ZILIPENDWA: Wanamuziki, nyimbo na mitindo yao

Hiyo band ilikuwa inaitwa Tancut Almasi ikiwa inamulikiwa na kiwanda cha kukata Alimasi kilichokuwa Iringa.
Asante sana mkuu kwa ufafanuzi wako, Mungu akubariki sana wewe na kizazi chako.
 
wadau nautafuta wimbo unaimbwa hivi
watoto wamekuja juu ,wanadai nyumba yao
 
wadau nautafuta wimbo unaimbwa hivi
watoto wamekuja juu ,wanadai nyumba yao
Kila nilifanyalooo wao haliwapendezi na Wala hawakumbuki usia wa baba yaooo,
Marehemu aliusia ooooh wasinituptupe Wala wasinyanyase babaaaa ooooh mamaaaa!
Wengi wamenishauri eti nirudi nyumbani Sina baba Wala mama huko niende kwa naniiii
[emoji2400]Ni washirika band/Vijana jazz/Hamza kalala Sina hakika.
 
Kuna huu wimbo wa mama Jane. Unaimbwa "mama jane mke wangu kwaheri mama, mungu akulaze mahala pema peponi" . Wimbo huu ni wa kitambo sana ila sifahamu ni nani alieimba. Mwenye kuwa na wimbo huu tafadhali naomb uniwekee hapa nauhitaji sana.
 
Hapa tuko pamoja sana mkuu.....Sikinde daima(damu damu).....

Pia zamani nilikuwa mnazi wa Vijana Jazz wana Pambamoto kabla haijaanza kupotea na kufifia kabisa....

Kuna wimbo unasema…

Mimi na wee na wee na wee
Tumeamua tusiachane mpaka kufa
Mimi nasema nawe wasema twaelewana
Tusipate machonganisho ya pembeni
Tuwe na umoja pia na raha vyote sawa…

Tumefika Moroo, kwa Mbaraka Mwishehe, Moro kwa Salum Abdallah…

Ebana huu wimbo unaitwaje?!
 

Balantanda nakuita tena Mkuu sambamba na Wakuu wengine mnaoweza nisaidia kuupata
 
kuna wimbo nautafuta sikumbuki kama waliimba vijana Jazz au bendi gani, kibwagizo chake kilikuwa hivi "enyi wote wake zangu mapenzi yangu kwenu ni sawa mpendane ndio heshima ya ndoa ee"
Dah umelenga mle mle.
 
Skärholmstorg Stokholms tour 2022
Sweden

DEKULA BAND : Song: Zinduna

Mtindo wa Sendema ya Moto ndani ya Sweden


Dekula Band Soukous Music: Song: Zinduna by Gaby K. Nkomba (live) Pakteatern skärholmstorg Stockholm Sweden 30/06/2022 Musicians:
  • Guitar/singer: Kahanga Dekula (Vumbi)
  • Guitar: Göran Larsson
  • Bass: Joseph Semafumu
  • Drums: Michigan Ngoy
  • Sax: Henrik Westerberg
  • Singer: Gaby Kababa Nkomba
  • Cameraman: Arwa Mzee Kobe Brayo
  • Quality images courtesy of Arwa-iCTv
Source : Dekula2 Band (official)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…