ZILIPENDWA: Wanamuziki, nyimbo na mitindo yao

ZILIPENDWA: Wanamuziki, nyimbo na mitindo yao

Mkuu, hizi nyimbo mbili ulizozitaja ni za Vijana Jazz - Pambo Moto chini ya Marehemu Hemed Maneti enzi hizo. Wa kwanza ulioutaja (Bwana Mwangusi) unaitwa 'Ogopa Matapeli," yule mwenye sauti tamu ya hajabu aliye imba huu wimbo ni Eddy Sheggy (R.I.P.) Huo wimbo wa pili (hunijali kwa chumvi) unaitwa "Penzi Haligawanyiki, Pt. I' uliimbwa na Chiriku Maneti na mkewe Kida Waziri. Baada ya kusikiliza hii dozi ya Vijana, niambie kwa akili yako....unaweza kweli kulinganisha na bongo fleva huu muziki wetu wa dansi? Muziki wa dansi ni kiboko ya mabishololo wa muziki.
Asante, kwa kweli kama ni mbio za kutoka dar kwenda mwanza leo asubuhi, muziki huu wa dansi wa zamani uko shinyanga bongo fleva pumzi imekata ndo wanaitafuta mlandizi!
je na hii inaitwaje kama hautomaindi;
....kuna gari limekuja hadi mlangoni kumuuliza akasema mjomba wake kaja..... Shikamoo ikaisha ikabaki vipi babu mambo zako eeee eeee...!
Nautafuta na huu ila sijajua title wala waliouimba ni kina nani.
Nyimbo za juu hapo zote nimezipata, alafu kuna wimbo mmoja wa Komando Hamza kalala Wa nimekusamehe lakini sitokusahauu alalala lalala laaa...
Niliusikiliza nikafurahi sana, kuna mtu kanikosea nimemtumia dedication, ni kijana mwenzangu tu ila kausikiliza ukamkolea juzi kaja kuniomba samahani hadi kupiga magoti!
oldies are timeless!
 
Hongera sana ila sasa una maktaba ndogo sana. Kuna nyimbo nyingi ambazo watu tunazo wewe huna.
 
  • Thanks
Reactions: OTG
Hongera sana ila sasa una maktaba ndogo sana. Kuna nyimbo nyingi ambazo watu tunazo wewe huna.
Mkuu kusema Kweli nina Collection Kubwa mno ila Muda wakuzipakia nakosa ndio maana najitahidi kupakia angalao Tano kwa siku. Usjali Shughuli zikiniisha Nitazijaza Kule.
 
Mkuu mimi ni mpenzi sana wa nyimbo za akina double M sound, mchinga sound, tam tam nk. Kama kuna uwezekano tupia izo mambo mkuu
 
Mkuu mimi ni mpenzi sana wa nyimbo za akina double M sound, mchinga sound, tam tam nk. Kama kuna uwezekano tupia izo mambo mkuu
Mbona Tam Tam Ipo mkuu icheki utaipata kule na Hizi nyingine Nitaziweka mkuu usjali
 
Asante, kwa kweli kama ni mbio za kutoka dar kwenda mwanza leo asubuhi, muziki huu wa dansi wa zamani uko shinyanga bongo fleva pumzi imekata ndo wanaitafuta mlandizi!
je na hii inaitwaje kama hautomaindi;
....kuna gari limekuja hadi mlangoni kumuuliza akasema mjomba wake kaja..... Shikamoo ikaisha ikabaki vipi babu mambo zako eeee eeee...!
Nautafuta na huu ila sijajua title wala waliouimba ni kina nani.
Nyimbo za juu hapo zote nimezipata, alafu kuna wimbo mmoja wa Komando Hamza kalala Wa nimekusamehe lakini sitokusahauu alalala lalala laaa...
Niliusikiliza nikafurahi sana, kuna mtu kanikosea nimemtumia dedication, ni kijana mwenzangu tu ila kausikiliza ukamkolea juzi kaja kuniomba samahani hadi kupiga magoti!
oldies are timeless!

Sawa.....ni hivi. Huu wimbo wa 'Shikamoo ikaisha...." ni Wimbo wa Super Rainbow chini ya Eddy Sheggy. Wimbo unaitwa "Milima Ya Kwetu, Part I. Huo wa Komando unaitwa: "Nimekusamehe," Au "Yaliyopita Si Ndwele." Waliufanyanyia remix na kulipa jina tofauti.
 
Jamani mimi kijana mwenzenu wa enzi hizo, nashindwa kudownload hizi nyimbo. Nikibofya ile sehemu ya *Download now* nyimbo inaplay badala ya kudownload.
Naombeni maelekezo wazee wenzangu
 
Salama wakuu?,ni jumapili nyingine tulivu....

Leo naomba tujikumbushe bendi zetu zilizotamba sana miaka ya 80 na 90,bendi ambazo ama zimekufa ama zinaendelea kusuasua na ambazo ukisikiliza muziki wake leo hii unatamani ungerudisha wakati nyuma.......

Kwa kuanzia tuanze na hawa Orchestra Vijana Jazz,bendi ambayo ilikuwa ikimilikiwa na Umoja wa vijana wa CCM,bendi hii ilikuwa ikitumia mitindo ya Sindimba,Hekaheka,Heka koka,Watoto wa nyumbani,Air Pambamoto(awamu ya kwanza na ya pili) na baadae mtindo wa Saga Rhumba.....

Kwangu mimi bendi hii ndiyo ilikuwa chaguo langu hasa......Ukitaka kuujua ukali wa bendi hii sikiliza nyimbo kama Chiku,Mary Maria,Penzi lamea penye penzi,Shemeji,Bujumbura,Ilikuwa lifti,Tambiko la Pambamoto,Adza(Aza),Ngapulila,Ogopa Tapeli,Mwisho wa Mwezi,Penzi haligawanyiki,Wivu,Malaine,Nyongise,Shoga,Theresa,V.I.P,Mama Chichi na nyingine nyingi tu tamu....

Bendi hii imewahi kuundwa na wanamuziki kama Hemed Maneti 'Chiriku',Hamza Kalala 'Komando',Manitu Mussa,Issa Chikupele,Hassan Dalali,Hassan Shaw,Ally Jamwaka,Abuu Semhando,Bakari 'Baker' Semhando,Mhina Panduka 'Toto Tundu',Adam Bakari 'Sauti ya zege',Eddy Sheggy,Shaban Yohana 'Wanted',Rashid Pembe 'Profesa',Kida Waziri,Beno Villa Anthony,Rahma Shally,Jerry Nashon 'Dudumizi',Suleiman Mbwembwe,Shaban Dogodogo,Aggrey Ndumbalo,John Kitime,Abdallah Mgonahazelu,Freddy Benjamin,Mohammed Gotagota,Said Hamis 'Misukosuko',Athumani Momba na wengine kibao...
mkuu niwekee milima ya kwetu 1 na 2 kama ipo tafadhari
 
Jamani mimi kijana mwenzenu wa enzi hizo, nashindwa kudownload hizi nyimbo. Nikibofya ile sehemu ya *Download now* nyimbo inaplay badala ya kudownload.
Naombeni maelekezo wazee wenzangu
No inashusha Mkuu
 
TAFADHALINI SANA WANA JAMII FORUM NAOMBA MWENYE NYIMBO YA "BABA PAROKO" By JUNIOR MAKASI ANIPATIE AU AWEKE UKU NIDOWNLOAD
 
Back
Top Bottom