ZILIPENDWA: Wanamuziki, nyimbo na mitindo yao

Waeleze wapenzi wafute , kabla ya mp3 waweke . ili wazifaidi
 
Sijaelewa hapo kaka wafute mp3 /hiyo ni non stop inaimba kwa saa moja na dakika ishirini nyimbo zote ni zile zilizopendwa kwa kiwango cha juu wanaweza sikiliza online nyimbo nne za mwanzo then utaweza pata picha fulani juu ya nyimbo za nyakati gani tunazungumzia
 

Rafiki, unakumbuka wimbo mmoja ulipigwa na Ndekule sikumbuki vizuri mashairi yake lakini ukienda hivi:

Mapenzi yananipa tabu jamaniee
Moyo waniuma sikia we mamaee
machozi yanitoka wakati wote
Nategemea kufunga ndoa nawewe ohhoo sofi

Nadhani ukiitwa Sofi
 
Nawatakiwa maandalizi mema ya Krismas na Mwaka mpya 2014

Balantanda

DDC walikuwa na gate keeper wao anaitwa KITWANA!Huyu jamaa aliwahi nikunja shati pale DDC-Magomeni kwa madai eti sijampa ticket so nataka kuingia kwa ujanja ujanja!

Ukweli wenyewe ticket nilimpa na aliichana kuashiria niingie!DDC walikuwa wanaujua sana muziki!
 
Last edited by a moderator:
Nawatakia Heri ya Mwaka mpya wa 2014 wadau wote wa Jukwaa hili..

Kila la heri...
 
Nawatakia Heri ya Mwaka mpya wa 2014 wadau wote wa Jukwaa hili..

Kila la heri...

Rafiki, unakumbuka wimbo mmoja ulipigwa na Ndekule sikumbuki vizuri mashairi yake lakini ukienda hivi:

Mapenzi yananipa tabu jamaniee
Moyo waniuma sikia we mamaee
machozi yanitoka wakati wote
Nategemea kufunga ndoa nawewe ohhoo sofi

Nadhani ukiitwa Sofi
 
Nawatakia Heri ya Mwaka mpya wa 2014 wadau wote wa Jukwaa hili..

Kila la heri...

Balantanda, kama ukiniwekea mashairi ya wimbo: Shahada ya Uvumilivu. Tunaambiwa ni kisa cha kweli.Naomi wa DDC,Ukewenza/ Kulala Sebuleni-Washirika. Pia Vijana Jazz: Top Queen, Visa vya mume( nikipika ugali unasema una mabuja, nikipika wali unasema una mawe, sema kinachokukera bwanaa ee),daa hadi raha. Shoga, V.I.P, Kapu la mjanja. Bantu Group- Baba Jane 1&2, mwaka mpya. Bimalee- Busu pande tatu, Makulata. Kama mzee John Kitime yumo humu jamvini yumo aje atupe uhondo. Huu music wa kubana sauti umenichosa sana. Na kwa bahati mbaya TBC nao wamekuwa .com, ni nadra sana kupiga nyimbo hizi. Hata vipindi ambavyo ilikuwa ni kichochoe cha nyimbo hizi havipo tena, labda kutokana na mabadiliko wa technology. Vipindi kama,jambo, pole kwa kazi,kombora, mchana mwema, misakato, club rahaleo show, chaguo la msikilizaji n.k. Ikumbukwe kuwa huwezi kukumbuka muziki wa dansi usihusishe RTD.
 
Nzuri mkuu....

Nyimbo nyingi ulizozitaja zipo humu....Fuatilia thread toka mwanzo mpaka hapa...
 
Masoud Masoud anamhoji Mutombo Lufungulo Odax...mmoja wa waanzirishi wa Bendi ya Marquees...87.5 FM
 
Balantanda (PhD)

Kuna wimbo ulikuwa una maneno haya:

....Unamtukana mke wangu nikiwa sipooo
Unamsimanga mke wangu eti kwao masikini, masikiniii, loh, mama Musa!


Chorus//

...Mama musa mama, kosa gani nimekukosea, iwapo nimekukosea, naomba unisamehe...


Nitashukuru kama unaweza kutukumbusha lyrics zake na details zingine.
 
Last edited by a moderator:

sikuwepo kipindi wimbo wa mzinga troupe mazoea unatoka ila huwa nikiusikiliza na-realize hicho ndo kipindi muziki ulikuwa muziki kweli... Maana hauchoshi kuusikiliza...
 
Kuna SALAMU BABA NA MAMA wa NATIONAL SERVICE JAZZ BAND...
 
Jaman kuna wimbo wa kasaro n kyanga unaitwa talaka mwenye nao anisaidie hata kwa PM
 
Nzuri mkuu....

Nyimbo nyingi ulizozitaja zipo humu....Fuatilia thread toka mwanzo mpaka hapa...

Ok, nazitafuta ni duka gani hapa mjini mahsusi kwa CD ya nyimbo nilizozitaja? Nitashukuru nikiarifiwa
 
Kuna wimbo wa zamani unaitwa usiwe kidomidomi wa bendi ya amboni.mnaupata huo?
 
kuna wimbo wa mzee makassy siujui jina lake lakini ndani yake kuna mistari hii
"mtoto wa arusha mama mbona wanipa shidaa, mchana na usikuu nakuwaza wewe, warembo wengi nimewaona mamaa, lakini roho yangu imekupenda wewe.............
mapenzi ya pesa hayadumu mamaa, mapenzi ya kwelii ni ya maisha, nimekupenda na wewe umekubali, tukila kisamvu kaza roho mama, daresalam jiji umbea mwingi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…