ZILIPENDWA: Wanamuziki, nyimbo na mitindo yao

ZILIPENDWA: Wanamuziki, nyimbo na mitindo yao

0766728326. WhatsApp mkuu
Mkuu wangu wimbo, nimeungalia kwenye memory card, sijauona, nadhani upo kwenye frash, nitautoa kwenye frash, niuweke kwenye memory card ili nikurushie.
 
Wewe pia ni mhanga-hujui utendalo. Ndo maana mimi nimetoa elimu, sijakulaumu. Nitajibu hoja zako kama ifuatavyo:
  1. Sheria ya Hakimiliki ipo na inasimamiwa kwa kiasi cha kuridhisha na BASATA. Mfano mzuri ni Mwinjuma Muumini ambaye ktk mahojiano fulani miaka kama 3 iliyopita alikiri kupokea kama laki 5 kila baada ya miezi 3 kutoka kwa wasambazaji wa kazi zake. Wasambazaji wanamlipa kwa sababu kuna watu wananunua kazi za wasanii-kumbuka Muumini ana miaka kadhaa hajarekodi nyimbo mpya. Wewe ukitoa bure, nani atanunua? BASATA wapo, na kama hawajakushughulikia basi shukuru Mungu.
  2. Kuhusu nyimbo kuwepo kwenye servers, hii hoja ni sawa na kujitetea kuwa wewe umeiba kwa sababu John na Halima pia wameiba. Ikifika wakati wa kuwajibishwa unawajibishwa wewe kama wewe. Huo utetezi ni butu. Nikiri kuwa kua pirated works nyingi sana mtandaoni, ulaya wanadhibitiwa kwa kuzifunga tovuti hizo ndo maana wanalazimika kubadilisha domain name kila mara. Hata wewe nikiwasiliana na host wako nikiwa kama mrithi wa kazi (mfano) za Mbaraka Mwinshehe, atalazimika kuifunga tovuti yako au atalazimika kulipa gharama za 'wizi' unaofanyika.
Mwisho nikushauri kwamba hapa tunaelimishana tu ili watoto wetu waje kuthamini kazi za sanaa na kufaidika nazo maana ni fursa kubwa sana za ajira. Itapendeza tukifika mahali tukalinda kazi za wasanii wetu na wa nje kama wanavyofanya Kenya na Nigeria ambako wanamuziki wanalipwa kwa kazi zao kupigwa ktk TV na redio. Leo Diamond anaenda Kenya kuchukua hela yake kwa sababu serikali ya Kenya inajitahidi kulinda kazi za wasanii.
duh! Tunatishana
 
Mimi mkuu natafuta nyimbo mbili tu..
1. Penzi kikohozi yake Fresh Jumbe.

2. Hii ni taarab sijaijua jina, ila mashairi yake yanaimbwa hivi, "Yailahi shoga si shoga, Kumbe ni hasidi eeh
Nalia shoga si shoga, kumbe ni hasidi"
Kama nitazipata hizi mkuu, utakuwa umenisaidia sana.
 
Mimi mkuu natafuta nyimbo mbili tu..
1. Penzi kikohozi yake Fresh Jumbe.

2. Hii ni taarab sijaijua jina, ila mashairi yake yanaimbwa hivi, "Yailahi shoga si shoga, Kumbe ni hasidi eeh
Nalia shoga si shoga, kumbe ni hasidi"
Kama nitazipata hizi mkuu, utakuwa umenisaidia sana.
Penzi ni kikohozi ya fresh Jumbe ipo humu, ameiweka labda hiyo ya taarabu.
 
Naomba wimbo wa soul n faith maumivu ya mapenzi
 
Hello wazee wa zilipendwa na muziki wa dansi.
Naweza kujua SIKINDE NGOMA YA UKAE watakuwa ukumbi gani siku ya Idd.?
Ukiweza nipe ratiba ya bend za muziki wa dansi siku ya Idd Mosi!

Mimi ni mnazi wa Nginde ngoma kubwa!
 
WIMBO WA BANZA STONE
UNAIMBWA HIVI

"MWENYE KWENU KWAHERI OOOH!! '
 
Pumzika kwa Amani Shaban Dede...

Mbele yako nyuma yetu...
 
Katika kumkumbuka Shaban Dede aliyefariki leo..Tujikumbushe nyimbo zake hizi zilizotamba

 
Hayati Shaban Dede amewahi kutamba na bendi kubwa za Bima Lee Orchestra (Magnet Tingisha) ,DDC Mlimani Park (Sikinde Ngoma ya ukae) na Msondi Ngoma Music Band
 
Nikuombe tafadhali, katika kumkumbuka marehemu Shabaan Dede tafadhali ungetuwekea hapa list ya nyimbo zake kadhaa zilizotamba katika hizo bendi alizopitia
 
Back
Top Bottom