Zijue taratibu za kufuata ili kufungiwa umeme na TANESCO

Zijue taratibu za kufuata ili kufungiwa umeme na TANESCO

Mtoa mada naomba unisaidie. Kuna jirani yangu kaunganishiwa umeme. Lakini huo waya unaoenda kwa jirani yangu, nikisimama kwenye varanda maeneo ya jikoni, nakuwa na uwezo wa kuushika waya huo maana mimi niko kwenye mwinuko na huyo jirani yangu yuko bondeni. Hivi karibuni nilimkuta msichana wa kazi kaanika nguo juu ya waya huo wa umeme unaoelekea kwa jirani yangu. Je, hii ni sahihi? Maana naona kama inatishia usalama wangu.
 
Sio sahihi dada, na walipokuwa wanavuta huo waya wewe haukuona?

Chakufanya andika barua kwa kwenda kwa manager wa Tanesco sehemu uliyopo ili kuangalia namna ya kuondoa huo waya sehemu hatarishi
 
tanesco mda mwingine mnasema uongo, sijui kama mmebadilika au la!!!

mwaka jana, eneo langu ilikua karibu na nguzo mita 15 ila imechukua hadi siku 60 baada ya kufanya malipo,

ni kwamba mmejirekebisha au ni kuridhisha umati,

asante
Mkuu ili kufungiwa umeme kuna vifaa vinahitajika hivyo kukiwa na upungufu wa hata material ya aina moja huwezi kufungiwa mpaka yakamilike hivyo Tanesco nao wanapenda kupata wateja wapya ili shirika lipate mapato na sio kwamba wanachelewesha makusudi
 
Naomba niwatie moto Ndugu zangu TANESCO kuwa wasikatishwe tamaa na watu watao waponda au kuwakandia , ndio changamoto za mitandao ya kijamii na Uhuru Wa kutoa hoja yako.

Ila mi naamini mpaka nimeingia online kimeo changu nimekichaji kwa Umeme Wa TANESCO ambao wengine wana ukandia. Ila nyie jibu masqali, hoja na duku duku zote bola jazba wala hasira. Hakika wataelewa wenyewe.
 
HATUA YA KWANZA-:- MAOMBI YA MWANZO

Je mteja anaweza kuchukua fomu ofisi yeyote ya tanesco?

Mteja anaweza kuchukua fomu ya maombi ya umeme katika ofisi yeyote ya shirika bila kujali kuwa eneo hilo linahudumiwa na ofisi husika. Ila atapaswa kurudisha ofisi ya maeneo ambayo makazi yake yapo ili kurahisisha kufanyiwa vipimo (service line survey)

JE KUNA GHARAMA ZOZOTE KATIKA UCHUKUAJI WA FOMU?

Fomu za maombi ya umeme zinatolewa bure kabisa kwa wateja wote.

VITU MUHIMU VYA KUZINGATIA WAKATI WA KUCHUKUA FOMU

1. Hakikisha umeme umefika maeneo yako na kama ni mradi uwe umekamilika.

2. Hakikisha mtandao wa nyaya ndani ya nyumba yako (wiring) umefanyika kupitia mkandarasi aliyesajiliwa.

3. Kitambulisho kinachomtambulisha muombaji wa umeme mfano leseni ya udereva, hati ya kusafiria, kitambulisho cha kazi (hii inasaidia shirika kumtambua mteja husika)

4. Kwa mwombaji wa mita ya ziada (meter separation) jina litakalotumika ni la mwenye nyumba kama linavyosomeka katika mita ya awali. Vinginevyo mteja atapaswa kutumia uthibitisho wa ruhusa ya mwenyenyumba kama atakuwa ni mpangaji. Lazima mteja aje na namba ya mita (kama zipo zaidi ya moja aje nazo zote) ili kuhakiki kama kuna yenye deni.

5. Kwa waombaji wanaomba kwa ajili ya ofisi, makapuni au taasisi za serikali au binafsi anapaswa kuja na leseni ya biashara, tin namba, udhibitisho wa usajili wa kampuni. Au udhibitisho wa ofisi ya serikali husika.

6. Kwa wapangaji wa nyumba za taasisi au makampuni waje na barua za waliopangisha zinazoonyesha kuwe wenye nyumba hizo wameridhia mita husika iwe na jina la mpangaji husika.

7. Shirika linapenda kuwaomba wamiliki wa nyumba kupenda kufika ofisi zetu wenyewe ili kuzuia udanganyifu ambao umekuwa ukifanywa na baadhi ya watu wasiokuwa waaminifu

HATUA YA PILI KUWEKA MCHORO, PICHA NA KUINGIA MAKUBALIANO YA KUFUNGIWA UMEME NAKUREJESHA FOMU

Endapo mteja atakidhi vigezo na masharti ya hatua ya mwanzo na kupatiwa fomu ya maombi ya mwanzo anatakiwa afanye yafuatayo

1. Kuisoma fomu kwa umakini mkubwa na kukubailiana na vigezo namba moja mpaka kumi na mbili. Mteja akijiridhisha kuwa amekubaliana na masharti yote ataweka sahihi sehemu husika (ukurasa wa pili wa fomu ya maombi ya umeme)

2. Kumpatia mkandarasi aliyesajiliwa ili achore mchoro wa mtandao wa nyaya (wiring diagram) wa nyumba husika pamoja na kugonga muhuri. (gharama ni makubaliano baina ya mteja na mkandarasi husika), wakandarasi wanapatikana kwenye ofisi zao maeneo mbalimbali, orodha ya waliosajiliwa pia inapatikana kwenye ofisi za tanesco. Mteja anapaswa kupewa orodha na kuchagua mkandarasi anayemtaka yeye.

3. Mteja atapaswa kuweka picha moja ya mwombaji wa umeme

4. Kisha mteja atarudisha fomu hiyo iliyokamilika ofisi ya eneo ambalo makazi yake yako (inayomudumia)

HATUA YA TATU- KUFANYIWA VIPIMO (SURVEY)

Mara baada ya mteja kurejesha fomu iliyojazwa kikamilifu, mteja atapangiwa tarehe ya kufanyiwa vipimo (survey). Mafundi watafika kwenye nyumba au sehemu inayoombewa umeme ili kutathimini gharama atakazolipia mteja kwa kuzingatia umbali wa eneo ilipo miundombinu ya umeme kama nguzo na transfoma na uwezo wa umeme huo kuunganisha kwa wateja wapya.

HATUA YA NNE: - KUPATIWA MAKADIRIO YA GHARAMA KIASI GANI ALIPE ILI AFUNGIWA UMEME

Mara baada ya kufanyiwa tathimini mteja anaweza kupatiwa makadirio ya gharama ya kiasi gani alipe ili kufungiwa umeme. Makadirio haya huweza kutumwa kwa njia ya nukushi, ujumbe mfupi wa meneno, barua pepe au mteja kufika ofisini na kuchukua barua. Viwango vya muda wa kutoa makadirio kama inavyoonekana kwenye jedwali hapo chini:

MAELEZO

Muda wa makadirio

Kama miundombinu iliyopo itatumika (ndani ya mita 30 kutoka kwenye nguzo iliyokaribu)

Ndani ya siku 7 za kazi

Ujenzi wa njia ya nyongeza unahitajika (mita 30- 100)

Ndani ya siku 10 za kazi

Kama mfumo mpya wa usambazaji unahitajika kujegwa au mfumo wa umeme mkubwa unahitajika kuongezwa kwa ajili ya kiwanda au biashara kubwa (kama hakuna mfumo wa kumuunganishia mwombaji) (zaidi ya mita 100)

Ndani ya siku 14 za kazi

HATUA YA TANO: - KUFANYA MALIPO

Mteja atafika ofisi ya tanesco ili kupatiwa namba ya kumbukumbu (reference number) itakayomuwezesha kufanya malipo bank, mteja atafanya malipo na atapatiwa stakabadhi ya malipo bank (risiti kwa njia ya ujumbe mfupi- sms) (kwa sasa ni bank ya nmb tu), wateja wanahimizwa kufanya malipo yote bank na si kwa mtu mwingine yeyote. Malipo yote yatakayofanyika nje ya mfumo uliwekwa hayatambulika na tanesco. Mteja akishafanya malipo bank husika hatatakiwa kurudi tena tanesco bali tanesco watakuwa na taarifa zake zote na kinachofuata ni kumfungia umeme.

HATUA YA SITA:-KUUNGANISHIWA UMEME

Mara baada ya mteja kufanya malipo viwango vya muda wa kumfungia umeme vitakuwa kama ilivyoonyeshwa kwenye jedwali hapo chini.

MAELEZO

Muda wa kufungiwa

Kama miundombinu iliyopo itatumika (ndani ya mita 30 kutoka kwenye nguzo iliyokaribu)

Ndani ya siku 30 za kazi

Ujenzi wa njia ya nyongeza itahitajika

(mita 30- 100)

Ndani ya siku 60 za kazi

KAMA MFUMO MPYA WA USAMBAZAJI UNAHITAJIKA KUJEGWA AU MFUMO WA UMEME MKUBWA UNAHITAJIKA KUONGEZWA KWA AJILI YA KIWANDA AU BIASHARA KUBWA (KAMA HAKUNA MFUMO WA KUMUUNGANISHIA MWOMBAJI) (ZAIDI YA MITA 100)

Ndani ya siku 90 za kazi

KWA MAULIZO WASILIANA NASI

Kituo cha huduma kwa wateja: - 0768985100/0222194400

Barua pepe: customer.Service@tanesco.Co.Tz

Facebook: www.Facebook.Com/tanesco yetu

Twitter: - www.Twitter.Com/tanesco yetu

Tovuti; www.Tanesco.Co.Tz

Elimu nzuri hii
 
Asanteni kwa ufafanuzi mzuri, naombeni mnisaidie swali hili hapa chini,
Kwasasa mimi nipo dodoma, ila nina nyumba ipo dar nimeshafanya wire-ring tayari ila process za mchoro bado, je kama process za kuomba umeme nikizifanyia uku dodoma, na mambo ya mchoro nikayafanyia uku uku itawezekana?
Ndio inawezekana ila kwenye mchoro huyo contractor awe registered na anayetambulika na shirika.
 
Gharama ya separeti mita za chumba kimoja zipo, na kama zipo ni kiasi gani mteja anatakiwa kulipa ila afanye matumizi ya kiwango cha chini cha nyumbani?
Gharama za ku separate meter ni sawa na gharama za s/l mpya. Bei yake inategemea ni meter ya aina gani (single phase au three phase) na upo sehemu gani (kijijini au mjini)
 
Tanesco nyiee bhana mnachelewesheaa sana kuwawekeaa watu umeme pindi mtu anapoitaji na anakuwa ameshalipaa kilaa kituu..ilaa mtamzungushaa weeee nakumtumiaa SMS za samahani mpk mtu uzalendo unampitaa ...jirani yangu hapa kalipiaa mwaka Jana nguzo pamoja na kujaa kufungiwa cha ajabu n mwezii wa sita sasa unaendaa anaambiwa nguzo zimeishaa ...jaman ktk miezi sita yote hyo amjaagizaa nguzoo tu uko zilipoo na kila cku naonaa garii ikipitaa na nguzoo.n kwann inatokeaa hvyoo ndugu zangu tanesco ..kumzungusha mtejaa wenu hvyooo.na si MTU wa kwanza kumshuhudiaa mkimzungushaa n wawilii watatuu
Na jamaa wakatakaa rushwaa akawapaa lakii na nusuu cha ajabu waonaa sijui ukaribuu wakumfungia mapema haupo wakamrudishiaa hela ilee aliyotoaa rushwa ..kiujumlaa jamaa kakataa tamaa na anataman hela yake irudishwe akae Giza lkn wanampa matumani...mm lukuu ilizinguaa tu nikatakiwaa kuwekaa mpyaa nikaendaa lipaa lakin cha moto nilikionaa nusuraa wapangaji wanitoee rohoo...tokaa mwaka Jana mwezi wa kumi na mbili mwakaa Jana imekujaa fungwaa mwezi wa pilii...nilijutaa...kiujumlaa tanesco hampoo makinii hataa kidogoo badoo hamwendii na kasii ya sasaaa...
 
Naomba usikimbie. Tujibu baadhi ya maswali japo machache:

1. Ni meter angapi maximum mtu atahitaji nguzo? (Yaani nguzo iliyopo hadi kufika ktk nyumba). Naomba maelezo hapa, kwani hapa ndio mafundi wa TANESCO hutupigia hela. mf ni 30m -70m au 30m to 100m? au 30-70m ni kile chuma tu bila nguzo kati ya 30m -100m?
2. Je ni sahihi ktk mfumo wa leo mtu kufunga/kuweka Cut-Out ktk meter kabla ya umeme kuingia ndani? (Japo ndani kutafungwa Circuit Breaker)
3. Naskia sijui Two Phases au Single Phase. Je ni mfumo upi ni mzr kwa matumizi ya nyumba ya makazi?

Note: Umesema Jedwali, lipo wapi sasa?
1. Kuhusu meter ngapi hapo huwezi kusema mpaka surveyor afike site na kuangalia mazingira yalivyokaa na namna gani ata design ili uweze kupata huo umeme

2. Cut out inafungwa baada ya meter kabla ya umeme kuingia kwenye main switch ambayo itakuwa na Circuit Breaker. Kuweka Cut Out sio lazima ila ukiweka ni sawa.

3. Kuhusu umeme wa single phase au three phase inatagemea na load yako. Load inamaanisha mahitaji yako ya umeme. Mfano unatumia taa ngapi, fridge ngapi, labda una pump ya maji, una cooker, una tv ngapi, una ac ngapi.

Hapo contractor wako wa umeme anataefanya wiring ya nyumba yako ndio ata calculate load yako na akipata total KW unazohitaji ndio ita determine unahitaji single au three phase..

Hivyo hakuna kusema eti umeme wa single au wa three phase ndio mzuri hapana. Aina ya phase unayowekewa inatokana na load yako. Mara nyingi ukiwa na load kuanzia 14kW kwenda juu hiyo ni three phase ina maana kushuka chini ni single phase.

Na huwezi kuwekewa three phase ukiwa na load ndogo kwakuwa umeme wa three phase una Volts kuanzia 400 wakati single phase ni 220- 200 Volts.

Hivyo basi ukiwekewa umeme wa Volts 400 wakati una load ndogo inaweza kupelekea vitu vyako kua overloaded na kuungua na ukiwekewe umeme wa volts 210 wakati load yako ni kubwa basi usishangae ukiwasha ac haziwaki mara cooker haliwaki maana umeme unakuwa mdogo. Asante
 
Ahsante sn mkuu.
Eti matumizi ya Cut-Out ni yapi ndg?
 
Asante sana TANESCO kwa maelezo na majibu mujarabu kabisa.

Labda nami nikuulize kitu kimoja.
Iwapo nimekodi eneo la biashara mfano ofisi na nikalazimika kufunga mita yangu ya umeme ili kuepusha usumbufu na watumiaji wengine. Na iwapo mita hiyo ipo kwa jina langu kwa malipo niliyofanya mwenyewe baada ya kukubaliana na mwenye jengo au eneo kwa utaratibu ulioueleza kwenye uzi wakohapo juu. Je pindi nikitaka kuama eneo au ofisi, ninaruhusiwa kumtafuta fundi wenu aweze kuniamishia mita yangu kwenda kunifungia mahali pengine ninapotaka kuhamia? Au ukishaifunga mita basi haihamishiki tena. Maelezo tafadhali
 
hongera kwa kulisaidia shirika.
 
@chaliifrancisco, TANESCO kuna swali jingine hapa. mie ni muhanga wa kusubiria umeme kwa muda mrefu katika maeneo tofauti. sehemu ya kwanza ni dsm na ya pili ni ikonda njombe kwenye mradi wa REA(umeme vijijin).

kwa dsm nimeletewa nguzo mbili kama wiki moja imepita, je swali langu ni tuuendelee kusubiria tena miezi sita mingine au kuna unafuu wa muda.
kwa kule kijijini pana hitaji nguzo moja lakini nakaribia miezi 9.

kingine nawapa Pongezi maana niliwalaumu bure lakini kuna mfanyakazi wa tanesco alinielewesha japo aliambulia yale maneno ya KA-TA
 
Ahsante sn mkuu.
Eti matumizi ya Cut-Out ni yapi ndg?
Cut-out ni kifaa cha umeme ambacho kina unganisha cable ya umeme ya tanesco na wiring ya mteja. Yaani hapa ndipo pale umeme wa tanesco unakutana na wiring system ya mteja inapoanzia.

Kazi yake ni kuhakikisha kuwa kuwa umeme unahitaji mteja unapita salama kwenda kwenye nyumba yako.

Inaunganishwa direct kwenye umeme unaokuja kwako mteja na ina kitu kinaitwa ‘main fuse’. Hii husaidia kuhakikisha kiwango sahihi cha umeme kinaingia kwenye nyumba yako.

Kama umeme ukiwa mwingi unataka kuingia kwenye nyumba yako hiyo main fuse inafanya isolation ili umeme huo usiingie kwenye nyumba ili vitu visiungue na hapo inafanya kuzuia umeme usiingie kwako kwa kiwango kikubwa kwa ku trip na umeme kukata kwemye jengo kukiwa na overload ya voltage.
 
Asante sana TANESCO kwa maelezo na majibu mujarabu kabisa.

Labda nami nikuulize kitu kimoja.
Iwapo nimekodi eneo la biashara mfano ofisi na nikalazimika kufunga mita yangu ya umeme ili kuepusha usumbufu na watumiaji wengine. Na iwapo mita hiyo ipo kwa jina langu kwa malipo niliyofanya mwenyewe baada ya kukubaliana na mwenye jengo au eneo kwa utaratibu ulioueleza kwenye uzi wakohapo juu. Je pindi nikitaka kuama eneo au ofisi, ninaruhusiwa kumtafuta fundi wenu aweze kuniamishia mita yangu kwenda kunifungia mahali pengine ninapotaka kuhamia? Au ukishaifunga mita basi haihamishiki tena. Maelezo tafadhali
Meter ikishafungwa sehemu hata ukitaka kuhama huwezi kuihamisha labda iwe within the sama plot (yaani mfano mita ipo chumbani unataka kuihamishia barazani au kuna nyumba nyingine kwenye the same plot)

Kama unahamia kwingine hapo meter hurudi Tanesco na wewe huko unapohamia utafanya maombi yakupata meter mpya
 
Back
Top Bottom