Hii huduma inatakiwa iwe rahisi ili kuokoa wazee wetu wanaokufa kwa misongo ya mawazo yakusababishwa na wake zao wenye tamaa.Kuna kisa nakifahamu kilichosababisha mzee wawatu akapata stroke iliyomtesa hadi mauti.Huyo mzee alifungashiwa mtoto pamoja na minong'ono kua sio mtoto wake alipotezea akamlea mtoto kwa mapenzi makubwa,sasa ikatokea yule baba halisi wa yule mtoto akaja akafariki na alikua kibopa mwenye hela zake ila ambaye anapenda kuchukua wake za watu,sasa yule mama alivyoona yule mzee amefariki akajua kuna mahela kayaacha akaenda kuiambia ile familia kua alizaa na yule mzee kwahiyo mwanae awe kwenye mirathi.Mumewe alipogundua alipata presha iliyompa stroke ikamsumbua miaka 4 akafariki.Nchi zawezetu walishatoka kwenye dunia yakucomplicate mambo ambayo yanaiumiza jamii.kama wewe ni mwanamke umekubali kuingia kwenye ndoa kaa utulie sio kuwaka tamaa hadi ukabebe mimba uilete ndani kwa kisingizio cha kitanda hakizai haramu.