ZILIPENDWA: Wanamuziki, nyimbo na mitindo yao

ZILIPENDWA: Wanamuziki, nyimbo na mitindo yao

Mkuu SI WAZURI BINADAMU imeimbwa na BICHUKA lakini akiwa na OSS sio MLIMANI PARK. "Ninakushukuru Mungu huso mshirikae kuiponya roho yangu ilotaka toweka binadamu madhurumu ana vituko vya sumu anavituko vya sumu kali kushinda ya nyokae si wazuri binadamu usione wachekaa ooh nhon."
Kweli mdau,upo sahihi
 
Hizi nyimbo na mie Mhhhhh! lakini siku za karibuni nimeanza kusikia chache ambazo zinanigusagusa.

Bongo fleva bwana ni shida tupu. Yaani mtu anakopi beats kisha analilia kazi yake ilindwe. Sasa kazi gani anayotaka ilindwe wakati muziki si wake? Radio za Tanzania inabidi waturudishie vipindi vyetu vya muziki wa nyumbani, yaani tunaonekana wajinga kwa kupiga nyimbo za kijinga na kukopi vitu vya hajabu hajabu bila mtazamo wowote ule.
 
Last edited by a moderator:
  • Thanks
Reactions: BAK
Naikumbuka siku ileeee ulipokuja asubuhi na mapema,
........

wimbo huo nautafuta sana, sikumbuki jina lake wala walioupiga

Huu wimbo ninao, nimejaribu ku-upload kwenye jf nimeshindwa.
 
Sikinde wapo mkoani mwanza kwa mwaliko wa Bendi ya Mwanza Carnival...
 
Dah.....

Wakuu jioni ya leo nimepata habari mbaya kabisa ambazo ni za kusikitisha....

Mtaalamu KABEYA BADU amefariki jioni ya leo...

R.I.P KABEYA BADU
 
Shikamoo Jazz was formed in Dar Es Salaam in October 1993 by a coterie of veteran musicians who were determined to recreate the glorious sounds of the heyday of Tanzanian jazz (dansi music) and in so doing ensure their economic livelihood at an age when elderly musicians have usually decided to hang up their horns.

They consists of band members: Iddi Nhende manager/vocals/percussion, Salum Zahoro Guitars, vocals, John Simon Vocals/percussion, Juma Mrisho Vocals, Athumani Manicho Drums, Kassim Mponda Guitars, Ali Adinani Guitars, Mohammed Tungwa Bass and guitars, Madar Msellem Trumpet, Bakari Majengo Sax/conga, Ally Rashid Sax/conga

Shikamoo Jazz Band - ''Kibwana Maradhi Yamemuondoa''

Source: soukousman wa youtube
 
Last edited by a moderator:
na hizi nyimbo za za mani ni website gani tunaweza kuzisikilza nipeni hebu jamani kama kuna mtu anajua
 
Wakuu, je hawa ni Masantula Ngoma ya Mpwita Orch Safari Sounds au Orch. Maquiz du Zaire chekechaa au Orch.Safari Nkoy? wakuu najua Jamiiforums mtatupatia majibu:

Orchestre Safaris Nkoy - Mijumbe Ya Kasongo (Ndala Kasheba):
Published on 24 Mar 201370's Swahili Rumba aka Musiki wa Dansi! Ndala Kasheba was the main behind this band, if anybody has any additional information then comment below.

Source: soukousman youtube
 
Last edited by a moderator:
mama - tancut almasi orchestra

hii band ya tancut almsi kwa kweli................ Bado naitafuta album nzima yenye wimbo huu wa mama.

Balantanda bado naisubiri maana uliniahidi kunitafutia nyimbo original za hawa mapacha wa kikongo.

Ukitaka kusikiliza, basi pitia hapa: wanamuziki wa tanzania :: Music - reverbnation
hii bendi naivulia kofia kweli ilisheheni vipaji akina kasaloo(r.i.p),kyanga songa(r.i.p),kalala mbwembwe(r.i.p),dingituka morlay(r.i.p),john kitime,kawalee,hashim kasanga(r.i.p)
 
Aza - Vijana Jazz (Utunzi wake 'Chiriku' Hemed Maneti)

Aza ee umelikatili pendo langu,(Maneti) Aza Aza mbona nilikwisha kuamini,ahadi ya kwetu,ahadi ya ndoa vipi sasa Aza eeh

Mama yoyoyoyoyo sheri wangu Aza ee,Mama yoyoyoyoyo sheri wangu Aza ee,Mama yoyoyoyoyo Azamela naumia(rudia tena)

Barua yako Aza eeh ilinishangaza hasa ulipoeleza umevunja mipango ya ndoa,lakini Aza ni kipi kilichokusibu hadi Aza ugeuke na kumbe tulishapanga

Barua yako Aza eeh ilinishangaza hasa ulipoeleza umevunja mipango ya ndoa,lakini Aza ni kipi kilichokusibu hadi Aza ugeuke na kumbe tulishapanga

Ningelikwisha oa toka siku za nyuma,lakini ilibidi nisubiri ahadi,umalizie kozi,ya masomo Tabora

Ningelikwisha oa toka siku za nyuma,lakini ilibidi nisubiri ahadi,umalizie kozi,ya masomo Tabora

Aza Aza mama umenipa aibu kwa ndugu na jamaa zangu Aza ee,Aza Aza mama umenipa aibu kwa ndugu na jamaa zangu Aza ee

(Maneti)Matarajio yangu Aza ee,ni kushi pamoja vipi leo Aza ee umenigeuka

(Maneti)Aza wangu mama ee unanishangaza Aza ee,vip leo Aza ee umenigeuka

Yaliyopita si ndwele - Washirika Tanzania Stars (Utunzi wake 'Komando' Hamza Kalala)

Nimekusamehe lakini sitokusahau visa ulivyonitendea Kalala ee eeh,visa ulivyonitendea Kalala ee eeh

Ulinikana ee wakati mi na shida,ukasahau yote tuliyofanya nawe,wakati unaelewa hakuna Komando wa shida,wakati unaelewa hakuna Bingwa wa shida,leo nakukumbusha shida huja na kupita,yaliyopita si ndwele tugange yajayo kakaa mimi nakusamehe lakini sitokusahau,lalalala lalalala laaaa,lalalala lalalala mimi nimekusamehee,lalalala lalalala laaaa,lalalala lalalala mimi nimekusamehee

(Eddy Sheggy) Nimekusamehe lakini sitokusahau

Nimekusamehe lakini sitokusahau visa ulivyonitendea Kalala ee eeh,visa ulivyonitendea Kalala ee eeh

Ulinikana ee wakati mi na shida,ukasahau yote tuliyofanya nawe,wakati unaelewa hakuna Komando wa shida,wakati unaelewa hakuna Bingwa wa shida,leo nakukumbusha shida huja na kupita,yaliyopita si ndwele tugange yajayo kakaa mini nakusamehe lakini sitokusahau,lalalala lalalala laaaa,lalalala lalalala mimi nimekusamehee,lalalala lalalala laaaa,lalalala lalalala mimi nimekusamehee

Rafiki wa kweli ni yule asiyekutupa ee kwenye dhiki na faraja mko wote mko wote,kwenye dhiki na faraja oooh oooh,uliniacha nateseka peke yangu peke yangu,pasipo msaada wowote kaka oo oooh,pasipo msaada wowote kaka oo oooh,lakini mola muweza wa yote(wa yote) kaninusuru na matatizo yamepita o kaka,kweli nimekusamehe lakini sitokusahau,yaliyopita si ndwele tugange yajayo kaka,kweli nimekusamehe lakini sitokusahau,yaliyopita si ndwele tugange yajayo kaka,lalalala lalalala laa,lalalala lalalala mimi nimekusamehe,alalala lalalala laa,lalalala lalalala mimi nimekusamehe
 
Milima ya Kwetu 1 - Super Rainbow Band (Utunzi wake Eddy Sheggy, waimbaji Eddy Sheggy na Emma Mkelo 'Lady Champion')

Nikitazama milima ya kwetu ee,
machozi yanitoka kwa uchungu na mawazo,
tulitoka wawili ninarudi peke yangu,
baba na mama wataniuliza bibi yako yuko wapi ee,
Ndugu jamaa wataniuliza bibi yako yuko wapi eee,

japokuwa ninakaribia kufika nyumbani ee,
Ninatamani gari isifikie upeesi,
kwa ile aibu nitakayopata mbele ya wazazi ii,
kwa vile ni miezi michache imepita nilitoka na bibi yangu,

(Eddy)
Nitasema nini kwa baba mimi najuta aa,
kwa pesa zake nyiingi alizopotezaa,
harusi ilifanyika kwa gharama kubwa sana,
watu walikula na kunywa na kusaza mamaa,

Nikaenda kuishi na bibi yule mjini,
kazi yake ilikuwa ni vituko,
nikaenda kuishi na bibi yule mjini kazi yake ilikuwa ni vitiimbwi,

Alianza kuweka sukari kwenye mboga,
nikaonja haviliki tukalala na njaa,

kafuatia na kuweka chumvi kwenye chai,
nilikuwa na wageni wakatoka bila kuaga,

kafuatia kuchelewa akienda sokoni,
nikimuuliza anitukana hadharani aibu,

kuna gari imekuja hadi mlangoni,
kujitetea akasema mjomba wake kaja,

hivi juzi kavunja kioo cha dirisha,
apate kuchungulia wapitao njiani,

hatimaye kunibeza na kunidharau,
shikamoo ikaisha ikabaki
Vipi babu, mambo zakoo ee x2

Nilishindwa kumuuliza ee sikutaka kumuudhi,
sababu nilikuwa nampenda nampenda saana x 2

chorus:

walisemaa dalili ya mvua ni mawingu,
niliyempenda kanitoroka mama,

(Eddy Sheggy)
Nilinyang'anywa tonge mdomoni,
nilinyang'anywa tonge kinywani,
niliyempenda kanikimbia mama yoyo,
niliempenda kanikimbia masikini nifanye nini mama,

(chorus)

Vituko ee, vituko vya bibi huyoo,
sitaweza kusahau mimi oo mama ee,
sitaweza kusahau mimi oo sheggy ee,
alikuwa kama helikopta, ndege isiyochagua mahali pa kutua ee,
kila mtaa hapa mjini jamani tazameni oo,
ana bwana mmoja ama wawili mama mama oo,
nifanye nini mama oo,

(chorus)
 
Mama Chichi - Vijana Jazz (utunzi wake Suleimani Mbwembwe)

Mara nyingi duniani mtu hukisifu kilicho chake,ni vizuri duniani mtu kukisifu anachopenda

Mara nyingi duniani mtu hukisifu kilicho chake,ni vizuri duniani mtu kukisifu anachopenda

Kwa hiyo na mimi aa kwako Diana sina budi kufanya hivyo,Kwa hiyo na mimi aa kwako Diana sina budi kufanya hivyo.
Kwa vile unatimiza yale yote ambayo anayostahili kuyatenda mke wa mtu

Mara nyingi duniani mtu hukisifu kilicho chake(kilicho chake),ni vizuri duniani mtu kukisifu anachopenda(anachopenda)

Aiyolele iyo mama Chichi yeye(we mama),aiyolele iyo mama Chichi mama

Aiyolele iyo mama Chichi yeye(we mama),aiyolele iyo mama Chichi mama

(Mbwembwe)Barafu ya roho yangu mama Chichi mama mwenye mahaba ya Kipangani mama Chichi,yanayofanana na yale ya njiwa manga tunduni,sikiliza ninayosema mama Chichi mama

Aiyolele iyo mama Chichi yeye(we mama),aiyolele iyo mama Chichi mama

Aiyolele iyo mama Chichi yeye(we mama),aiyolele iyo mama Chichi mama

Barafu ya roho yangu mama Chichi mama mwenye mapenzi ya Kizamani mama Chichi,yanayofanana na yale ya njiwa manga tunduni,sikiliza maneno yangu mama Chichi mama

Aiyolele iyo mama Chichi yeye(we mama),aiyolele iyo mama Chichi mama

Aiyolele iyo mama Chichi yeye(we mama),aiyolele iyo mama Chichi mama

(Momba)Maisha ni safari ndefu itabidi tuheshimiane tujichunge na vizabizabina(zabina),maisha ni safari ndefu itabidi tuelewane na kila kwenye makosa tukosoane mama Chichi ee

Aiyolele iyo mama Chichi yeye(we mama),aiyolele iyo mama Chichi mama

Aiyolele iyo mama Chichi yeye(we mama),aiyolele iyo mama Chichi mama,malkia wa nyumba yangu mama Chichi mama

Maisha ni safari ndefu itabidi tuheshimiane tujichunge na vizabizabina(zabina),maisha ni safari ndefu itabidi tuelewane na kila kwenye makosa tukosoane mama Chichi ee

Aiyolele iyo mama Chichi yeye(we mama),aiyolele iyo mama Chichi mama

Aiyolele iyo mama Chichi yeye(we mama),aiyolele iyo mama Chichi mama,malkia wa nyumba yangu mama Chichi mama

Kasoro za binadamu tangu enzi na enzi ni kutopenda maendeleo ya mwingine(kama kiwangawanga) lakini sisi tupendane mapenzi ya njiwa kwani upendo na uaminifu ndiyo heshima ya ndoa

Nawe nami bara mpaka pwani,pamba moto shambuliaa
Nawe nami bara mpaka pwani,pamba moto shambuliaa
Nawe nami bara mpaka pwani,pamba moto shambuliaa

Saga saga rhumba,saga saga rhumba
 
Pia kuna Orch. Marquiz Original,kundi hili liliundwa miaka ya 70 na wanamuziki waliotoka katika jimbo la Shaba nchini Zaire(DRC) waliingia nchini wakiitwa Orchestre Super Gabby,baada ya kuingia nchini walibadilisha jina na kuanza kuitwa Orchestra Maquis du Zaire/Marquis Original.....Mitindo waliyoitumia ni pamoja na Ogelea Piga Mbizi,Zembwela na Sendema.....Ukumbi waliokuwa wakipiga(uwanja wao wa nyumbani) ni Lang'ata Social Hall pale Kinondoni(FM Club ambapo kwa sasa ni kanisa).....Hawa pia walikuwa wanaujua muziki hasa kutokana na aina ya muziki mchanganyiko wa kizaire(kavasha) na vionjo vya kitanzania walivyopiga....

Bendi hii ilitamba na nyimbo nyingi sana,nyimbo kama Mayanga,Ngalula,Makumbele,Mpenzi Luta,Mpenzi Scola,Karubandika,Seya,Tipwatipwa,Kisabengo,Wakati nilikuwa mdogo,Bi Sofia,Hali ngumu,Ni wewe pekee,Kibulwa,Huba wangu,Mapenzi sio masihara,Wanaume wa leo,Clara,Mayasa,Wema wangu,Double double,Mabruki,Anjelu,Balimwacha,Kazi yangu Baharia,Mapenzi ya pesa na nyingnie nyingi....Hawa jamaa wanaweza kuwa wanaongoza Tanzania kwa kuwa na nyimbo nyingi sana....

Bendi hii imewahi kuwa na wanamuziki kama Tshimanga Kalala Assosa,Issa Nundu,Mukumbule Lulembo 'Parash',Mbuya Makonga 'Adios',Ilunga Banza Mchafu.Dekula Kahanga 'Vumbi',Bobo Sukari,Fredito Butamu,Mbwana Kocks,Kabea Badu,Mutombo Lufungula Audax,Matei Joseph,Kaumba Kalemba,Mukuna Roy,Berry Kankonde,William Maselenge,Seif Said,Nguza Vicking,Kyanga Songa,Kasaloo Kyanga,Kiniki Kieto na wengine kibao..............

Hakika ya kale ni dhahabu...

Aisee Balantanda unatisha sana, hapo naupenda sana wimbo huo wa Bi Sophia, hapo NGUZA VIKINGI kapiga solo balaa, dah wimbo mzuri sana huo waga naurudiaga hata mara 6 nikiwa peke yangu, maana watu wangu wengi wa karibu hawazipendi nyimbo hizi
 
Nashukuru mkuu nimeamini jf hakishindikani kitu, siku zote nilidhani kwenye wimbo wa Mwamvua ni kishwahili tupu lkn nilipousikia kwenye kipindi kinachorushwa kila ijumaa na redio flani sipendi kuitaja nikagundua kile sio kiswahili, bahati namba ya muendesha kipindi nnayo maana anapenda kuitaja ili mwenye swali amuulize nami nikampigia lakini alijibu kwa jazba kuwa "kila siku najibu hilo swali akakata simu" nilimsamehe bure na kumtumia msg kuwa umeshajitolea kuwa muelimishaji usiwe na jazba ualimu ni wito, nikaona ngoja niende kwa Balantanda na kweli japo sio yeye aliyejibu nimefarijika kuona wataalamu wapo wengi. Nashauri tuwe tunapita hapa mara kwa mara tusipotee sana. kwenye Mwamvua Jerry anasema
"Pesa yeyeye pesaa pesaaa ye ye ye ye x2 subiri kidogoo mamy haiyeaye mamaa pesa zinazonisumbua ee mama aiyeaye mamaa, usinione hivi mamiii haiyeaye mamaa pesa zinazonisumbua ee mama aiyeaye mama". sasa panapofuata mi nilikuwa nachapia kwa kishwahili kuwa ni "Nyota na mwezi na ardhi mama ooh nyota na mwezi na ardhi mama ooh, nyota na mwezi na ardhi mamamama Mwamvua mamaaa". Ni juzi ndio nimegundua ni kilugha.

Hyo radio station ni Radio One, na mtu anayezungumzwa hapo bila shaka atakuwa ni Zomboko Rajabu ndo anakuwaga na jazba wakati mwingine, namba yake ni 0713 670065
 
Hyo radio station ni Radio One, na mtu anayezungumzwa hapo bila shaka atakuwa ni Zomboko Rajabu ndo anakuwaga na jazba wakati mwingine, namba yake ni 0713 670065

tawile mkuu, namkubali sana kwa uchabuzi wake na karibu kila wiki natenga muda wa kufuatilia kipindi chao lakini siku hiyo ainisikitisha. lakini nimemsamehe tu maana hakuna mkamilifu na inategemea aliamka vipi maana siku hazifanani.
 
wadau naomba mwenye mashahili au audio wimbo wa chiku ulioimbwa na kimulimuli aiwekee hapa jamii.
 
Salama wakuu?,ni jumapili nyingine tulivu....

Leo naomba tujikumbushe bendi zetu zilizotamba sana miaka ya 80 na 90,bendi ambazo ama zimekufa ama zinaendelea kusuasua na ambazo ukisikiliza muziki wake leo hii unatamani ungerudisha wakati nyuma.......

Kwa kuanzia tuanze na hawa Orchestra Vijana Jazz,bendi ambayo ilikuwa ikimilikiwa na Umoja wa vijana wa CCM,bendi hii ilikuwa ikitumia mitindo ya Sindimba,Hekaheka,Heka koka,Watoto wa nyumbani,Air Pambamoto(awamu ya kwanza na ya pili) na baadae mtindo wa Saga Rhumba.....

Kwangu mimi bendi hii ndiyo ilikuwa chaguo langu hasa......Ukitaka kuujua ukali wa bendi hii sikiliza nyimbo kama Chiku,Mary Maria,Penzi lamea penye penzi,Shemeji,Bujumbura,Ilikuwa lifti,Tambiko la Pambamoto,Adza(Aza),Ngapulila,Ogopa Tapeli,Mwisho wa Mwezi,Penzi haligawanyiki,Wivu,Malaine,Nyongise,Shoga,Theresa,V.I.P,Mama Chichi na nyingine nyingi tu tamu....

Bendi hii imewahi kuundwa na wanamuziki kama Hemed Maneti 'Chiriku',Hamza Kalala 'Komando',Manitu Mussa,Issa Chikupele,Hassan Dalali,Hassan Shaw,Ally Jamwaka,Abuu Semhando,Bakari 'Baker' Semhando,Mhina Panduka 'Toto Tundu',Adam Bakari 'Sauti ya zege',Eddy Sheggy,Shaban Yohana 'Wanted',Rashid Pembe 'Profesa',Kida Waziri,Beno Villa Anthony,Rahma Shally,Jerry Nashon 'Dudumizi',Suleiman Mbwembwe,Shaban Dogodogo,Aggrey Ndumbalo,John Kitime,Abdallah Mgonahazelu,Freddy Benjamin,Mohammed Gotagota,Said Hamis 'Misukosuko',Athumani Momba na wengine kibao...

Sasa huwezi kuamini juzi nimeenda South Africa nikakuta audio CD orijino ya vijana jazz ya 1975 wakitumia style ya koka koka.
imerekodiwa ujerumani na ina nyimbo 12 ukiwemo ule wa Niliruka ukuta.
 
Back
Top Bottom