barafuyamoto
JF-Expert Member
- Jul 26, 2014
- 32,378
- 29,739
Asante, kwa kweli kama ni mbio za kutoka dar kwenda mwanza leo asubuhi, muziki huu wa dansi wa zamani uko shinyanga bongo fleva pumzi imekata ndo wanaitafuta mlandizi!Mkuu, hizi nyimbo mbili ulizozitaja ni za Vijana Jazz - Pambo Moto chini ya Marehemu Hemed Maneti enzi hizo. Wa kwanza ulioutaja (Bwana Mwangusi) unaitwa 'Ogopa Matapeli," yule mwenye sauti tamu ya hajabu aliye imba huu wimbo ni Eddy Sheggy (R.I.P.) Huo wimbo wa pili (hunijali kwa chumvi) unaitwa "Penzi Haligawanyiki, Pt. I' uliimbwa na Chiriku Maneti na mkewe Kida Waziri. Baada ya kusikiliza hii dozi ya Vijana, niambie kwa akili yako....unaweza kweli kulinganisha na bongo fleva huu muziki wetu wa dansi? Muziki wa dansi ni kiboko ya mabishololo wa muziki.
je na hii inaitwaje kama hautomaindi;
....kuna gari limekuja hadi mlangoni kumuuliza akasema mjomba wake kaja..... Shikamoo ikaisha ikabaki vipi babu mambo zako eeee eeee...!
Nautafuta na huu ila sijajua title wala waliouimba ni kina nani.
Nyimbo za juu hapo zote nimezipata, alafu kuna wimbo mmoja wa Komando Hamza kalala Wa nimekusamehe lakini sitokusahauu alalala lalala laaa...
Niliusikiliza nikafurahi sana, kuna mtu kanikosea nimemtumia dedication, ni kijana mwenzangu tu ila kausikiliza ukamkolea juzi kaja kuniomba samahani hadi kupiga magoti!
oldies are timeless!