ZILIPENDWA: Wanamuziki, nyimbo na mitindo yao

sasa hivi maproducer mavi watakopi haya maandishi na kuharibu kabisa kwenye fleva.
 
Vijana walikuwa juu sana katika muziki hata upigaji na mpangilio wao wa vyombo tofauti kabisa na hizi bendi zilizokuwa zinajiita wazee wa muziki Bongo. Nyimbo za Vijana zilikuwa tamu sana mpaka sasa na ndiyo bendi pekee iliyopitiwa na wapiga solo hatari sana hapa nchini, nani anabisha?
 
kabla ya mwaka 2000 vijana ilikua juu kuliko ottu ebu sikiliza vibao kama tereza, mvuvi kinda, mwisho wa mwezi, bujumbura, aza, shingo feni mfano ile albam ya top quine kunzia muziki wa kwanza mpaka wa mwisho huwezi kukaa isipokua mama wa kambo tu
 
jamani kama kuna mtu anavibao vya tereza na mvuvi kinda maana mjaruo jery nashon dudumizi alitisha RIP wekeni hapa jf tu download
 
jamani kama kuna mtu anavibao vya tereza na mvuvi kinda maana mjaruo jery nashon dudumizi alitisha RIP wekeni hapa jf tu download

Nenda youtube kuna jamaa anaitwa "eddie nassor" ana library nzima ya RTD, mwimbo wowote anakuwekea , kie kie kie
 
Huo wimbo unaitwa Hanifa.
 
WOOOOOOTEE MME TAJA BENDI NYINGI LAKINI KIBOKO YA BENDI ZOTE ni moja tuu , WAZEE WA KAZI , TABORA JAZZY!!!!!, nani anabisha????????
Acha kabisa segere matata segua segua, iko vile bwana.
 
vifo vingi hutokea kwa kukosa misaada na kutomudu gharama za matibabu....................DDC MLIMAN PARK
 
Wanaofahamu naomba wanijuze kuna wimbo wa vijana jazz unaitwa Stella ni Stella yupi aliyeimbwa maana Hamza Kalala na Hemed Maneti wote wamezaa na wanawake tofauti wenye jina hilo.
 
Wanaofahamu naomba wanijuze kuna wimbo wa vijana jazz unaitwa Stella ni Stella yupi aliyeimbwa maana Hamza Kalala na Hemed Maneti wote wamezaa na wanawake tofauti wenye jina hilo.
Habari yako Chifu...

Ameimbwa Stella Cheyo, binti wa Mzee Mapesa John Cheyo ambaye sasa ni mke wa Komando Hamza Kalala....

Wimbo ni utunzi wa Komando Hamza Kalala na uliimbwa na Vijana Jazz chini ya Hemed Maneti Ulaya (R.I.P)...

Stella - Vijana Jazz

Sio kwamba ninakusifia eti kwa sababu wewe ni wangu, Stella eeeh,
Sio kwamba ninakusifia eti kwa sababu wewe ni wangu, Stella eeeh,
Miezi mitatu ya majaribio tumebaki tunaulizana ndugu kwa ndugu, mtoto wa Kisukuma ulivyolelewa,
Hata jirani zangu dirishani nimewasikia wakikusfu kwa ukarimu, Stella eeeh,
Kutokana na uwezo mwingi walionao wazazi wako wengi wao huwa wangeringa....

Hata jirani zangu dirishani nimewasikia wakikusfu kwa ukarimu, Stella eeeh,
Kutokana na uwezo mwingi walionao wazazi wako wengi wao huwa wangeringa....

Sio kwamba ninakusifia eti kwa sababu ya sura nzuri, Stella eeeh,
Miezi mitatu ya majaribio Kalala nabaki mi najiuliza hata Msai nitamueleza siku nitakayofika Mwanza,
Miezi mitatu ya majaribio hata mama yangu amekusifia hata Ilemela nitawaeleza siku nitakayofika huko,
Stella eeh, eeeh, Stella eeh, eeeh, Mwadilaa, Stella eeh, eeeh....

Sio kwamba ninakusifia eti kwa sababu ya sura nzuri, Stella eeeh,
Miezi mitatu ya majaribio Kalala nabaki mi najiuliza hata Msai nitamueleza siku nitakayofika Mwanza,
Miezi mitatu ya majaribio hata mama yangu amekusifia hata Ilamela nitawaeleza siku nitakayofika huko,
Stella eeh, eeeh, Stella eeh, eeeh, Mwadilaa, Stella eeh, eeeh....

Nikupe nini ee, nikupe nini ee, nikupe nini ee mayo wee,
Nikupe nini ee nasema cha kukupa sina iliyobaki mimi na wewe tu tuoanee...

Nikupe nini ee, nikupe nini ee, nikupe nini ee mayo wee,
Nikupe nini ee nasema cha kukupa sina iliyobaki mimi na wewe tu tuoanee...

Iliyobaki mimi na wewe tu tuoanee....
Iliyobaki mimi na wewe tu tuoanee....
Iliyobaki mimi na wewe tu tuoanee....
 
Mimi mzima sana mwanajangwani mwenzangu.

Nashukuru sana kwa kunijuza na kisha kuniwekea vionjo halisi, kwa kweli huu wimbo naupenda sana japo ni miongoni mwa nyimbo ngumu sana kuziiga uimbaji kwa jinsi mpangilio wake wa maneno ulivyo. Kuna wimbo umeimbwa na UDA jazz kwa lugha ya kimwera unaitwa 'Tulele tubone' sina uhakika kama nimetamka sawa naupenda mno lkn sijui maana ya ujumbe wake kama unaufahamu mwaga hapa pia kuna wimbo wa Dar International 'Siwema part 2' maarufu kama 'Sadiki' naomba mashahiri yake kama unao.
 
Asante mdau, kila nikisikia wimbo huu namkumbuka kipenzi changu Frank.
Tuliachana jioni, asubuhi akasafiri, njiani akapata ajali na kufariki dunia.
Huwa nikienda live band lazima niombe huu wimbo, huwa nausikiliza kwa hisia kali sana.
Asante Balantanda.....umenikumbusha mbali sanaaa.
Ohhhhh.....Frank, safari kwako imekuwa ni kifo.
Sijui lini utarudi....dahhh!!!!!, mdau, unaniliza ujue.
 
Last edited by a moderator:
ndugu nyimbo zote nimezikubali mno, PIA nia shida na nyimbo ya salum abdallah aliyoimba na cuban malimba band iitwayo "mkono wa eidd"
 
Idd Mubarak!
Daa! Nilikuwa sijafuatilia kona hii kwa umakini kama leo!
Mimi kuna wimbo wa MK GROUP ni kitendawili kwangu kama jina lake lilivyo! Unaitwa KITENDAWILI. Nafikiri ni akili ya hali ya juu ilitumika.
Hebu nipe shule!! Ni ushirikina kweli?
Nikitembea nasikia mwanangu ananiita
niligeuka hamijibu jamani, walimwengu siyo wemaa!
Yoo mama yo
 
jamani, huku ndani kuna audio ya hiba - bitchuka? maana nimeangalia sana sijaona
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…