Zilikuwa nyakati za Chico, Nat King Cole, Dean Martin, Sammy Davis Jr, Sidney Poitier..Ukipenda Sal

Puti...
Zawadi hii kutoka kwangu:





Hiyo picha ya Ali na Frazier imetundikwa hapo Guy Madison
Square Garden New York

Umesoma autobiography ya Ali: ''Muhammad Ali My Own Story?''
 
Wazee wangu mna story nzuri sana, uandishi na mtiririko wake unamvuta anaesoma hata kama ni story ndefu aendelee kusoma, mimi ni mdogo kwenu ila hadithi za dar tulikua tukizipata huku Tanga na baadae Tabora wakati nasoma, na hasa za hapo saigon na cosmo nilikua nikisikia mtu katoka dar basi napenda ahadithie habari za mitaa ya karikoo.
Ushauri hivi mzee wangu ukifanya utafiti kidogo na nduguzo ambao bado wapo hai hudhani waweza kuandika kitabu cha story za dar na kariakoo kwa jumla, maana nimeona uwezo wako wa uandishi ni mkubwa sana pengine ingekua ni ukumbusho kwa sisi wadogo zenu.
Uniwie radhi kama nitakua nimekukwaza
 
Mimi nikisomaga hizi Story zako huwa sipendi sana kuendelea kwa kuwa hujikuta nabubujikwa na Machozi as I can't undue the Past!

Nikikuona na Kaka Yangu Ferej Tamim naona kweli tumezeeka
 
Kwemanga wewe si wa kwanza kunipa ushauri huu In Shaa Allah...ingia www.mohammedsaid.com kuna historia...
 
Shukran sana kwa kutumia muda wako kutujuza kuhusu habari nzuri za wakati huo, hususan, habari za Kamanda Chico. Mimi nikutana naye uso kwa uso siku moja tu akiwa Kamanda Arusha,nikiwa Afisa mwandamizi Serikalini; nikajitambulisha kwake tukasalimiana kwa kupeana mikono. Namkumbuka kwa kiganja kikubwa bila shaka kwa sababu alikuwa na umbo kubwa. Ni watu wachache sana ambao hupenda udhaifu wa binadamu kuchimbuliwa na kuandikwa. Hakuna faida kwa jamii hasa ukizikatia kuwa hakuna binadamu aliyekamilika. Itoshe tu kukushukuru mwandishi kwa kutusimulia Dar ilivyokuwa enzi hizo kupitia maisha ya Kamanda Chico na kizazi chenu. Shukran sana.
 
Kwanza heshima kwako mzee wangu Mohammed Said , ni mengi nimejifunza kutokana na maandiko yako hasa hasa heshima hata kwa wadogo, umekua ukituasa sana juu ya kuishi kwa amani na upendo kwani hakuna aijuaye kesho. Wasalaam.
 
Kwanza heshima kwako mzee wangu Mohammed Said , ni mengi nimejifunza kutokana na maandiko yako hasa hasa heshima hata kwa wadogo, umekua ukituasa sana juu ya kuishi kwa amani na upendo kwani hakuna aijuaye kesho. Wasalaam.
Chotera,
Ahsante kaka.
Alikuwa akiosha sufuria leo ana hoteli na watumishi.

Huyo ndiye Allah anampeleka juu aliyekuwa chini na
kumshusha aliyekuwa chini.

Mikasa kama hii ninayo mingi.
Uzee dawa.
 
Peter...
Ahsante sana.

''Zungumzeni mema ya maiti zenu.''
Muhammad SAW
 
Mimi nikisomaga hizi Story zako huwa sipendi sana kuendelea kwa kuwa hujikuta nabubujikwa na Machozi as I can't undue the Past!

Nikikuona na Kaka Yangu Ferej Tamim naona kweli tumezeeka
Pohamba,
Usitokwe na machozi bali shukuru kuwa Allah katuweka kiasi hiki
kwani wenzetu wengi wameshatangulia.

Tamim ni rafiki yangu wa miaka mingi sana.
Nikipata picha za zamani nitakuwekea hapa.
 
Habari murua kweli wewe ni gwiji wa uhandishi.
 
Nakumbuka wakati akiwa kamanda wa polisi mkoa wa kilimanjaro alialikwa kwenye mahafali yetu ya kidato ya kidato cha sita. Kwa kuwa alijua wanafunzi huwa wanawadharau polisi kwanza alipasua yai dakika tano ndio akarudi kwenye kiswahili. Akatusuuza sana. Pia alisema yeye alibobea katika usalama baharini na kwamba yeye alikuwa ni PhD holder! Baadae nilikutana naye alipokuja mtaani kwetu kufanya harambee ua ujenzi wa msikiti ambapo tulifanikiwa sana. Allaah amasamehe na amthibitishie kauli
 
sheikh huyo Sammy kafanana na Salim Hirizi alokuwa Dubai
Je wana undue au watu kufanana tuu?
 
sheikh huyo Sammy kafanana na Salim Hirizi alokuwa Dubai
Je wana undue au watu kufanana tuu?
Saul,
Ndiyo yeye huyo Salim Hariz.

Unajua jina ni Hariz lakini watu wakaona Hirizi ni jepesi
basi ndiyo ikawa hivyo.

Alikuwa anakaa nyuma ya Carlton Hotel.
Mi nimefika pale kwake 1991 na nikikaa Carlton.
 
Saul,
Ndiyo yeye huyo Salim Hariz.

Unajua jina ni Hariz lakini watu wakaona Hirizi ni jepesi
basi ndiyo ikawa hivyo.

Alikuwa anakaa nyuma ya Carlton Hotel.

Mi nimefika pale kwake 1991 na nikikaa Carlton.
Hii Sammy Davis ni ''nickname,'' yake.
 
Mohammed Said

Unajua kama Al Jareau ametangulia mbele ya Haki leo?
Naomba nikurudishe kwenye miaka ya 70 hivi ndio alikuwa ametoa Albums mzuri zaidi kwa mtazamo wangu na albums zake 3 nizipendazo ni We Got By, kisha akatoa double album ambayo ilikuwa live na album yake ya 3 niliykuwa nikiipenda zaidi ni Look to the Rainbow, which I played the hell out of.

Kama unakumbuka ile tv show ya Moonlight ya 1980's bas utakumbuka hii nyimbo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…