Ogopa Tapeli
Penzi la Ulaghai
Kapu la Mjanja
Julie
1. Ogopa Tapeli-Watu hao wameeneaaa sanaa kila pembe hapa nchiniii kazi yao kuibia watu jina lao matapeliii. Huibia watu mashamba magari pesa hizo zoteee ni za bandia jina lao ni tapeli(Eddie SHEGGIE-RIP)
2.Penzi la ulaghai-Ama kweli kizurii hakikosi kasoroo jama eee kwa muda mfupi niliyoishi nae, nilimpenda sana lakini mwenzangu penzi lake likawa la ulaghai eee la Ulagahaii.
Nimekanyaga motoo, yamenikuta kijana mwenzenu nifanye nini.
Hata wazazi wangu kweli walimpenda sana lakini mwenyewe kajiharibiaaa, tabia ya mchumba wangu ingefanana na urembo wake kweli angefanikiwaaa, siku ya kuondoka kwake alisomba kila kitu ndani ya nyumba nikabaki sina kitu(Eddie SHEGGIE-RIP)
3.Kapu la Mjanja-Ndege wa rangi moja ee huruka pamoja eee, uliona wapi Bundi kwenye kundi la njiwaaa eeeee kaka eee kaka eeee
Eddie Sheggie-Dunia haina siri mwenyewe watambua aa kaka eee kaka ee, sasa utalala wapi ee kaka ee kaa eeew, leo utakula nini kaka eeee kakaa eeeee eeee aiiibuuuuu.
Chorus all(Vijana jazz)- Ona sasa huna pa kula na kulala umekua kama bundi ukioneka mkosi wabaki wawaya waya ee dunia haina siri elewa kapu la mjanja mjinga hatii mkono, umebaki wawaya wawaya maji yameshamwagika.
Eddie Sheggie-Shetani kamwingia..........
Daaa!
hatari sana Vijana Jazz imekufa, siamini macho yangu ladha.
4.Julie(Washirika Tanzania Stars/Eddie Sheggie)
Julieee eee eeee nikupe nini uridhikeee cha kukupa sinaa mamaaaa eeee*3
Ufukara nilio nao oooo mamaaa maaaa, ufukara umekua kashfa ya mapenzi yanguuu kwako kwakooooo ingawa................
Wadau, huo ndiyo ulikua muziki hasa ulioitambulisha Tanzania. Nikikumbuka vibao kama NAOMI cha DDC Mlimani Park, Busu Pande Tatu wa Bimalee, Baba Jane 1&2 wa Bantu Group, Makulata n.k nasikia Uchungu kuwa mambo hayo yamebaki historia na hata redio nyingi hawapigi kabisa,either kwa kuwa hata watangazaji wake wengi walikua watoto enzi hizo au hawapendi tu. Kwa hakika natafuta CD collection ya nyimbo zote za hayati EDDIE SHEGGIE!