Zijue taratibu za kufuata ili kufungiwa umeme na TANESCO

Zijue taratibu za kufuata ili kufungiwa umeme na TANESCO

Tunashukuru kuna maeneo kule moshi vijijini ambayo yalibahatika kuwa na umeme tooka enzi za mwalimu na kila uchwao kule nyumba zinajengwa na mahitaji ya umeme kuongezeka sasa mdau kero yake inakuja baadhi ya maeneo ambayo nimeshuhudia kwa macho yangu umeme wake ule mwanga ni bora uwashe chemli au mshumaa yaani ni mdogo tena unaumiza macho tena ikifika majira ya jioni ambapo uhitaji huongezeka ukiwasha taa zingine haziwaki kabisa tembeleeni huko vijijini hasa vunjo mkajionee
Wafikishie na hili kwa kweli Tanesco huku kwetu vunjo kuna maeneo mnatukera kama sio kuboa badilisheni mfumo au muongeze transifoma manake yaliyopo yana zaidi ya karne na yanahudumia sehemu kubwa kwa kweli ni kero
tafadhali Eng_CNT je wewe umewahi kupata tatizo hilo? kama sawa je ulipata mkoa,wilaya gani?
 
Samahani. Je distance kati ya nguzo na nguzo ni meter ngapi?

Na Range ya distance isiyo hitaji nguzo ni ipi?
Service lin zimegawanyika

1. Njia moja/tatu ndani ya mita 30 (bila nguzo)
2. Njia moja/tatu nguzo moja ndani ya mita sabini
3. Njia moja/tatu nguzo mbili ndani ya mita 120

Ikizidi hapo basi inakuwa mfumo wa mradi na gharama zake ni mpaka estimates zifanyike.

Kuhusu distance kati ya nguzo na nguzo maximum ni 50meters lakini kuna some exceptions (hapa naongelea masuala ya engineering) na inategemea mazingira yalivyo site.

Kwasisi wateja tunaweza kuona kwa macho yetu kuwa labda ni umbali fulani na kukadiria idadi ya nguzo kitu ambacho ni makosa.

Kujua vyote hivyo inatakiwa usubiri mtaalamu wa TANESCO afike site nakufanya vipimo.
 
Hongereni je kureplce luku ya zamani yenye hitilafu upate mpya ni bei
 
Tanesco nyiee bhana mnachelewesheaa sana kuwawekeaa watu umeme pindi mtu anapoitaji na anakuwa ameshalipaa kilaa kituu..ilaa mtamzungushaa weeee nakumtumiaa SMS za samahani mpk mtu uzalendo unampitaa ...jirani yangu hapa kalipiaa mwaka Jana nguzo pamoja na kujaa kufungiwa cha ajabu n mwezii wa sita sasa unaendaa anaambiwa nguzo zimeishaa ...jaman ktk miezi sita yote hyo amjaagizaa nguzoo tu uko zilipoo na kila cku naonaa garii ikipitaa na nguzoo.n kwann inatokeaa hvyoo ndugu zangu tanesco ..kumzungusha mtejaa wenu hvyooo.na si MTU wa kwanza kumshuhudiaa mkimzungushaa n wawilii watatuu
Na jamaa wakatakaa rushwaa akawapaa lakii na nusuu cha ajabu waonaa sijui ukaribuu wakumfungia mapema haupo wakamrudishiaa hela ilee aliyotoaa rushwa ..kiujumlaa jamaa kakataa tamaa na anataman hela yake irudishwe akae Giza lkn wanampa matumani...mm lukuu ilizinguaa tu nikatakiwaa kuwekaa mpyaa nikaendaa lipaa lakin cha moto nilikionaa nusuraa wapangaji wanitoee rohoo...tokaa mwaka Jana mwezi wa kumi na mbili mwakaa Jana imekujaa fungwaa mwezi wa pilii...nilijutaa...kiujumlaa tanesco hampoo makinii hataa kidogoo badoo hamwendii na kasii ya sasaaa...
uandishi gani huu? pumbavu kabisa
 
HATUA YA KWANZA-:- MAOMBI YA MWANZO

Je mteja anaweza kuchukua fomu ofisi yeyote ya tanesco?

Mteja anaweza kuchukua fomu ya maombi ya umeme katika ofisi yeyote ya shirika bila kujali kuwa eneo hilo linahudumiwa na ofisi husika. Ila atapaswa kurudisha ofisi ya maeneo ambayo makazi yake yapo ili kurahisisha kufanyiwa vipimo (service line survey)

JE KUNA GHARAMA ZOZOTE KATIKA UCHUKUAJI WA FOMU?

Fomu za maombi ya umeme zinatolewa bure kabisa kwa wateja wote.

VITU MUHIMU VYA KUZINGATIA WAKATI WA KUCHUKUA FOMU

1. Hakikisha umeme umefika maeneo yako na kama ni mradi uwe umekamilika.

2. Hakikisha mtandao wa nyaya ndani ya nyumba yako (wiring) umefanyika kupitia mkandarasi aliyesajiliwa.

3. Kitambulisho kinachomtambulisha muombaji wa umeme mfano leseni ya udereva, hati ya kusafiria, kitambulisho cha kazi (hii inasaidia shirika kumtambua mteja husika)

4. Kwa mwombaji wa mita ya ziada (meter separation) jina litakalotumika ni la mwenye nyumba kama linavyosomeka katika mita ya awali. Vinginevyo mteja atapaswa kutumia uthibitisho wa ruhusa ya mwenyenyumba kama atakuwa ni mpangaji. Lazima mteja aje na namba ya mita (kama zipo zaidi ya moja aje nazo zote) ili kuhakiki kama kuna yenye deni.


5. Kwa waombaji wanaomba kwa ajili ya ofisi, makapuni au taasisi za serikali au binafsi anapaswa kuja na leseni ya biashara, tin namba, udhibitisho wa usajili wa kampuni. Au udhibitisho wa ofisi ya serikali husika.

6. Kwa wapangaji wa nyumba za taasisi au makampuni waje na barua za waliopangisha zinazoonyesha kuwe wenye nyumba hizo wameridhia mita husika iwe na jina la mpangaji husika.

7. Shirika linapenda kuwaomba wamiliki wa nyumba kupenda kufika ofisi zetu wenyewe ili kuzuia udanganyifu ambao umekuwa ukifanywa na baadhi ya watu wasiokuwa waaminifu

HATUA YA PILI KUWEKA MCHORO, PICHA NA KUINGIA MAKUBALIANO YA KUFUNGIWA UMEME NAKUREJESHA FOMU

Endapo mteja atakidhi vigezo na masharti ya hatua ya mwanzo na kupatiwa fomu ya maombi ya mwanzo anatakiwa afanye yafuatayo

1. Kuisoma fomu kwa umakini mkubwa na kukubailiana na vigezo namba moja mpaka kumi na mbili. Mteja akijiridhisha kuwa amekubaliana na masharti yote ataweka sahihi sehemu husika (ukurasa wa pili wa fomu ya maombi ya umeme)

2. Kumpatia mkandarasi aliyesajiliwa ili achore mchoro wa mtandao wa nyaya (wiring diagram) wa nyumba husika pamoja na kugonga muhuri. (gharama ni makubaliano baina ya mteja na mkandarasi husika), wakandarasi wanapatikana kwenye ofisi zao maeneo mbalimbali, orodha ya waliosajiliwa pia inapatikana kwenye ofisi za tanesco. Mteja anapaswa kupewa orodha na kuchagua mkandarasi anayemtaka yeye.

3. Mteja atapaswa kuweka picha moja ya mwombaji wa umeme

4. Kisha mteja atarudisha fomu hiyo iliyokamilika ofisi ya eneo ambalo makazi yake yako (inayomudumia)

HATUA YA TATU- KUFANYIWA VIPIMO (SURVEY)

Mara baada ya mteja kurejesha fomu iliyojazwa kikamilifu, mteja atapangiwa tarehe ya kufanyiwa vipimo (survey). Mafundi watafika kwenye nyumba au sehemu inayoombewa umeme ili kutathimini gharama atakazolipia mteja kwa kuzingatia umbali wa eneo ilipo miundombinu ya umeme kama nguzo na transfoma na uwezo wa umeme huo kuunganisha kwa wateja wapya.

HATUA YA NNE: - KUPATIWA MAKADIRIO YA GHARAMA KIASI GANI ALIPE ILI AFUNGIWA UMEME

Mara baada ya kufanyiwa tathimini mteja anaweza kupatiwa makadirio ya gharama ya kiasi gani alipe ili kufungiwa umeme. Makadirio haya huweza kutumwa kwa njia ya nukushi, ujumbe mfupi wa meneno, barua pepe au mteja kufika ofisini na kuchukua barua. Viwango vya muda wa kutoa makadirio kama inavyoonekana kwenye jedwali hapo chini:

MAELEZO

Muda wa makadirio

Kama miundombinu iliyopo itatumika (ndani ya mita 30 kutoka kwenye nguzo iliyokaribu)

Ndani ya siku 7 za kazi

Ujenzi wa njia ya nyongeza unahitajika (mita 30- 100)

Ndani ya siku 10 za kazi

Kama mfumo mpya wa usambazaji unahitajika kujegwa au mfumo wa umeme mkubwa unahitajika kuongezwa kwa ajili ya kiwanda au biashara kubwa (kama hakuna mfumo wa kumuunganishia mwombaji) (zaidi ya mita 100)

Ndani ya siku 14 za kazi

HATUA YA TANO: - KUFANYA MALIPO

Mteja atafika ofisi ya tanesco ili kupatiwa namba ya kumbukumbu (reference number) itakayomuwezesha kufanya malipo bank, mteja atafanya malipo na atapatiwa stakabadhi ya malipo bank (risiti kwa njia ya ujumbe mfupi- sms) (kwa sasa ni bank ya nmb tu), wateja wanahimizwa kufanya malipo yote bank na si kwa mtu mwingine yeyote. Malipo yote yatakayofanyika nje ya mfumo uliwekwa hayatambulika na tanesco. Mteja akishafanya malipo bank husika hatatakiwa kurudi tena tanesco bali tanesco watakuwa na taarifa zake zote na kinachofuata ni kumfungia umeme.

HATUA YA SITA:-KUUNGANISHIWA UMEME

Mara baada ya mteja kufanya malipo viwango vya muda wa kumfungia umeme vitakuwa kama ilivyoonyeshwa kwenye jedwali hapo chini.

MAELEZO

Muda wa kufungiwa

Kama miundombinu iliyopo itatumika (ndani ya mita 30 kutoka kwenye nguzo iliyokaribu)

Ndani ya siku 30 za kazi

Ujenzi wa njia ya nyongeza itahitajika

(mita 30- 100)

Ndani ya siku 60 za kazi

KAMA MFUMO MPYA WA USAMBAZAJI UNAHITAJIKA KUJEGWA AU MFUMO WA UMEME MKUBWA UNAHITAJIKA KUONGEZWA KWA AJILI YA KIWANDA AU BIASHARA KUBWA (KAMA HAKUNA MFUMO WA KUMUUNGANISHIA MWOMBAJI) (ZAIDI YA MITA 100)

Ndani ya siku 90 za kazi

KWA MAULIZO WASILIANA NASI

Kituo cha huduma kwa wateja: - 0768985100/0222194400

Barua pepe: customer.Service@tanesco.Co.Tz

Facebook: www.Facebook.Com/tanesco yetu

Twitter: - www.Twitter.Com/tanesco yetu

Tovuti; www.Tanesco.Co.Tz
Asante
 
Asante sana Tanesco.Nataka kufahamu gharama za kulipia three phase bila nguzo ni bei gani.
 
Hongereni je kureplce luku ya zamani yenye hitilafu upate mpya ni bei
Kama ina hitilafu ku replace inatagemea na situation.

Fundi mkaguzi wa mita akifika site na kukagua mita ndio atagundua hiyo itilafu umesababisha mteja au sio.

Kama sio wewe uliyesababisha basi kubadili ni bure ila kama ni wewe basi utalipa gharama za kuweka nyingine
 
]Kuwa mvumilivu mkuu, utapata umeme soon. Chamuhimu epuka vishoka ambao wanaharibu taswira ya Tanesco kwa kutapeli wateja, usitoe hela yako kwa cash, mpesa au tigo pesa. Malipo yote halali yanafanyika bank na unapata receipt.
Unasema tunalipa bank,mbona Tanesco Tarime tunaelekezwa kulipa Kwa mhasibu palepale ofisini kwenu ?
Au ndo nimeliwa!!! LAKINI walinipa receipt.ebu msaada hapo.
 
Mimi naomba MSAADA wa Maelezo kuhusu zile mita ndogo ambazo unaweza kufungiwa chumbani kwako.
Kwani tupo wapangaji wengi na mimi sina matumizi mengi, najikuta nalipa hela wakati sina matumizi mengi.
Naomba kufahamu
1-zinapatikana kwa kutumia utaratibu upi?
2-zinapatikana kwa sh.ngapi,
3-ninaweza pata baada ya mda gani??? MSAADA wenu tafadhali
 
Mimi naomba MSAADA wa Maelezo kuhusu zile mita ndogo ambazo unaweza kufungiwa chumbani kwako.
Kwani tupo wapangaji wengi na mimi sina matumizi mengi, najikuta nalipa hela wakati sina matumizi mengi.
Naomba kufahamu
1-zinapatikana kwa kutumia utaratibu upi?
2-zinapatikana kwa sh.ngapi,
3-ninaweza pata baada ya mda gani??? MSAADA wenu tafadhali
Hizo meter hazitolewi na TANESCO bali zinauzwa kwenye hardwares na bei yake binafsi sifahamu.

Otherwise ukitaka kuwekewa meter ya TANESCO unaomba huduma ya kufungiwa umeme kama kawaida na utafungiwa meter yako peke yako.

Gharama ni 320,960/- kwa single phase maeneo ya mijini, kwa maeneo ya kijijini ni 177,000/-

Kama ni meter ya three phase basi ni 912,013.74/-
 
Mkuu ili kufungiwa umeme kuna vifaa vinahitajika hivyo kukiwa na upungufu wa hata material ya aina moja huwezi kufungiwa mpaka yakamilike hivyo Tanesco nao wanapenda kupata wateja wapya ili shirika lipate mapato na sio kwamba wanachelewesha makusudi
ukifanyiwa survey wakakupa Go Ahead ni kwambaumemaliza kila kitu ndo maana unaruhusiwa kulipia garama

hii proccess yote nilimaliza mkuu
 
Hizo meter hazitolewi na TANESCO bali zinauzwa kwenye hardwares na bei yake binafsi sifahamu.

Otherwise ukitaka kuwekewa meter ya TANESCO unaomba huduma ya kufungiwa umeme kama kawaida na utafungiwa meter yako peke yako.

Gharama ni 320,960/- kwa single phase maeneo ya mijini, kwa maeneo ya kijijini ni 177,000/-

Kama ni meter ya three phase basi ni 912,013.74/-
Asante. Mimi nataka hivyo. Najua hata nikihama ntahama nacho
 
Asante sana Tanesco.Nataka kufahamu gharama za kulipia three phase bila nguzo ni bei gani.
Ni Tsh 912000,Makadirio haya utapatiwa baada ya kufanyiwa vipimo (survey)
 
Wapuuzi kabisa mkuu, wamepitisha main line eneo yalipo makazi yangu leo mwaka wa tano hawataki kutandaza nyaya ndogo lakini badala wameenda kutandaza eneo la mbele.

Yaan assume starting point ni A then unaenda B, C, D etc sasa wao wameenda kutandaza point D na kuruka B na C. Hapa utawaelewa?


Hapo nawa disqualify kabisa
 
Nasubiri Survey week ya 2 sasa ubungo Kibo,mchoro tayari nasubiri Survey niwalipe
 
Sasa mkuu katika hizi nyumba tunazopanga huwa na kero sana kwa upande kulipia luku kama Tanesco wanatusaidia vipi kupata mita ambazo nikwaajili ya matumizi chini ya Units 01-75. Kwasababu wapo baadhi ya wapangaji wagumu kulipia luku.
 
Back
Top Bottom