Zijue taratibu za kufuata ili kufungiwa umeme na TANESCO

Tafadhali tambua kuwa zipo taarifa za mtu binafsi hizi zinatolewa na mteja mwenye kutaka huduma fulani kwenye makazi yake au taarifa za wengi pale ambapo kuna ombi au tatizo la eneo kubwa. Hivyo ikiwa taarifa inakuhusu wewe mwenyewe toa kwetu huku ukionyesha taarifa kamili kwa kuwa taarifa za kila mteja zipo kwenye mfumo wetu
 
Nimekuelewa mkuu. Hongera kwa kazi nzuri
 
Jina lako, Wilaya na namba ya simu tafadhali
 
Habari..hapo kwenye hatua ya TANO ya kufanya Malipo ndio tumekwama ni Wiki ya pili ka sio ya tatu kila tukieenda ofisn kwenu tunaambiwa Mtandao unasumbua yaani tatizo ni kutoa account namba yenu ya CRDB ili tuweze kufanya malipo kila tukienda mtandao unasumbua hii ni kweli au wanataka tutoe Rushwa, Nyumba iko Tabata Kisukuru .
 
Sio kweli, meter inahamishika ila iwe within same district
 
Nimesikia kuwa katika mkoa wa kilimanjaro wilaya ya moshi vijijini, marangu, samanga kuna ofa ya kuunganishiwa umeme kwa Tshs. 27000/= ikiwa nguzo iko ndani ya mita 30. Je ni kweli kuna ofa hiyo?

Pili naomba maelekezo ya kurudishwa tarif 1 maana nimeshajaza fomu na ni miezi 3 sasa hawajaja kukagua luku ili kujiridhisha.
 
Maeneo gani hua mnapanga kwamba hapa itapita phase I au III, kigezo ni kipi ili upate phase III?
 
Unaomba jina la wilaya unadhani,utasaidia chochote,acheni porojo zenu za kutesa watu,yaani kuwasha umeme ndani ya mita 20( nguzo tayari) ndiyo ichukue miezi 3, kwendeni uko ,tumewachoka sana.
Tupo tayari kukusikiliza na kukuhumia mpendwa mteja wetu
 
Muda mnaochukua kufungia wateja umeme ni mrefu sana mimi nina miezi miwili tangu nilipie lakini hakuna dalili ya kuja kufungiwa ndio wanasema wamewafikia wateja wa mwezi wa 11/2018 sasa tuliolipia mwaka 2019 tutafikiwa 2021au
 
Inaelezwa kuwa kuna UTATU MTSKATIFU wa kuingiza majumbani umeme wa REA:
1. REA, mlipiaji wa gharama za miradi ya usambazaji wa umeme vijijini,
2. WAKANDARASI, watandaza nyanya, na
3. TANESCO, wasimamiji wa miradi sehemu husika.
Nguzo za nyaya za umeme usiopoozwa zimepitishwa uwanjani kwangu. Miti yangu mingi ilikatwa ili kuwezesha nguzo kujengewa. Nilikubali hiyo gharama nikiamini ningeneemeka kwa kupata huduma ya umeme.
Mkandarasi ameruka kitongoji changu kwenye kutandaza nguzo za nyaya za kuingiza umeme kwenye nyumba zetu.
* TANESCO wanatuambia hakuna cha mradi mwingine wa REA; II wala III.
* Wananchi wa kijiji cha Bisarwi, Manga, Tarime, hali zetu ni duni. Hatuna uwezo wa kulipia gharama ya mamilioni za maombi ya mradi wa kuwezesha kupata umeme:
(a) dhana ya umeme wa gharama nafuu iko wapi?
(b) kwanini tumekuwa wahanga wakati kama shirika, ofisi yenu ya wilaya haikusimamia ipasavyo utelekezaji wa mradi wa REA? Ushaidi:
- transfoma zilizowekwa ama ni ndogo, mbovu, au zilikuwa chache ikilinganishwa na mahitaji.
- ndiyo maana mkalazimika kibadikisha baadhi baada ya kulipuka, na
- kazi chini ya kiwango. Nimeshuhudia TANESCO wakirekebisha baadhi ya dosari kama kufunga earthwire.
Najiuliza: hapakuwepo na kipengele cha muda wa matazamio ya mradi kama Sheria ya Manunuzi ya Umma inavyotaka?
Sijapata muda wa kutosha kufuatilia suala hili.
 
Changamoto ni kitengo cha kupima, surveyor ni wachache mno kulinganisha na waitaji wa huduma hiyo. Waweza kaa hadi miezi miwili hujapimiwa. All in all asanteni kwa elimu
 
Dah Huo ujasiri wa tanesco nimeukubali..hii ni roho ya kisomali kabisa, umepata ujasiri wa kujibu kero za Tanesco, Tanesco mnakera sana nyie watu nahisi hata wafanyakazi hampati neema sababu ya laana za wananchi...Mimi kuna nguzo ipo pembeni ya duka langu...nimeomba mita mwezi wa pili sasa...duka lenyewe vyumba viwili tu..watu wakufanya survey ndio kila siku wanakuja j3...yaani j3 usipopitiwa imekula kwako....sasa najiuliza, inamaana hawa jamaa wanafanya kazi jumatatu tu? (kama una meter ya magendo sema nikupe hela uje unifungie tu..bila hivyo mwaka utaisha)
 
Jamaa anavyojibu kiutaratibu humu ni kama ndiyo walivyo field?watu wa hovyo sana hawa
 
Tangu tarehe 12 watu wanauliza maswali hawajibiwi, leo tarehe 21 mko kimya tu.

Watu wameuliza maswali wanahitaji msaada ila hamtaki kujibu mko kimya tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…