Zijue taratibu za kufuata ili kufungiwa umeme na TANESCO

Wafikishie na hili kwa kweli Tanesco huku kwetu vunjo kuna maeneo mnatukera kama sio kuboa badilisheni mfumo au muongeze transifoma manake yaliyopo yana zaidi ya karne na yanahudumia sehemu kubwa kwa kweli ni kero
tafadhali Eng_CNT je wewe umewahi kupata tatizo hilo? kama sawa je ulipata mkoa,wilaya gani?
 
Samahani. Je distance kati ya nguzo na nguzo ni meter ngapi?

Na Range ya distance isiyo hitaji nguzo ni ipi?
Service lin zimegawanyika

1. Njia moja/tatu ndani ya mita 30 (bila nguzo)
2. Njia moja/tatu nguzo moja ndani ya mita sabini
3. Njia moja/tatu nguzo mbili ndani ya mita 120

Ikizidi hapo basi inakuwa mfumo wa mradi na gharama zake ni mpaka estimates zifanyike.

Kuhusu distance kati ya nguzo na nguzo maximum ni 50meters lakini kuna some exceptions (hapa naongelea masuala ya engineering) na inategemea mazingira yalivyo site.

Kwasisi wateja tunaweza kuona kwa macho yetu kuwa labda ni umbali fulani na kukadiria idadi ya nguzo kitu ambacho ni makosa.

Kujua vyote hivyo inatakiwa usubiri mtaalamu wa TANESCO afike site nakufanya vipimo.
 
Hongereni je kureplce luku ya zamani yenye hitilafu upate mpya ni bei
 
uandishi gani huu? pumbavu kabisa
 
Asante
 
Asante sana Tanesco.Nataka kufahamu gharama za kulipia three phase bila nguzo ni bei gani.
 
Hongereni je kureplce luku ya zamani yenye hitilafu upate mpya ni bei
Kama ina hitilafu ku replace inatagemea na situation.

Fundi mkaguzi wa mita akifika site na kukagua mita ndio atagundua hiyo itilafu umesababisha mteja au sio.

Kama sio wewe uliyesababisha basi kubadili ni bure ila kama ni wewe basi utalipa gharama za kuweka nyingine
 
]Kuwa mvumilivu mkuu, utapata umeme soon. Chamuhimu epuka vishoka ambao wanaharibu taswira ya Tanesco kwa kutapeli wateja, usitoe hela yako kwa cash, mpesa au tigo pesa. Malipo yote halali yanafanyika bank na unapata receipt.
Unasema tunalipa bank,mbona Tanesco Tarime tunaelekezwa kulipa Kwa mhasibu palepale ofisini kwenu ?
Au ndo nimeliwa!!! LAKINI walinipa receipt.ebu msaada hapo.
 
Mimi naomba MSAADA wa Maelezo kuhusu zile mita ndogo ambazo unaweza kufungiwa chumbani kwako.
Kwani tupo wapangaji wengi na mimi sina matumizi mengi, najikuta nalipa hela wakati sina matumizi mengi.
Naomba kufahamu
1-zinapatikana kwa kutumia utaratibu upi?
2-zinapatikana kwa sh.ngapi,
3-ninaweza pata baada ya mda gani??? MSAADA wenu tafadhali
 
Hizo meter hazitolewi na TANESCO bali zinauzwa kwenye hardwares na bei yake binafsi sifahamu.

Otherwise ukitaka kuwekewa meter ya TANESCO unaomba huduma ya kufungiwa umeme kama kawaida na utafungiwa meter yako peke yako.

Gharama ni 320,960/- kwa single phase maeneo ya mijini, kwa maeneo ya kijijini ni 177,000/-

Kama ni meter ya three phase basi ni 912,013.74/-
 
Mkuu ili kufungiwa umeme kuna vifaa vinahitajika hivyo kukiwa na upungufu wa hata material ya aina moja huwezi kufungiwa mpaka yakamilike hivyo Tanesco nao wanapenda kupata wateja wapya ili shirika lipate mapato na sio kwamba wanachelewesha makusudi
ukifanyiwa survey wakakupa Go Ahead ni kwambaumemaliza kila kitu ndo maana unaruhusiwa kulipia garama

hii proccess yote nilimaliza mkuu
 
Asante. Mimi nataka hivyo. Najua hata nikihama ntahama nacho
 
Asante sana Tanesco.Nataka kufahamu gharama za kulipia three phase bila nguzo ni bei gani.
Ni Tsh 912000,Makadirio haya utapatiwa baada ya kufanyiwa vipimo (survey)
 


Hapo nawa disqualify kabisa
 
Nasubiri Survey week ya 2 sasa ubungo Kibo,mchoro tayari nasubiri Survey niwalipe
 
Sasa mkuu katika hizi nyumba tunazopanga huwa na kero sana kwa upande kulipia luku kama Tanesco wanatusaidia vipi kupata mita ambazo nikwaajili ya matumizi chini ya Units 01-75. Kwasababu wapo baadhi ya wapangaji wagumu kulipia luku.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…