Wewe pia ni mhanga-hujui utendalo. Ndo maana mimi nimetoa elimu, sijakulaumu. Nitajibu hoja zako kama ifuatavyo:
- Sheria ya Hakimiliki ipo na inasimamiwa kwa kiasi cha kuridhisha na BASATA. Mfano mzuri ni Mwinjuma Muumini ambaye ktk mahojiano fulani miaka kama 3 iliyopita alikiri kupokea kama laki 5 kila baada ya miezi 3 kutoka kwa wasambazaji wa kazi zake. Wasambazaji wanamlipa kwa sababu kuna watu wananunua kazi za wasanii-kumbuka Muumini ana miaka kadhaa hajarekodi nyimbo mpya. Wewe ukitoa bure, nani atanunua? BASATA wapo, na kama hawajakushughulikia basi shukuru Mungu.
- Kuhusu nyimbo kuwepo kwenye servers, hii hoja ni sawa na kujitetea kuwa wewe umeiba kwa sababu John na Halima pia wameiba. Ikifika wakati wa kuwajibishwa unawajibishwa wewe kama wewe. Huo utetezi ni butu. Nikiri kuwa kua pirated works nyingi sana mtandaoni, ulaya wanadhibitiwa kwa kuzifunga tovuti hizo ndo maana wanalazimika kubadilisha domain name kila mara. Hata wewe nikiwasiliana na host wako nikiwa kama mrithi wa kazi (mfano) za Mbaraka Mwinshehe, atalazimika kuifunga tovuti yako au atalazimika kulipa gharama za 'wizi' unaofanyika.
Mwisho nikushauri kwamba hapa tunaelimishana tu ili watoto wetu waje kuthamini kazi za sanaa na kufaidika nazo maana ni fursa kubwa sana za ajira. Itapendeza tukifika mahali tukalinda kazi za wasanii wetu na wa nje kama wanavyofanya Kenya na Nigeria ambako wanamuziki wanalipwa kwa kazi zao kupigwa ktk TV na redio. Leo Diamond anaenda Kenya kuchukua hela yake kwa sababu serikali ya Kenya inajitahidi kulinda kazi za wasanii.