarisha hayo matatu!!! Na bila kuyajadili kwa kina, hatutagundua kama katiba iliyopo ni kweli haifai kuyawezesha hayo mambo matatu kuimarishwa ama la!!! Tuanze na haya matatu kwanza.
 
Back
Top Bottom