Zijue taratibu za kufuata ili kufungiwa umeme na TANESCO

Zijue taratibu za kufuata ili kufungiwa umeme na TANESCO

Kuna jambo limeniumiza to the maximum baada ya jitihada zetu za kuweza kujumuishwa kwenye miradi ya REA kugonga mwamba, tukajikusanya vijana kadhaa ili tuweze kuchanga pesa kidogo kidogo hata iwe ndani ya miaka kadhaa tuvute umeme, ili tubidi twende tanesco ili kuulizia gharama ya nguzo. Mbali na masuala ya bei ya kawaida kilichotuchosha ni kwamba tuliambiwa nguzo tutauziwa nguzo mbili kwa shilingi 450,000/= lakini pale tulipokuwa tunahitaji kuweka umeme kutoka kwenye source ya umeme zinatakiwa nguzo takriban 40, tukapanga tugawane pesa inayotakiwa ili tupate nguzo hizo, lakini tuliporudi tanesco ili kupata mchanganuo zaidi, tuliambiwa Hivi "ikisha zidi nguzo mbili kutoka kwenye source basi mteja hauziwi nguzo ktk bei za kawaida bali huuziwa nguzo kama ni kwa ajiri ya MRADI, hivyo zikishazidi nguzo mbili gharama huingia jumla ya shilingi 2,800,000/= tuliishiwa nguvu, hatukutaka tena kuzungumzia tena masuala ya umeme bali tuliridhika kuwa UMEME ni kwa ajili ya watanzania wengine tena wateule siyo sisi. Sasa humu naomba msaada kwanini mnatufikisha hatua hiyo? Umeme huu kwa hali hii ni Watanzania wangapi wanaweza kujivutia umeme? Tanesco mmeamua kutubagua watanzania ? Je, mnataka vijiji/ vitongoji ambavyo havina umeme wala havimo kwenye mpango wa REA vikae gizani miaka yote? Naomba msaada hata wa mawazo kwani miaka karibia mitatu humu nawaeleza juu ya uhitaji wetu wa umeme kwenye Kitongoji chetu lakini sijawahi kupata hata msaada tofauti na kuambiwa kuwa suala lako linashughulikiwa.
WILAYA

ENEO

NAMBA YA SIMU TAFADHALI
 
TANESCO ni nina mwaka mmoja na miezi minne tangu nilipoandika na kuwasilisha katika moja ya ofisi zenu barua ya kuomba kubadilishiwa mita ya luku iliyofungwa ndani ili kufungiwa mita nyingine mnazofunga nje huku zikitumia remote kujaza units zilizonunuliwa. Je, ni sahihi kupita muda wote huo pasipo TANESCO kubadilisha mita hiyo au hata kujibu barua hiyo niliyowaandikia?
Wilaya

Eneo

Namba ya simu


Tafadhali
 
Ipo siku Tanesco itakua inahangaika kuwatafuta wateja kama ilivyo TTCL leo. Wafanyakazi wa TTCL miaka ya 90 ulikua ukienda kuomba form ya kuwekewa simu, unaulizwa " Simu unataka we ya nini" but leo, mmh.
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]eti we unataka simu ya nini?Kama ni Mimi ningewajibu na nyie mnauza simu za nini?
 
Aisee napoishi mita namba nikinunua umeme napewa mchache sana
Na matumizi yangu ni chini ya unit 2 kwa siku
Mfano 2000/= 5.7 unit
While nnachojua 2000/=14.... Unit

Sasa apo ni hasaraa
 
HATUA YA KWANZA

MAOMBI YA MWANZO

Je mteja anaweza kuchukua fomu ofisi yeyote ya tanesco?


Mteja anaweza kuchukua fomu ya maombi ya umeme katika ofisi yeyote ya shirika bila kujali kuwa eneo hilo linahudumiwa na ofisi husika. Ila atapaswa kurudisha ofisi ya maeneo ambayo makazi yake yapo ili kurahisisha kufanyiwa vipimo (service line survey)

JE KUNA GHARAMA ZOZOTE KATIKA UCHUKUAJI WA FOMU?

Fomu za maombi ya umeme zinatolewa bure kabisa kwa wateja wote.

VITU MUHIMU VYA KUZINGATIA WAKATI WA KUCHUKUA FOMU

1. Hakikisha umeme umefika maeneo yako na kama ni mradi uwe umekamilika.

2. Hakikisha mtandao wa nyaya ndani ya nyumba yako (wiring) umefanyika kupitia mkandarasi aliyesajiliwa.

3. Kitambulisho kinachomtambulisha muombaji wa umeme mfano leseni ya udereva, hati ya kusafiria, kitambulisho cha kazi (hii inasaidia shirika kumtambua mteja husika)

4. Kwa mwombaji wa mita ya ziada (meter separation) jina litakalotumika ni la mwenye nyumba kama linavyosomeka katika mita ya awali. Vinginevyo mteja atapaswa kutumia uthibitisho wa ruhusa ya mwenyenyumba kama atakuwa ni mpangaji. Lazima mteja aje na namba ya mita (kama zipo zaidi ya moja aje nazo zote) ili kuhakiki kama kuna yenye deni.


5. Kwa waombaji wanaomba kwa ajili ya ofisi, makapuni au taasisi za serikali au binafsi anapaswa kuja na leseni ya biashara, tin namba, udhibitisho wa usajili wa kampuni. Au udhibitisho wa ofisi ya serikali husika.

6. Kwa wapangaji wa nyumba za taasisi au makampuni waje na barua za waliopangisha zinazoonyesha kuwe wenye nyumba hizo wameridhia mita husika iwe na jina la mpangaji husika.

7. Shirika linapenda kuwaomba wamiliki wa nyumba kupenda kufika ofisi zetu wenyewe ili kuzuia udanganyifu ambao umekuwa ukifanywa na baadhi ya watu wasiokuwa waaminifu

HATUA YA PILI KUWEKA MCHORO, PICHA NA KUINGIA MAKUBALIANO YA KUFUNGIWA UMEME NAKUREJESHA FOMU

Endapo mteja atakidhi vigezo na masharti ya hatua ya mwanzo na kupatiwa fomu ya maombi ya mwanzo anatakiwa afanye yafuatayo

1. Kuisoma fomu kwa umakini mkubwa na kukubailiana na vigezo namba moja mpaka kumi na mbili. Mteja akijiridhisha kuwa amekubaliana na masharti yote ataweka sahihi sehemu husika (ukurasa wa pili wa fomu ya maombi ya umeme)

2. Kumpatia mkandarasi aliyesajiliwa ili achore mchoro wa mtandao wa nyaya (wiring diagram) wa nyumba husika pamoja na kugonga muhuri. (gharama ni makubaliano baina ya mteja na mkandarasi husika), wakandarasi wanapatikana kwenye ofisi zao maeneo mbalimbali, orodha ya waliosajiliwa pia inapatikana kwenye ofisi za tanesco. Mteja anapaswa kupewa orodha na kuchagua mkandarasi anayemtaka yeye.

3. Mteja atapaswa kuweka picha moja ya mwombaji wa umeme

4. Kisha mteja atarudisha fomu hiyo iliyokamilika ofisi ya eneo ambalo makazi yake yako (inayomudumia)

HATUA YA TATU- KUFANYIWA VIPIMO (SURVEY)

Mara baada ya mteja kurejesha fomu iliyojazwa kikamilifu, mteja atapangiwa tarehe ya kufanyiwa vipimo (survey). Mafundi watafika kwenye nyumba au sehemu inayoombewa umeme ili kutathimini gharama atakazolipia mteja kwa kuzingatia umbali wa eneo ilipo miundombinu ya umeme kama nguzo na transfoma na uwezo wa umeme huo kuunganisha kwa wateja wapya.

HATUA YA NNE: - KUPATIWA MAKADIRIO YA GHARAMA KIASI GANI ALIPE ILI AFUNGIWA UMEME

Mara baada ya kufanyiwa tathimini mteja anaweza kupatiwa makadirio ya gharama ya kiasi gani alipe ili kufungiwa umeme. Makadirio haya huweza kutumwa kwa njia ya nukushi, ujumbe mfupi wa meneno, barua pepe au mteja kufika ofisini na kuchukua barua. Viwango vya muda wa kutoa makadirio kama inavyoonekana kwenye jedwali hapo chini:

MAELEZO

Muda wa makadirio

Kama miundombinu iliyopo itatumika (ndani ya mita 30 kutoka kwenye nguzo iliyokaribu)

Ndani ya siku 7 za kazi

Ujenzi wa njia ya nyongeza unahitajika (mita 30- 100)

Ndani ya siku 10 za kazi

Kama mfumo mpya wa usambazaji unahitajika kujegwa au mfumo wa umeme mkubwa unahitajika kuongezwa kwa ajili ya kiwanda au biashara kubwa (kama hakuna mfumo wa kumuunganishia mwombaji) (zaidi ya mita 100)

Ndani ya siku 14 za kazi

HATUA YA TANO: - KUFANYA MALIPO

Mteja atafika ofisi ya tanesco ili kupatiwa namba ya kumbukumbu (reference number) itakayomuwezesha kufanya malipo bank, mteja atafanya malipo na atapatiwa stakabadhi ya malipo bank (risiti kwa njia ya ujumbe mfupi- sms) (kwa sasa ni bank ya nmb tu), wateja wanahimizwa kufanya malipo yote bank na si kwa mtu mwingine yeyote. Malipo yote yatakayofanyika nje ya mfumo uliwekwa hayatambulika na tanesco. Mteja akishafanya malipo bank husika hatatakiwa kurudi tena tanesco bali tanesco watakuwa na taarifa zake zote na kinachofuata ni kumfungia umeme.

HATUA YA SITA:-KUUNGANISHIWA UMEME

Mara baada ya mteja kufanya malipo viwango vya muda wa kumfungia umeme vitakuwa kama ilivyoonyeshwa kwenye jedwali hapo chini.

MAELEZO

Muda wa kufungiwa

Kama miundombinu iliyopo itatumika (ndani ya mita 30 kutoka kwenye nguzo iliyokaribu)

Ndani ya siku 30 za kazi

Ujenzi wa njia ya nyongeza itahitajika

(mita 30- 100)

Ndani ya siku 60 za kazi

KAMA MFUMO MPYA WA USAMBAZAJI UNAHITAJIKA KUJEGWA AU MFUMO WA UMEME MKUBWA UNAHITAJIKA KUONGEZWA KWA AJILI YA KIWANDA AU BIASHARA KUBWA (KAMA HAKUNA MFUMO WA KUMUUNGANISHIA MWOMBAJI) (ZAIDI YA MITA 100)

Ndani ya siku 90 za kazi

KWA MAULIZO WASILIANA NASI

Kituo cha huduma kwa wateja: - 0768985100/0222194400

Barua pepe: customer.Service@tanesco.Co.Tz

Facebook: www.Facebook.Com/tanesco yetu

Twitter: - www.Twitter.Com/tanesco yetu

Tovuti; www.Tanesco.Co.Tz
Mbona inaelekea kuna mgomo baridi,TANESCO wamekuwa wagumu sana kufungia watu umeme kwa hii rate mpya ya Sh.27,000.Nasema hivyo kwa kuwa upo ulalamishi wa wazi kutoka kwa watumishi wa TANESCO kwamba rate hiyo haina maslahi.And then mbona kiuhalisia bei ya kufungiwa umeme sio 27,000 ni 57,000,kwa kuwa ipo Sh.30,000 ambayo inabidi ulipe kwa mtu anayeitwa Contractor,wakati kazi ya huyo contractor haionekani kazi zote wanafanya TANESCO wenyewe?Huu si upigaji jamani.
 
Leo Sichangi Sana Nawasubiri Bado Siku Kazaa Hapo Mbele Umeme Walete Malipo Nimeshamaliza Na Rist Ya Benk Ninayo
 
WILAYA

ENEO

NAMBA YA SIMU TAFADHALI
Nilitegemea jibu kama hili maana huu takribani mwaka wa 3 kila nikijaribu kuelezea na kuleta maombi humu mimi huwa naambiwa kauli kama hii, ok namba nakupatia tena ni, 0684542853
 
Nilitegemea jibu kama hili maana huu takribani mwaka wa 3 kila nikijaribu kuelezea na kuleta maombi humu mimi huwa naambiwa kauli kama hii, ok namba nakupatia tena ni, 0684542853
Ndugu mpendwa mteja wetu tumekupigia simu yako haipokelewi,Je ni kijiji gani na wilaya tafadhali
 
Nashukuru sana ni kweli nimepigiwa sim sikuweza kuipokea nilikuwa kusali. Ni miaka mingi sana nilileta ombi langu la kuomba kusaidiwa suala la kupatiwa umeme wa REA kwenye kitongoji cha KIJUKA Kijiji Mabuye Wilaya ya Missenyi mkoani Kagera. Kitongoji cha KIJUKA kiko Kaskazini Mashariki mwa Wilaya ya Missenyi ni mwendo wa km Kilometa mbili tu kutoka yalipo makao makuu ya wilaya ya Missenyi na ni kitongoji cha kwanza kutoka yalipo makao makuu ya Wilaya ya ya Missenyi ukiwa unaelekea kwenye kijiji cha Mabuye. Hiki kitongoji cha KIJUKA kimebaki kama kisiwa kimerukwa na hakijapewa umeme wa REA japo kina kila sifa ya kupewa Umeme wa REA. Tumejaribu kufuatilia lakini mpaka sekunde ya leo hakuna majibu ya kuridhisha Kibaya zaidi hata viongozi hawatupi ushirikiano ni sisi wananchi tunahangaika wenyewe. Tumeenda mbali tukapanga vijana tuunganishe nguvu tujivutie umeme lakini imeshindikana kumbe hatuwezi kutokana na gharama kuwa juu. Sasa tunaomba msaada tafadhali sana hiki kitongoji kipatiwe huduma ya REA. Aidha hata mimi nashukuru nimepigiwa sim kwa bahati mbaya nilikuwa kanisani ila nimepiga tena sikupokelewa nitafurahi kesho nikipigiea tena nitatoa ushirikiano.
0684542853
 
Nashukuru sana ni kweli nimepigiwa sim sikuweza kuipokea nilikuwa kusali. Ni miaka mingi sana nilileta ombi langu la kuomba kusaidiwa suala la kupatiwa umeme wa REA kwenye kitongoji cha KIJUKA Kijiji Mabuye Wilaya ya Missenyi mkoani Kagera. Kitongoji cha KIJUKA kiko Kaskazini Mashariki mwa Wilaya ya Missenyi ni mwendo wa km Kilometa mbili tu kutoka yalipo makao makuu ya wilaya ya Missenyi na ni kitongoji cha kwanza kutoka yalipo makao makuu ya Wilaya ya ya Missenyi ukiwa unaelekea kwenye kijiji cha Mabuye. Hiki kitongoji cha KIJUKA kimebaki kama kisiwa kimerukwa na hakijapewa umeme wa REA japo kina kila sifa ya kupewa Umeme wa REA. Tumejaribu kufuatilia lakini mpaka sekunde ya leo hakuna majibu ya kuridhisha Kibaya zaidi hata viongozi hawatupi ushirikiano ni sisi wananchi tunahangaika wenyewe. Tumeenda mbali tukapanga vijana tuunganishe nguvu tujivutie umeme lakini imeshindikana kumbe hatuwezi kutokana na gharama kuwa juu. Sasa tunaomba msaada tafadhali sana hiki kitongoji kipatiwe huduma ya REA. Aidha hata mimi nashukuru nimepigiwa sim kwa bahati mbaya nilikuwa kanisani ila nimepiga tena sikupokelewa nitafurahi kesho nikipigiea tena nitatoa ushirikiano.
0684542853
Tumewahi kukupatia maelezo mara kadhaa zidi ya eneo hili tutakupatia tena maelezo ya ziada
 
Biharamulo niliomba umeme tangu mwezi 02/2019 Hadi leo nimeishia kufanyiwa tathimini tu! Kila nikienda nazungushwa mara fomu haionekani, mara hakuna mtandao wa kutolea control number huu ni mwezi wa sita namba sipewi ili nikafanye malipo. Japo Kuna mtumishiwa wao sliniambia bila kutoa chochote nitasikia tu kwa majirani na Mimi hela ya kuwapa nje na malipo halali Sina. Sijui hata la kufanya.
 
Waziri wa nishati kasema ni marufuku kununua nguzo,kwa nn mlikuwa mnatuuzia nguzo?
 
Hawa Tanesco wa jamii forum hawana msaada kabisa ni simba aliyechorwa tu
 
Kwa nn Tanesco wanaweka matumiz makubwa kwa walioingiza Umeme three phase ikiwa matumiz ya mteja hayazidi unit 70 kwa mwezi????
 
Kiongoz, hili linafikishwa kwa Rais moja kwa moja, hawa watumishi wa tanesco haiwezekani watuchezee akili
Biharamulo niliomba umeme tangu mwezi 02/2019 Hadi leo nimeishia kufanyiwa tathimini tu! Kila nikienda nazungushwa mara fomu haionekani, mara hakuna mtandao wa kutolea control number huu ni mwezi wa sita namba sipewi ili nikafanye malipo. Japo Kuna mtumishiwa wao sliniambia bila kutoa chochote nitasikia tu kwa majirani na Mimi hela ya kuwapa nje na malipo halali Sina. Sijui hata la kufanya.
 
Back
Top Bottom