Zijue taratibu za kupima DNA, gharama ya kipimo ni Tsh.100,000/=

Zijue taratibu za kupima DNA, gharama ya kipimo ni Tsh.100,000/=

Yaani mwanangu mwenyewe nishindwe kumtambua? First time anatolewa labor nikaangalia nikajua hii chata! Ni natural DNA tu huhitaji kwenda kwa mkemia
 
Naona mnatetea ujinga et mauaji acha wafe,kupma inabidi tunalea matoto yenye tabia za ajabu sana kumbe sio damu zetu.

umeongea point sana, unakuta familia yenu sio magenius halafu linakuja toto genius lazima muanze mashaka.

Kuna Mzee mmoja alikuwa ananiambia, kuna binti anahisi sio wake, maana kabinti ni kimalaya balaa wakati ukoo wao hakuna mwenye tabia hiyo hata mmoja..
 
Kumekuwa na minong'ono mitaani kuwa upimaji wenu unaangalia zaidi athari kwa mtoto na sio ukweli wa mtoto.

Yaani kama baba ni mmoja basi atapatiwa huyo mtoto atake asitake majibu yatakuja upande wake. Hii imewafanya wengi wenye kauwezo kukimbizia sampo zao Kenya. Kama ni kweli mjitathimini.

Binafsi hela yangu na sioni haja ya kuhusisha mtu mwingine zaidi ya mm na mtoto na mpimaji.

Hao ustawi watanisamehe kwenye DNA. Kwa ufupi bado nazichanga na mm nivushe sampuli upande mwingine.
 
Lakini msimamiz mkuu wa majibu hayo ni afisa ustawi endapo Kuna mgogoro wa familia Kama unao usema
 
Kumekuwa na minong'ono mitaani kuwa upimaji wenu unaangalia zaidi athari kwa mtoto na sio ukweli wa mtoto. Yaani kama baba ni mmoja basi atapatiwa huyo mtoto atake asitake majibu yatakuja upande wake. Hii imewafanya wengi wenye kauwezo kukimbizia sampo zao Kenya. Kama ni kweli mjitathimini. Binafsi hela yangu na sioni haja ya kuhusisha mtu mwingine zaidi ya mm na mtoto na mpimaji. Hao ustawi watanisamehe kwenye DNA. Kwa ufupi bado nazichanga na mm nivushe sampuli upande mwingine.
Duh kumbe ndio hivo ...basi wanaume wengi wanalea watoto watoto ambao sio wao
 
Mtagombanisha Wananchi wa Tanzania na kuleta tafarani nchini

Familia za kitanzania tangu enzi zinalea Watoto wasio wao na kulelewa Watoto wao na familia zingine na hawajawahi kuja kushitaki kwenu wala kufungua kesi mahakamani

Waacheni watanzania waishi namna hiyo na Watoto wapate haki ya kutunzwa.
Acha wewe,hiyo dunia ya hivyo ilishapita miaka mingi sana acha kuishi kwa historia.mtoto ni haki miliki kama ilivyo kwenye mali sasa iweje tuendelee kua na tamaduni zakumiliki mali isiyo yako kwasababu zakijinga zisizotatua tatizo la wanawake kutokua waaminifu.
 
Hii huduma inatakiwa iwe rahisi ili kuokoa wazee wetu wanaokufa kwa misongo ya mawazo yakusababishwa na wake zao wenye tamaa.Kuna kisa nakifahamu kilichosababisha mzee wawatu akapata stroke iliyomtesa hadi mauti.Huyo mzee alifungashiwa mtoto pamoja na minong'ono kua sio mtoto wake alipotezea akamlea mtoto kwa mapenzi makubwa,sasa ikatokea yule baba halisi wa yule mtoto akaja akafariki na alikua kibopa mwenye hela zake ila ambaye anapenda kuchukua wake za watu,sasa yule mama alivyoona yule mzee amefariki akajua kuna mahela kayaacha akaenda kuiambia ile familia kua alizaa na yule mzee kwahiyo mwanae awe kwenye mirathi.Mumewe alipogundua alipata presha iliyompa stroke ikamsumbua miaka 4 akafariki.Nchi zawezetu walishatoka kwenye dunia yakucomplicate mambo ambayo yanaiumiza jamii.kama wewe ni mwanamke umekubali kuingia kwenye ndoa kaa utulie sio kuwaka tamaa hadi ukabebe mimba uilete ndani kwa kisingizio cha kitanda hakizai haramu.
 
Kuna ile kusingiziwa na single parent kisa tu baba una uwezo, kumbe mwenye uhalali kachukiwa tu. Unaingia mkataba wa kutoa matumizi mwanzo mwisho kumbe zigo sio lako.

Kwenye ndoa kikubwa kuvumiliana tu. Sisi bado ni wajamaa kwa matendo na mabeberu kwa maneno
 
Back
Top Bottom