ZILIPENDWA: Wanamuziki, nyimbo na mitindo yao

Sasa huwezi kuamini juzi nimeenda South Africa nikakuta audio CD orijino ya vijana jazz ya 1975 wakitumia style ya koka koka.
imerekodiwa ujerumani na ina nyimbo 12 ukiwemo ule wa Niliruka ukuta.


Wanaiuza bei gani?
 
Yani kipande hiki cha hapa nilikuwa na wageni wakatoka bila kuagaaaa! kinanikumbusha siku naangalia final euro 2008 Spain vs Germn final,mimi pekee nilikuwa nasapoti Spain wote wenzangu walikuwa German sasa Torres akawafunga halafu karibia mpira unaisha huu wimbo ukapigwa basi na wengi wao wakaanza kuondoka mmoja mmoja bila kuagaaaaa! samahani lakini nimeingiza mada ya soka.:heh:
 
Oh baba mapenzi ya pesa kaka ni ya shida kwelimkwa mbele ya wandugu dada nakuambia yote lakini mapenzi ya pesa si ya kweli dada aa dada aa,waniumiza roho oh Tabu Ley na Mbilia Bel intro hiyo anaejua vizuri amalizie
 
Official Vijana Jazz Orchestre known as Sagarumba Air Pamba Moto distributed by Viva Conscious arts Presenting ..Its Tanzanian music Gerned Rhumba .enjoy and rate it ..
+255712845804
+255756694227
Its Official Number of VIJANA JAZZ BAND source: Joseph viva Stephen wa Youtube- Vijana Jazz Orchestre (Sagarumba Air Pamba Moto)-
 
Last edited by a moderator:
Kaka unatisha enzi hizo ni noma
 
Mark Africa Band - MATUKIO source: markafricaband wa youtube
 
Last edited by a moderator:
Super Kamanyola Band wakiendeleza ''Sendema ya Moto' muziki wa dansi ya iliyokuwa Maquiz Orignal, wakiwa ndani ya ukumbi wa Villa Park Resort, Jijini Mwanza wakifanya vitu vyao chini ya Parashi, Roy Mukuna na wengineo: source: 00051 Avondje stappen Anne Kuijs wa youtube : Live music in Villa Park, Mwanza Jarmo wa youtube
 
Last edited by a moderator:
Da, vijana Jazz usipime wandugu. Ule uliluwa muziki hasa wa Ki-Tanzania. Bantu Group nayo ilikuwa hatari. MCA International,Bimalee, Washirika Tanzania Stars, DDC, Juwata/OTTU, ZAITA Musica, Police kutaja chache.
 

Sory kwa kuchelewa kujibu mkuu wangu sana Mnyalu..........

Huu hapa wimbo wa Mazoea yananikondesha kutoka kwa Mzinga Troupe utunzi wake Issa Mrisho amb aye pia ndiye aliimba wimbo huu....


Mazoea yananikondeshaaaa eeeeee,
Nimpendae kachukuliwa eeeh mamaaa,
Wala sina la kutamka, wenye nguvu wamerudia eeeh!,
Wala sina pa kushitaki, wenye nguvu wamerudia eeh eeh...

Tuliishi bila matatizoo, nyumbani vitu teletele wallahi oooh,
Kama mimi nina kasoro wandugu natakanijulishweeee,
Aaaah, kwa ninimumezoea kunichukulia nimpendaeee.....

Daima hakutenda ovu wala sikutenda ovu lililoacha makovu ya kutokusahau mileleeee....

Aaah, sikutenda ovu la kuweza kulipwa kisasi, wala hakutenda ovu la kutokusahau milele,
Oooh, tuliishi kwa mapendo mamaaaa aaah aaah....

Mazoea, mazoea yananikondeshaa.....

Kinachonifanya nisemee, sio sifa ya uzuri wake tuuu,
Ama sitopata zaidi yake aaah aaah,
Ama nimeshakula kizizi labda lakini siamni,
Alijua matatizooo, kweli nasema mtoto kalelewaa....

Kinachonifanya nimuwazee, sio sifa ya upole wake tuu,
Ama sifa zake nyingine aaah, hapana alijua matatizoo,
Kwa haki nasema Mungu amjalieeee,
Walimwengu mama eeeh eeeh, walitaka niteterekeee....

Mbona mjusi ama Kinyonga, anapata riziki yake,
Tena hula vijidudu hai, hasa vyenye kurukaruka,
Mbona yeye hana mbawaa, hana makucha wala vikumboo,
Hashiki panga wala bundukii, masikini eeeh, unamtosha ulimi wakee,
Sembuse mimi mwanadamuuuu.....Mazoea yananikondesha eeeh eeeh.....

Mbona mjusi ama Kinyonga, anapata riziki yake,
Tena hula vijidudu hai, hasa vyenye kurukaruka,
Mbona yeye hana mbawaa, hana makucha wala vikumboo,
Hashiki panga wala bundukii, masikini eeeh, unamtosha ulimi wakee,
Anakula kwa ulimi wakee, anashiba kwa ulimi wakee,
Anapata riziki kwa ulimi wakee,sembuse mimi mwanadamuuuu.....

 
Laah, aisee kali kweli balantanda umetukumbusha mbali.
 
Thanks a lot mkuu. Kwa hakika huu wimbo huwa unaniburudisha sana, kwa namna ulivyoimbwa na ujumbe. Good composition. Sijui tutawapata wapi akina Mrisho wengine miaka hii ya leo.
 
Odama Band ikitoa burudani ya muziki wa dansi jijini Dar-es-Salaam, Aug 10, 2013 kwa cover wimbo original 'AFRO' wa Simba Wanyika Source: Ahmad Michuzi wa youtube.
 
Last edited by a moderator:

Hapa naona umemsahau mzee King Kiki....🙂
 

Yaani hiki kitu kimekaa sawa mno, hawa so-called producer wa Bongo fleva wanatakiwa wawe wanasikiliza hizi rare gems....:A S-fire1:
 
Last edited by a moderator:
Reactions: BAK
Umeona eeh! Msondo ngoma hao banaaa!!! Kitu kimepangika na kimetulia mnooo, siyo hizi Bongo Fleva.


Yaani hiki kitu kimekaa sawa mno, hawa so-called producer wa Bongo fleva wanatakiwa wawe wanasikiliza hizi rare gems....:A S-fire1:
 
Last edited by a moderator:
Umeona eeh! Msondo ngoma hao banaaa!!! Kitu kimepangika na kimetulia mnooo, siyo hizi Bongo Fleva.



Mkuu
Ngoma hii nayo imetulia, yaani hapa unaweza tengenezea hawa vijana wa b-fleva beat moja kali sana, unafanya loop/sample ya hilo pini kuanzia hapo 0:08 min (tan tan tatanh tan tan tantaah tan tan tataaah), unacombine na rythm guitar inayoanzia 1:03 weka hi-hat na drums tulivu na vichombwezo viwili vitatu basi umemaliza....kijiwe cha BET nominations hicho lol...

Sijui huwa wanasilikiliza nini hawa vijana...:tape:
 
Last edited by a moderator:
Reactions: BAK
Msondo ngoma ni kama Zaiko Langa langa ya Congo.mziki umetulia
 

Mkuu hizo Nyimbo hazina mwenyewe zipo free sababu zamani hatukuwa na sheria kali na wanamuziki wa zamani walikuwa wakiimba kama sehemu ya starehe tu na sio Biashara sana RTD ndio waliwaingiza mkenge wakiwaambia kama wanataka sawa kama hawataki wasepe wengi walikubali ili wasikike tu.... pesa walikuwa wakizipata kwenye live tu so hadi sasa huyo anayesimamia atakuwa ni mwizi tu.... unaposema aende dukani akanunue hizo pesa zitaenda kwa nani?
 

Haya kazi kwako mkuu Bujibuji
 

Attachments

Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…