ZILIPENDWA: Wanamuziki, nyimbo na mitindo yao

ZILIPENDWA: Wanamuziki, nyimbo na mitindo yao

Sijaelewa hapo kaka wafute mp3 /hiyo ni non stop inaimba kwa saa moja na dakika ishirini nyimbo zote ni zile zilizopendwa kwa kiwango cha juu wanaweza sikiliza online nyimbo nne za mwanzo then utaweza pata picha fulani juu ya nyimbo za nyakati gani tunazungumzia
 
Yaliyopita si ndwele - Washirika Tanzania Stars (Utunzi wake 'Komando' Hamza Kalala)

Nimekusamehe lakini sitokusahau visa ulivyonitendea Kalala ee eeh,visa ulivyonitendea Kalala ee eeh

Ulinikana ee wakati mi na shida,ukasahau yote tuliyofanya nawe,wakati unaelewa hakuna Komando wa shida,wakati unaelewa hakuna Bingwa wa shida,leo nakukumbusha shida huja na kupita,yaliyopita si ndwele tugange yajayo kakaa mimi nakusamehe lakini sitokusahau,lalalala lalalala laaaa,lalalala lalalala mimi nimekusamehee,lalalala lalalala laaaa,lalalala lalalala mimi nimekusamehee

(Eddy Sheggy) Nimekusamehe lakini sitokusahau

Nimekusamehe lakini sitokusahau visa ulivyonitendea Kalala ee eeh,visa ulivyonitendea Kalala ee eeh

Ulinikana ee wakati mi na shida,ukasahau yote tuliyofanya nawe,wakati unaelewa hakuna Komando wa shida,wakati unaelewa hakuna Bingwa wa shida,leo nakukumbusha shida huja na kupita,yaliyopita si ndwele tugange yajayo kakaa mini nakusamehe lakini sitokusahau,lalalala lalalala laaaa,lalalala lalalala mimi nimekusamehee,lalalala lalalala laaaa,lalalala lalalala mimi nimekusamehee

Rafiki wa kweli ni yule asiyekutupa ee kwenye dhiki na faraja mko wote mko wote,kwenye dhiki na faraja oooh oooh,uliniacha nateseka peke yangu peke yangu,pasipo msaada wowote kaka oo oooh,pasipo msaada wowote kaka oo oooh,lakini mola muweza wa yote(wa yote) kaninusuru na matatizo yamepita o kaka,kweli nimekusamehe lakini sitokusahau,yaliyopita si ndwele tugange yajayo kaka,kweli nimekusamehe lakini sitokusahau,yaliyopita si ndwele tugange yajayo kaka,lalalala lalalala laa,lalalala lalalala mimi nimekusamehe,alalala lalalala laa,lalalala lalalala mimi nimekusamehe

Rafiki, unakumbuka wimbo mmoja ulipigwa na Ndekule sikumbuki vizuri mashairi yake lakini ukienda hivi:

Mapenzi yananipa tabu jamaniee
Moyo waniuma sikia we mamaee
machozi yanitoka wakati wote
Nategemea kufunga ndoa nawewe ohhoo sofi

Nadhani ukiitwa Sofi
 
Nawatakiwa maandalizi mema ya Krismas na Mwaka mpya 2014

Balantanda

DDC walikuwa na gate keeper wao anaitwa KITWANA!Huyu jamaa aliwahi nikunja shati pale DDC-Magomeni kwa madai eti sijampa ticket so nataka kuingia kwa ujanja ujanja!

Ukweli wenyewe ticket nilimpa na aliichana kuashiria niingie!DDC walikuwa wanaujua sana muziki!
 
Last edited by a moderator:
Nawatakia Heri ya Mwaka mpya wa 2014 wadau wote wa Jukwaa hili..

Kila la heri...
 
Nawatakia Heri ya Mwaka mpya wa 2014 wadau wote wa Jukwaa hili..

Kila la heri...

Rafiki, unakumbuka wimbo mmoja ulipigwa na Ndekule sikumbuki vizuri mashairi yake lakini ukienda hivi:

Mapenzi yananipa tabu jamaniee
Moyo waniuma sikia we mamaee
machozi yanitoka wakati wote
Nategemea kufunga ndoa nawewe ohhoo sofi

Nadhani ukiitwa Sofi
 
Nawatakia Heri ya Mwaka mpya wa 2014 wadau wote wa Jukwaa hili..

Kila la heri...

Balantanda, kama ukiniwekea mashairi ya wimbo: Shahada ya Uvumilivu. Tunaambiwa ni kisa cha kweli.Naomi wa DDC,Ukewenza/ Kulala Sebuleni-Washirika. Pia Vijana Jazz: Top Queen, Visa vya mume( nikipika ugali unasema una mabuja, nikipika wali unasema una mawe, sema kinachokukera bwanaa ee),daa hadi raha. Shoga, V.I.P, Kapu la mjanja. Bantu Group- Baba Jane 1&2, mwaka mpya. Bimalee- Busu pande tatu, Makulata. Kama mzee John Kitime yumo humu jamvini yumo aje atupe uhondo. Huu music wa kubana sauti umenichosa sana. Na kwa bahati mbaya TBC nao wamekuwa .com, ni nadra sana kupiga nyimbo hizi. Hata vipindi ambavyo ilikuwa ni kichochoe cha nyimbo hizi havipo tena, labda kutokana na mabadiliko wa technology. Vipindi kama,jambo, pole kwa kazi,kombora, mchana mwema, misakato, club rahaleo show, chaguo la msikilizaji n.k. Ikumbukwe kuwa huwezi kukumbuka muziki wa dansi usihusishe RTD.
 
Nzuri mkuu....

Nyimbo nyingi ulizozitaja zipo humu....Fuatilia thread toka mwanzo mpaka hapa...
 
Masoud Masoud anamhoji Mutombo Lufungulo Odax...mmoja wa waanzirishi wa Bendi ya Marquees...87.5 FM
 
Balantanda (PhD)

Kuna wimbo ulikuwa una maneno haya:

....Unamtukana mke wangu nikiwa sipooo
Unamsimanga mke wangu eti kwao masikini, masikiniii, loh, mama Musa!

Chorus//

...Mama musa mama, kosa gani nimekukosea, iwapo nimekukosea, naomba unisamehe...

Nitashukuru kama unaweza kutukumbusha lyrics zake na details zingine.
 
Last edited by a moderator:
bala, huwakumbuki mzinga troupe ya moro? Waliibuka na kibao kiitwacho mazoea yanikondesha kilichotungwa na kuimbwa na issa mrisho kwa sauti nzuri sana. Kibao hicho kikipigwa hata leo utadhani ni cha jana. Baadhi ya masahiri ni haya

mazoea yananikondesha eee
sio kama nimelishwa kizizi, labda,
laini siamini alijua matatizo

hata mjusi hata kinyonga,
wao hula vijidudu hai
hasa vyenye kurukaruka, mbona yeye hana mbawaaaa
anapata riziki yakeee, sembuse mimi mwanadamu

bala, umtaja kurugenzi jazz, bila shaka ni ile ya arusha iliyokuwa na kibao kikali sana wivu

wivu ukizidi nyumbani mapenzi yapunguaa
wivu usiyo na maana waleta hasara
umefanya kitu gani, bibi umemkataza kufanya kazi
ati sababu wachelelewa nyumbani....

Kibwagizo
maisha ya leo, ni kufanya kazi
mke na mume, kusaidiana

sikuwepo kipindi wimbo wa mzinga troupe mazoea unatoka ila huwa nikiusikiliza na-realize hicho ndo kipindi muziki ulikuwa muziki kweli... Maana hauchoshi kuusikiliza...
 
Kuna SALAMU BABA NA MAMA wa NATIONAL SERVICE JAZZ BAND...
 
Jaman kuna wimbo wa kasaro n kyanga unaitwa talaka mwenye nao anisaidie hata kwa PM
 
Nzuri mkuu....

Nyimbo nyingi ulizozitaja zipo humu....Fuatilia thread toka mwanzo mpaka hapa...

Ok, nazitafuta ni duka gani hapa mjini mahsusi kwa CD ya nyimbo nilizozitaja? Nitashukuru nikiarifiwa
 
Kuna wimbo wa zamani unaitwa usiwe kidomidomi wa bendi ya amboni.mnaupata huo?
 
kuna wimbo wa mzee makassy siujui jina lake lakini ndani yake kuna mistari hii
"mtoto wa arusha mama mbona wanipa shidaa, mchana na usikuu nakuwaza wewe, warembo wengi nimewaona mamaa, lakini roho yangu imekupenda wewe.............
mapenzi ya pesa hayadumu mamaa, mapenzi ya kwelii ni ya maisha, nimekupenda na wewe umekubali, tukila kisamvu kaza roho mama, daresalam jiji umbea mwingi
 
sikinde.jpg
 
Back
Top Bottom