Zijue taratibu za kufuata ili kufungiwa umeme na TANESCO

Kuna walakini Sana kwenye kusubiri surveyor au funding wenu aje akague site. Mara kuchangia gari Mara like mko kiswahili Sana. Hakuna transparency.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tanesco Sometimes, mna mambo ya "Kipumbavu" in Mkapa's Voice.
Mie mkazi wa Chato.
Juzi nmekuwa geita mjini hadi sengerema, Eneo la Ibanda kuna nguzo nyingi sana zipo chini. Mtaa mzima hauna nyumba hata mia. Hizo zote hakuna hata aliye na uwezo wa kumiliki friji.
Geita Mjini mtaa wa Mwatulole secondary Nyumba nyingi hazina umeme ila watu wake wanahitaji umeme tena kwa gharama ya 321K,
Kasamwa ambapo ndio Center watu wamelipa umeme toka November last year hadi leo hawajawekewa, Nyankumbu , mbugani hakuna umeme japo ndio mji mpya , mmekimbilia mwabasabi.
Katoro mji wa kibiashara umeme upo mjini tu , Buseresere empty.

GEITA kuna tatizo , jichunguzeni.
Hongereni Tanesco Mwanza.
Jiji linapendeza Umeme hadi milimani.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Umeme Mwanza nguzo nazo tabu toka mwaka Jana tulipe usishangae taa kuwaka milimani usiku wengi Ni mobisol na Zola Ni wapuuzi tanesco mi muhanga kitambo
 
katika mashirika ya uma ya kipuuzi Tanesco linaweza kuwa la kwanza, mnahubiri viwanda kwa umeme upi?
 
Na hela tumelipa miezi tupo Gizani mh. Rais atupie jicho hi taasisi au TAKUKURU wafanye uchunguzi wake maana nguzo imekuwa ndo kisingizio
 
Asante sana mleta mada kwa uzi murua kabisa. Sina mengi ila naomba Moderators wabadilishe kidogo heading ya uzi. Badala ya ...".kufungiwa umeme"...isomeke ..."kuunganishiwa umeme"
 
Eneo?wilay? Namba ya simu tafadhali
 
Mnazingua sana nyinyi Tanesco, niliomba kufungiwa umeme nikazungushwa kwa zaidi ya miezi sita, mara ooh kuna wateja wengi yaani visababu kibao!
Na sababu kubwa ilikuwa ni wahusika kutengeneza mazingira ya rushwa...
Umeomba kwa jina gani? Namba ya sinu na wilaya yako tafadhali
 
Hivi ni vigezo vipi vinatumika kumuingizia umeme kwenye ile miradi ya REA?
Maana huku vijijini kama ukiritimba umezidi
maana mlivyorahisisha kwenye matangazo yenu kwenye TV eti elfu 23 tu,ila ukifuatilia ofisini kwenu hiyo gharama unaweza ukazimia
Kama ulipitia gharama halisi bei imekuwa 27000 tu kwa wakazi wa vijijini waliopo ndNi ya mita 30 kutoka kwenye nguzo zaidi ya hapo bei imebaki kama awali na makadirio ya gharama za kulipia unapewa kwa maandishi.wewe ulipewa kiasi gani? Namba ya simu na wilaya yako tunayaona yote kwenye mfumo wetu
 
Tunaomba namba yako ya simu, na eneo husika tafadhali
 
Nimeenda office ya Dodoma kadilisha Tariff three times naambiwa form zimeisha, nije siku nyingine nitakuta.
.
Mlifanyie kazi.
 
Nimeenda office ya Dodoma kadilisha Tariff three times naambiwa form zimeisha, nije siku nyingine nitakuta.
.
Mlifanyie kazi.
Tunaomba namba yako ya mita namba ya simu na eneo lako tafadhali
 
Ni kwanini kwa sasa ule utaratibu wa malipo ya elfu 9 kwa mwezi haupo?
 
Tunaomba namba yako ya mita namba ya simu na eneo lako tafadhali
Tanesco mtu anapotoa kero ni anawakilisha watu wengi. Ukweli watu wengi humu tunamalalamiko kuhusu tanesco na mengi au yote yanafanana hivyo shugulikieni hizo changamoto sio kwa mtu mmoja mmoja. Hiyo kuomba namba za simu za mteja inamaana mnamsaidia huyo tu mwenye uwezo wa kuja huku JamiiForums je wengine wasio na uwezo inakuaje?
 
Tunashukuru kwa uwakilishi wako lakini tambua kuwa kila mteja wetu ana account yake hivyo taarifa anazoulizia ni za kwake kwani matumizi ya umeme na mengine ni ya mtu sio kikundi ndio maana tunapenda kumsikiliza mteja moja kwa moja
 
Tunaomba namba yako ya simu, na eneo husika tafadhali

TANESCO nataka kujua kama mradi wa REA mwananchi anatakiwa kununua NGUZO MBILI Laki nne, ilihali wengine wanasogezewa. Naongelea Mradi wa REA wilayani Tarime, mji wa Nyamongo kijiji cha kewanja kitongoji cha kemambo
 
Tunashukuru kwa uwakilishi wako lakini tambua kuwa kila mteja wetu ana account yake hivyo taarifa anazoulizia ni za kwake kwani matumizi ya umeme na mengine ni ya mtu sio kikundi ndio maana tunapenda kumsikiliza mteja moja kwa moja
Asante kwa jibu. Lakini unajua watu wengi wanamalalamiko kama hayo lakini hawana uwezo au hawajui JamiiForums na kuleta shida zao hapa? Sehemu wanayoweza kwenda ni ofisi za tanesco maeneo yao na huko ndo kwenye shida hasa. Hivi kweli tanesco hamna nguzo kweli? Mfano mkoa wa mwanza maeneo ya kisesa ilo ndo limekua jibu lao kila siku na ukienda au ukipita ofisini kwao hapo kijereshi nguzo zipo za kutosha zinapigwa jua tu. Hivyo ombi la tulio wengi ni changamoto za kwenye ofisi na wafanyakazi zishugulikiwe tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…