Wanabodi,
Nami niko hapa Dodoma Jiji kuhudhuria Mkutano Mkuu wa CCM.
Rais Samia katupiga bonge la surprise ya mwaka kututeulia Stephen Wasira kuwa M/Mwenyekiti CCM Bara!.
Wakati Comred Kinana aking'atuka, aliomba kupumzika, na kutoa sababu ni kupisha vijana, damu changa, damu chemka, kuendeleza kulisongesha.
Kinana ana umri wa miaka 71, the big surprise ni kama mtu mwenye umri wa miaka 71, ameachia nafasi ili kupisha damu changa, halafu anayeletwa kujaza nafasi hiyo ni mtu mwenye umri wa miaka 80!, hili ni bonge la surprise!.
Swali la kwanza kujiuliza ni Why Wasira?.
Kwa maoni yangu Stephen Wasira, he is the right man at the right time & the right place, who will do it right!. To me Wasira is a special project!, ikikamilika, na yeye atang'atuka kupumzika, just kama Kinana!.
Sababu pekee iliyomfanya Wasira kuteuliwa ni uwezo wake wa uelewa na anavyomwelewa Rais Samia, na uwezo wake wa kujieleza, na kuuelwzea umma Rais Samia anataka nini, hivyo uteuzi huu wa Wazira ni uteuzi wa kimkakati, kulikamilisha tuu lile jambo letu lile, likikamilika, na yeye pia atapumzika kama Kinana, sio lazima akamilishe miaka yote mitano!.
Swali la kwanza, je Wasira licha ya kuwa na umri wa miaka 80, hakuna ubishi kuwa Wasira ni Mzee, ila je amezeeka?. Kuna mtu kuwa na umri mkubwa na kuna mtu kuzeeka, sio kila mzee ni amezeeka, kuna wazee wana umri mkubwa lakini wako active kuliko vijana!.
Mimi na Wasira.
Mimi nimeingia newsroom Januari 2 1990, huu ni mwaka wangu wa 34, hivyo Wasira namfahamu sana tuu, ile siku anamtwanga makonde mwandishi Yasin Sadiki pale Maelezo, nilikuwepo!. Makonde hayo yakafanya tumpe jina la Stephen Tyson Wasira!.
Nilikuja kumfahamu vizuri na kwa karibu Stephen Wasira wakati nikiishi jijini New Delhi nchini India, Wasira akiwa katika moja ya ziara zake za kiserekali, alikuja India na kutembelea hapo nilipo na kuzungumza nae.
Baada ya kuondoka, kuna wadada watatu wa Kitanzania wakapiga umbeya, mmoja wa wadada hao akazungumzia sura yake, ndipo mdada mwingine akatumwagia ubuyu kuwa huyu jamaa yukp fit kweli kweli!, Bongo anagombaniwa, kuna watu wanapigana kwa ajili yake!, mara ghafla wale wadada nao wakaanza kumgombania!, hayo yeye hakuyajua!.
Hili za Uzee na kuzeeka, nilipokutana nae nilimuuliza swali kuhusu yeye kuzeeka.
View: https://youtu.be/UR6qPKMfZXw?si=a7BFb6YvGKVk40iM
Msikilize Hoja zake kumhusu Rais Samia
View: https://youtu.be/5kIid09GCqQ?si=b-wlN6bc7m_JMbz8
Ukiangalia vipindi hivi, ukaisikia michanga ya Steven Wasira, utakubaliana na mimi huyu ni mmoja wa viongozi wachache wanaioelewa vizuri na kikamilifu falsafa ya 4R za Samia, na nadhani ndizo sababu zilizo muibua mkongwe huyu kwa ule mchaka mchaka wa project ya lile jambo letu lile!.
Karibu
Paskali
Namalizia Shahada yangu ya Uzamivu, inayoangazia kwa namna gani IQ ya mtu inaweza athiriwa na umri. Bila shaka nawe utakuwa mfano hai katika kablasha langu, haiwezekani mtu unayejipambanua kuwa umeanza uandishi wa habari miaka ya 1990, na bado unaendelea kuandika MASHUDU