Zijue taratibu za kufuata ili kufungiwa umeme na TANESCO

Zijue taratibu za kufuata ili kufungiwa umeme na TANESCO

Tunajibu wateja wetu kote karibu tukusikilize
Kule kwenye main thred sijui hampitii kusoma, huku ni kipengele kingine hakuhusiani na maswali na malalamiko yaliyotolewa kule, fungueni kule muone maswali na malalamiko yaliyotolewa tangu tarehe 12 mpaka leo hamjajibu.
 
Kule kwenye main thred sijui hampitii kusoma, huku ni kipengele kingine hakuhusiani na maswali na malalamiko yaliyotolewa kule, fungueni kule muone maswali na malalamiko yaliyotolewa tangu tarehe 12 mpaka leo hamjajibu.
Tupo tunaomba utupatie taarifa kamili na namba yako ya simu tafadhali
 
Tupo tunaomba utupatie taarifa kamili na namba yako ya simu tafadhali
Vipi ukinunua umeme namba zile za LUKU zinakaa muda gan bila kuharibika,, namaaninsha zinaexpire baada ya muda gani?
 
Vipi ukinunua umeme namba zile za LUKU zinakaa muda gan bila kuharibika,, namaaninsha zinaexpire baada ya muda gani?
Zinaandikaje ukiingiza na namba yako ya mita
 
Nataka nijue kwa sababu huku tulipanga umeme unakata mara kwa mara na tunalipa kwa mwez, soo nataka ninunue hadi wa mwez tisa sasa cjui utaexpire
Zinaandikaje ukiingiza na namba yako ya mita
 
Hapana ndugu mteja.
Nataka nijue kwa sababu huku tulipanga umeme unakata mara kwa mara na tunalipa kwa mwez, soo nataka ninunue hadi wa mwez tisa sasa cjui utaexpire
 
Unaweza lakn. Kati ya sasa na mwezi wa 9 unaweza kupata matitizo yafuatayo; Mita kuungua au kuharibika, Kupoteza token au kufutika kwa namba.n.k

Kwa ushauri mzuri. Ingependeza kusubiri na sio kununua kwa ajimi ya mwezi wa 9
Kwa hiyo nikinunua saiz nkaja kuuweka mwezi wa tisa hautaniletea shida
 
Kama nipo mita hamsini kutoka kijijini na Nina uwezo wa kununua nguzo je siwezi kuwa mnufaika wa mradi wa REA?
 
Unajifanya kusaidia watu Hanna chochote nilikupa malalamiko yangu wiki 3 zilizopita nikakufata na pm ukaniomba namba ya simu na wilaya vyote nilikupa lkn hakuna chochote ulichofanya, yaani kupata namba ya account ya bank ili kufanya Malipo tu ni Shida kila ukienda Mtandao unasumbua mpaka nimetoa Rushwa ya 20,000 ndo nimepewa account no ..kumbe Hanna cha mtandao kusumbua wala nn na we unalijua ili Dawa yenu iko Jikoni subirini
HATUA YA KWANZA

MAOMBI YA MWANZO

Je mteja anaweza kuchukua fomu ofisi yeyote ya tanesco?


Mteja anaweza kuchukua fomu ya maombi ya umeme katika ofisi yeyote ya shirika bila kujali kuwa eneo hilo linahudumiwa na ofisi husika. Ila atapaswa kurudisha ofisi ya maeneo ambayo makazi yake yapo ili kurahisisha kufanyiwa vipimo (service line survey)

JE KUNA GHARAMA ZOZOTE KATIKA UCHUKUAJI WA FOMU?

Fomu za maombi ya umeme zinatolewa bure kabisa kwa wateja wote.

VITU MUHIMU VYA KUZINGATIA WAKATI WA KUCHUKUA FOMU

1. Hakikisha umeme umefika maeneo yako na kama ni mradi uwe umekamilika.

2. Hakikisha mtandao wa nyaya ndani ya nyumba yako (wiring) umefanyika kupitia mkandarasi aliyesajiliwa.

3. Kitambulisho kinachomtambulisha muombaji wa umeme mfano leseni ya udereva, hati ya kusafiria, kitambulisho cha kazi (hii inasaidia shirika kumtambua mteja husika)

4. Kwa mwombaji wa mita ya ziada (meter separation) jina litakalotumika ni la mwenye nyumba kama linavyosomeka katika mita ya awali. Vinginevyo mteja atapaswa kutumia uthibitisho wa ruhusa ya mwenyenyumba kama atakuwa ni mpangaji. Lazima mteja aje na namba ya mita (kama zipo zaidi ya moja aje nazo zote) ili kuhakiki kama kuna yenye deni.


5. Kwa waombaji wanaomba kwa ajili ya ofisi, makapuni au taasisi za serikali au binafsi anapaswa kuja na leseni ya biashara, tin namba, udhibitisho wa usajili wa kampuni. Au udhibitisho wa ofisi ya serikali husika.

6. Kwa wapangaji wa nyumba za taasisi au makampuni waje na barua za waliopangisha zinazoonyesha kuwe wenye nyumba hizo wameridhia mita husika iwe na jina la mpangaji husika.

7. Shirika linapenda kuwaomba wamiliki wa nyumba kupenda kufika ofisi zetu wenyewe ili kuzuia udanganyifu ambao umekuwa ukifanywa na baadhi ya watu wasiokuwa waaminifu

HATUA YA PILI KUWEKA MCHORO, PICHA NA KUINGIA MAKUBALIANO YA KUFUNGIWA UMEME NAKUREJESHA FOMU

Endapo mteja atakidhi vigezo na masharti ya hatua ya mwanzo na kupatiwa fomu ya maombi ya mwanzo anatakiwa afanye yafuatayo

1. Kuisoma fomu kwa umakini mkubwa na kukubailiana na vigezo namba moja mpaka kumi na mbili. Mteja akijiridhisha kuwa amekubaliana na masharti yote ataweka sahihi sehemu husika (ukurasa wa pili wa fomu ya maombi ya umeme)

2. Kumpatia mkandarasi aliyesajiliwa ili achore mchoro wa mtandao wa nyaya (wiring diagram) wa nyumba husika pamoja na kugonga muhuri. (gharama ni makubaliano baina ya mteja na mkandarasi husika), wakandarasi wanapatikana kwenye ofisi zao maeneo mbalimbali, orodha ya waliosajiliwa pia inapatikana kwenye ofisi za tanesco. Mteja anapaswa kupewa orodha na kuchagua mkandarasi anayemtaka yeye.

3. Mteja atapaswa kuweka picha moja ya mwombaji wa umeme

4. Kisha mteja atarudisha fomu hiyo iliyokamilika ofisi ya eneo ambalo makazi yake yako (inayomudumia)

HATUA YA TATU- KUFANYIWA VIPIMO (SURVEY)

Mara baada ya mteja kurejesha fomu iliyojazwa kikamilifu, mteja atapangiwa tarehe ya kufanyiwa vipimo (survey). Mafundi watafika kwenye nyumba au sehemu inayoombewa umeme ili kutathimini gharama atakazolipia mteja kwa kuzingatia umbali wa eneo ilipo miundombinu ya umeme kama nguzo na transfoma na uwezo wa umeme huo kuunganisha kwa wateja wapya.

HATUA YA NNE: - KUPATIWA MAKADIRIO YA GHARAMA KIASI GANI ALIPE ILI AFUNGIWA UMEME

Mara baada ya kufanyiwa tathimini mteja anaweza kupatiwa makadirio ya gharama ya kiasi gani alipe ili kufungiwa umeme. Makadirio haya huweza kutumwa kwa njia ya nukushi, ujumbe mfupi wa meneno, barua pepe au mteja kufika ofisini na kuchukua barua. Viwango vya muda wa kutoa makadirio kama inavyoonekana kwenye jedwali hapo chini:

MAELEZO

Muda wa makadirio

Kama miundombinu iliyopo itatumika (ndani ya mita 30 kutoka kwenye nguzo iliyokaribu)

Ndani ya siku 7 za kazi

Ujenzi wa njia ya nyongeza unahitajika (mita 30- 100)

Ndani ya siku 10 za kazi

Kama mfumo mpya wa usambazaji unahitajika kujegwa au mfumo wa umeme mkubwa unahitajika kuongezwa kwa ajili ya kiwanda au biashara kubwa (kama hakuna mfumo wa kumuunganishia mwombaji) (zaidi ya mita 100)

Ndani ya siku 14 za kazi

HATUA YA TANO: - KUFANYA MALIPO

Mteja atafika ofisi ya tanesco ili kupatiwa namba ya kumbukumbu (reference number) itakayomuwezesha kufanya malipo bank, mteja atafanya malipo na atapatiwa stakabadhi ya malipo bank (risiti kwa njia ya ujumbe mfupi- sms) (kwa sasa ni bank ya nmb tu), wateja wanahimizwa kufanya malipo yote bank na si kwa mtu mwingine yeyote. Malipo yote yatakayofanyika nje ya mfumo uliwekwa hayatambulika na tanesco. Mteja akishafanya malipo bank husika hatatakiwa kurudi tena tanesco bali tanesco watakuwa na taarifa zake zote na kinachofuata ni kumfungia umeme.

HATUA YA SITA:-KUUNGANISHIWA UMEME

Mara baada ya mteja kufanya malipo viwango vya muda wa kumfungia umeme vitakuwa kama ilivyoonyeshwa kwenye jedwali hapo chini.

MAELEZO

Muda wa kufungiwa

Kama miundombinu iliyopo itatumika (ndani ya mita 30 kutoka kwenye nguzo iliyokaribu)

Ndani ya siku 30 za kazi

Ujenzi wa njia ya nyongeza itahitajika

(mita 30- 100)

Ndani ya siku 60 za kazi

KAMA MFUMO MPYA WA USAMBAZAJI UNAHITAJIKA KUJEGWA AU MFUMO WA UMEME MKUBWA UNAHITAJIKA KUONGEZWA KWA AJILI YA KIWANDA AU BIASHARA KUBWA (KAMA HAKUNA MFUMO WA KUMUUNGANISHIA MWOMBAJI) (ZAIDI YA MITA 100)

Ndani ya siku 90 za kazi

KWA MAULIZO WASILIANA NASI

Kituo cha huduma kwa wateja: - 0768985100/0222194400

Barua pepe: customer.Service@tanesco.Co.Tz

Facebook: www.Facebook.Com/tanesco yetu

Twitter: - www.Twitter.Com/tanesco yetu

Tovuti; www.Tanesco.Co.Tz
 
Unajifanya kusaidia watu Hanna chochote nilikupa malalamiko yangu wiki 3 zilizopita nikakufata na pm ukaniomba namba ya simu na wilaya vyote nilikupa lkn hakuna chochote ulichofanya, yaani kupata namba ya account ya bank ili kufanya Malipo tu ni Shida kila ukienda Mtandao unasumbua mpaka nimetoa Rushwa ya 20,000 ndo nimepewa account no ..kumbe Hanna cha mtandao kusumbua wala nn na we unalijua ili Dawa yenu iko Jikoni subirini
Tunaomba taarifa yako kamili na huduma uliyoomba. Kama kuna mfanyakazi uliyempa rushwa ni kosa tafadhali tumia njia sahihi kupata huduma bila rushwa
 
Kama nipo mita hamsini kutoka kijijini na Nina uwezo wa kununua nguzo je siwezi kuwa mnufaika wa mradi wa REA?
Ukishachukua fomu ya maombi ya umeme tunakupimia na kukupa makadirio ya kiasi halisi cha kulipia kutokana na vifaa vinavyohitajika kukufungia umeme
 
Back
Top Bottom