Kweli mdau,upo sahihiMkuu SI WAZURI BINADAMU imeimbwa na BICHUKA lakini akiwa na OSS sio MLIMANI PARK. "Ninakushukuru Mungu huso mshirikae kuiponya roho yangu ilotaka toweka binadamu madhurumu ana vituko vya sumu anavituko vya sumu kali kushinda ya nyokae si wazuri binadamu usione wachekaa ooh nhon."
Hizi nyimbo na mie Mhhhhh! lakini siku za karibuni nimeanza kusikia chache ambazo zinanigusagusa.
Naikumbuka siku ileeee ulipokuja asubuhi na mapema,
........
wimbo huo nautafuta sana, sikumbuki jina lake wala walioupiga
Dah.....
Wakuu jioni ya leo nimepata habari mbaya kabisa ambazo ni za kusikitisha....
Mtaalamu KABEYA BADU amefariki jioni ya leo...
R.I.P KABEYA BADU
hii bendi naivulia kofia kweli ilisheheni vipaji akina kasaloo(r.i.p),kyanga songa(r.i.p),kalala mbwembwe(r.i.p),dingituka morlay(r.i.p),john kitime,kawalee,hashim kasanga(r.i.p)mama - tancut almasi orchestra
hii band ya tancut almsi kwa kweli................ Bado naitafuta album nzima yenye wimbo huu wa mama.
Balantanda bado naisubiri maana uliniahidi kunitafutia nyimbo original za hawa mapacha wa kikongo.
Ukitaka kusikiliza, basi pitia hapa: wanamuziki wa tanzania :: Music - reverbnation
Pia kuna Orch. Marquiz Original,kundi hili liliundwa miaka ya 70 na wanamuziki waliotoka katika jimbo la Shaba nchini Zaire(DRC) waliingia nchini wakiitwa Orchestre Super Gabby,baada ya kuingia nchini walibadilisha jina na kuanza kuitwa Orchestra Maquis du Zaire/Marquis Original.....Mitindo waliyoitumia ni pamoja na Ogelea Piga Mbizi,Zembwela na Sendema.....Ukumbi waliokuwa wakipiga(uwanja wao wa nyumbani) ni Lang'ata Social Hall pale Kinondoni(FM Club ambapo kwa sasa ni kanisa).....Hawa pia walikuwa wanaujua muziki hasa kutokana na aina ya muziki mchanganyiko wa kizaire(kavasha) na vionjo vya kitanzania walivyopiga....
Bendi hii ilitamba na nyimbo nyingi sana,nyimbo kama Mayanga,Ngalula,Makumbele,Mpenzi Luta,Mpenzi Scola,Karubandika,Seya,Tipwatipwa,Kisabengo,Wakati nilikuwa mdogo,Bi Sofia,Hali ngumu,Ni wewe pekee,Kibulwa,Huba wangu,Mapenzi sio masihara,Wanaume wa leo,Clara,Mayasa,Wema wangu,Double double,Mabruki,Anjelu,Balimwacha,Kazi yangu Baharia,Mapenzi ya pesa na nyingnie nyingi....Hawa jamaa wanaweza kuwa wanaongoza Tanzania kwa kuwa na nyimbo nyingi sana....
Bendi hii imewahi kuwa na wanamuziki kama Tshimanga Kalala Assosa,Issa Nundu,Mukumbule Lulembo 'Parash',Mbuya Makonga 'Adios',Ilunga Banza Mchafu.Dekula Kahanga 'Vumbi',Bobo Sukari,Fredito Butamu,Mbwana Kocks,Kabea Badu,Mutombo Lufungula Audax,Matei Joseph,Kaumba Kalemba,Mukuna Roy,Berry Kankonde,William Maselenge,Seif Said,Nguza Vicking,Kyanga Songa,Kasaloo Kyanga,Kiniki Kieto na wengine kibao..............
Hakika ya kale ni dhahabu...
Nashukuru mkuu nimeamini jf hakishindikani kitu, siku zote nilidhani kwenye wimbo wa Mwamvua ni kishwahili tupu lkn nilipousikia kwenye kipindi kinachorushwa kila ijumaa na redio flani sipendi kuitaja nikagundua kile sio kiswahili, bahati namba ya muendesha kipindi nnayo maana anapenda kuitaja ili mwenye swali amuulize nami nikampigia lakini alijibu kwa jazba kuwa "kila siku najibu hilo swali akakata simu" nilimsamehe bure na kumtumia msg kuwa umeshajitolea kuwa muelimishaji usiwe na jazba ualimu ni wito, nikaona ngoja niende kwa Balantanda na kweli japo sio yeye aliyejibu nimefarijika kuona wataalamu wapo wengi. Nashauri tuwe tunapita hapa mara kwa mara tusipotee sana. kwenye Mwamvua Jerry anasema
"Pesa yeyeye pesaa pesaaa ye ye ye ye x2 subiri kidogoo mamy haiyeaye mamaa pesa zinazonisumbua ee mama aiyeaye mamaa, usinione hivi mamiii haiyeaye mamaa pesa zinazonisumbua ee mama aiyeaye mama". sasa panapofuata mi nilikuwa nachapia kwa kishwahili kuwa ni "Nyota na mwezi na ardhi mama ooh nyota na mwezi na ardhi mama ooh, nyota na mwezi na ardhi mamamama Mwamvua mamaaa". Ni juzi ndio nimegundua ni kilugha.
Hyo radio station ni Radio One, na mtu anayezungumzwa hapo bila shaka atakuwa ni Zomboko Rajabu ndo anakuwaga na jazba wakati mwingine, namba yake ni 0713 670065
Salama wakuu?,ni jumapili nyingine tulivu....
Leo naomba tujikumbushe bendi zetu zilizotamba sana miaka ya 80 na 90,bendi ambazo ama zimekufa ama zinaendelea kusuasua na ambazo ukisikiliza muziki wake leo hii unatamani ungerudisha wakati nyuma.......
Kwa kuanzia tuanze na hawa Orchestra Vijana Jazz,bendi ambayo ilikuwa ikimilikiwa na Umoja wa vijana wa CCM,bendi hii ilikuwa ikitumia mitindo ya Sindimba,Hekaheka,Heka koka,Watoto wa nyumbani,Air Pambamoto(awamu ya kwanza na ya pili) na baadae mtindo wa Saga Rhumba.....
Kwangu mimi bendi hii ndiyo ilikuwa chaguo langu hasa......Ukitaka kuujua ukali wa bendi hii sikiliza nyimbo kama Chiku,Mary Maria,Penzi lamea penye penzi,Shemeji,Bujumbura,Ilikuwa lifti,Tambiko la Pambamoto,Adza(Aza),Ngapulila,Ogopa Tapeli,Mwisho wa Mwezi,Penzi haligawanyiki,Wivu,Malaine,Nyongise,Shoga,Theresa,V.I.P,Mama Chichi na nyingine nyingi tu tamu....
Bendi hii imewahi kuundwa na wanamuziki kama Hemed Maneti 'Chiriku',Hamza Kalala 'Komando',Manitu Mussa,Issa Chikupele,Hassan Dalali,Hassan Shaw,Ally Jamwaka,Abuu Semhando,Bakari 'Baker' Semhando,Mhina Panduka 'Toto Tundu',Adam Bakari 'Sauti ya zege',Eddy Sheggy,Shaban Yohana 'Wanted',Rashid Pembe 'Profesa',Kida Waziri,Beno Villa Anthony,Rahma Shally,Jerry Nashon 'Dudumizi',Suleiman Mbwembwe,Shaban Dogodogo,Aggrey Ndumbalo,John Kitime,Abdallah Mgonahazelu,Freddy Benjamin,Mohammed Gotagota,Said Hamis 'Misukosuko',Athumani Momba na wengine kibao...