ZILIPENDWA: Wanamuziki, nyimbo na mitindo yao

ZILIPENDWA: Wanamuziki, nyimbo na mitindo yao

Asnte sana mkuu Alichachi, hizi nyimbo za bicko star, naikumbuka sana nyimbo ya Tabu, walimwengu wamenigeuza kama shina la muhogo, huliwa majani, huliwa mizizi yake, na unatupwa jalalani na unaota tena. Kama huu mkuu tupia tafadhari.
 
Kwakweli hili ni jukwaa zuri, la kupeana vitu vilivyoadimika masikioni mwa wengi, hasa kwa kizazi cha miaka 40 hadi 55 hizi nyimbo ni tamu sana, siku zote ninapozihitaji hizi naenda pale Temeke Stireo, jamaa anazo nyingi mno.
 
Mi natumia simu mkuu
Mfano huyo wimbo wa mzee Mwinamila, na bicko star, nenda gonga kwenye alama ya Download kuna rangi ya blue, itaserch alafu yatatokea maandishi ya seve na censel chagua seve, iache rudi jamii itafute kingine unachota kukiona. Hapa unaweza pakia nyimbo unazo taka zikaendelea zenyewe wewe unafanya shuhuri zingine.
 
Acha z

Acha hizo wewe, ungeanza na wale wanauza nyimbo kwenye computer, hapa sisi tunapeana kama wanafamilia tu, asie mwana forums anapataje nyimbo hizi.
Mimi nimetoa tu angalizo na elimu. Leo ni wanamuziki wanaumia kesho itakuwa wewe na kitabu chako au ndugu yako na software/App yake. Tusaidiane kutoa elimu kwa hao wanaouza nyimbo kwenye computer-wengi wao hawajui kama wanafanya makosa, kama wewe tu.
 
Mimi nimetoa tu angalizo na elimu. Leo ni wanamuziki wanaumia kesho itakuwa wewe na kitabu chako au ndugu yako na software/App yake. Tusaidiane kutoa elimu kwa hao wanaouza nyimbo kwenye computer-wengi wao hawajui kama wanafanya makosa, kama wewe tu.
Nimekuelewa ndugu yangu, hivi hao wanamziki wanaoumia sisi kurushiana nyimbo, je wameandaa mazingira rafiki ya sisi kununua nyimbo tunazozihitaji, hususani hizi za zamani. Maana tusiwe tunanyima sisi, lakini wengine wakirushiana kwa njia hizi hizi unazozipinga.
 
Nimekuelewa ndugu yangu, hivi hao wanamziki wanaoumia sisi kurushiana nyimbo, je wameandaa mazingira rafiki ya sisi kununua nyimbo tunazozihitaji, hususani hizi za zamani. Maana tusiwe tunanyima sisi, lakini wengine wakirushiana kwa njia hizi hizi unazozipinga.
Nadhan hata wao wanakosa uelewa wa haki zao hasa wanamuziki wa zamani na warithi wao (maana wengi wametangulia mbele ya haki). Kazi ya msanii inalindwa na sheria ya hakimiliki hadi miaka 50 baada ya kifo cha msanii au msanii wa mwisho kufa kama kazi ilifanywa na kundi/bendi. Hiki kitu sio wengi wanakifahamu.

Wanamuziki wanapaswa kusaidiwa na serikali kupitia vyombo vya dola (polisi, mahakama) na wizara ya utamaduni na michezo ili kuweza kutokomeza uharamia wa kazi za kisanii. Pia wasambazaji wana jukumu la kulinda kazi za wasanii maana na wao wanafaidika kupitia wasanii. Mfano mzuri ni bongo movie, mhindi aliyekuwa anamkandamiza msanii anapata faida gan sasa ambapo soko la filamu limefifia?

Mwisho jamii pia inapaswa kuunga mkono juhudi za kulinda kazi za kisanii. Hakuna familia isiyokuwa na msanii, hivyo kuna fursa kubwa sana ya kujiajiri na kubadili maisha ya familia kupitia sanaa. Lazima tuhakikishe wasanii wanafaidika.
 
Mkuu weka nyimbo ya Monisandesa hapa, unaitwa shida haibishi hodi, wimbo wa vijana, mama ninapokula anisema, na wanaupendana siku zote hufa wangali vijana (Chiku). Kuna wimbo wa Banza Stone, siujui jina ila kuna sehemu anaimba: siku ya kufa kwake atamuomba Mungu apate kuwasikia watu wanasema nini kuhusu kifo chake. wimbo kiyongo band siikumbuki.
Usijali Mkuu tatizo Muda, nkipata Muda ntazipandisha
 
Kwanza Mkuu hakuna hicho kitu kinachoitwa HAKIMILIKI hapa bongo maana ingekuwepo mpaka leo Hawa wazee wangekua na Maisha mazuri mno, na Kingine ni kwamba nyimbo hizi zipo kwenye servers tofauti tofauti huku mitandaoni hivyo mimi nimefanya kuzikusanya pamoja ili kurahisisha mambo. Je Mdundo.com ni nani kawapa Ruhusa yakusambaza hizi ngoma za kale????

Wewe pia ni mhanga-hujui utendalo. Ndo maana mimi nimetoa elimu, sijakulaumu. Nitajibu hoja zako kama ifuatavyo:
  1. Sheria ya Hakimiliki ipo na inasimamiwa kwa kiasi cha kuridhisha na BASATA. Mfano mzuri ni Mwinjuma Muumini ambaye ktk mahojiano fulani miaka kama 3 iliyopita alikiri kupokea kama laki 5 kila baada ya miezi 3 kutoka kwa wasambazaji wa kazi zake. Wasambazaji wanamlipa kwa sababu kuna watu wananunua kazi za wasanii-kumbuka Muumini ana miaka kadhaa hajarekodi nyimbo mpya. Wewe ukitoa bure, nani atanunua? BASATA wapo, na kama hawajakushughulikia basi shukuru Mungu.
  2. Kuhusu nyimbo kuwepo kwenye servers, hii hoja ni sawa na kujitetea kuwa wewe umeiba kwa sababu John na Halima pia wameiba. Ikifika wakati wa kuwajibishwa unawajibishwa wewe kama wewe. Huo utetezi ni butu. Nikiri kuwa kua pirated works nyingi sana mtandaoni, ulaya wanadhibitiwa kwa kuzifunga tovuti hizo ndo maana wanalazimika kubadilisha domain name kila mara. Hata wewe nikiwasiliana na host wako nikiwa kama mrithi wa kazi (mfano) za Mbaraka Mwinshehe, atalazimika kuifunga tovuti yako au atalazimika kulipa gharama za 'wizi' unaofanyika.
Mwisho nikushauri kwamba hapa tunaelimishana tu ili watoto wetu waje kuthamini kazi za sanaa na kufaidika nazo maana ni fursa kubwa sana za ajira. Itapendeza tukifika mahali tukalinda kazi za wasanii wetu na wa nje kama wanavyofanya Kenya na Nigeria ambako wanamuziki wanalipwa kwa kazi zao kupigwa ktk TV na redio. Leo Diamond anaenda Kenya kuchukua hela yake kwa sababu serikali ya Kenya inajitahidi kulinda kazi za wasanii.
 
Back
Top Bottom