ZILIPENDWA: Wanamuziki, nyimbo na mitindo yao

ZILIPENDWA: Wanamuziki, nyimbo na mitindo yao

TehTeh....Ngoja nizichangamkie buku 40 aisee....Naziangalia kunako kalibrary kangu mkuu...Nikizipata nitaziweka hapa ASAP....

Haha kaka I'm serious, sasa hvi 50,000. Kazi kwako.

Sent from my iPad using Tapatalk HD
 
kaka kuna viba vya zamani 2 navitafuta kwa udi na uvumba, nio tayari utoa 40,000tsh kwa yeyote ataenitaftia.
1. kivumbi kimenizonga (ioss ya Ndala kasheba) na tucheze sote tukunyema ( Mk beats ya shem karenga)

Oya Barantanda amekupatia hizo nyimbo?
Na je ubani uko kweli?
 
Naam kaka, ubani upo bila Shaka , zikowapi?????

Sent from my NOKIA 3310 using Tapatalk HD
 
Kaka Balantanda umepotea kabisa/Unakikumbuka kisa cha kweli cha nyimbo hizi?1) Homa imenizidia (OSS-Bitchuka)2) Mtoto akililia wembe (DDC-Chidumule)3) Nimekubali maneno -Mwana Kaza moyo (DDC)
 
Kaka Balantanda umepotea kabisa/Unakikumbuka kisa cha kweli cha nyimbo hizi?1) Homa imenizidia (OSS-Bitchuka)2) Mtoto akililia wembe (DDC-Chidumule)3) Nimekubali maneno -Mwana Kaza moyo (DDC)

Nyimbo zenyewe hizi hapa.....Hebu tueleze kisa cha nyimbo hizi mkuu wangu...

Last edited by a moderator:
Kaka Balantanda umepotea kabisa/Unakikumbuka kisa cha kweli cha nyimbo hizi?1) Homa imenizidia (OSS-Bitchuka)2) Mtoto akililia wembe (DDC-Chidumule)3) Nimekubali maneno -Mwana Kaza moyo (DDC)

Umesahau na fordi( OSS- Bitchuka)

Sent from my NOKIA 3310 using Tapatalk HD
 
Mkuu Balantanda,Homa imenizidia ni wimbo alioimba Bitchuka akiwa OSS, na kisa hasa ni kuwa wakati Hugo Kisima anawachukua kutoka Nginde (Bitchuka, Ngurumo,Bartazar nk) aliwaahidi kuwapa fedha, nyumba, gari na vitu vingine na ndio kisa cha kutimukia humo huku wakimwacha Chidumule kama ndio mwimbaji kiongozi Ngindesasa walipofika kule wakakuta yale yote waliyoahidiwa hakuana hata moja ni la kweli, hivyo Bitchuka ndio akaingia hewani kutoa hicho kibao, sasa angalia zamani watu walivyokuwa wanapanga mashairi, yaani huwezi kujua kabisa story hasa ni niniHoma imenizidia mie............kisa alichonitenda rehani (HUGO)...alinishawishi nimuaache mume wangu (DDC) ili niishi nae (OSS)nikaachana na mume wangu (DDC), nikaenda kwa rehani (OSS)..Mama yamenikuta..ndugu zangu mlioolewa.....sasa baada ya Bitchuka kutoka hivyo, Mzee mzima Chidumule akaingia hewani na mtoto akililia wembeMtoto (Bitchuka, ngurumo nk) akililia wembe wacha Umkate...dada (Bitchuka) yetu ee we ulishaolewa (na DDC), lakini kwa tamaa yako ulikubali kumwacha mumeo (DDC) ....... na kwenda kwa bwana mwenye pesa (HUGO/OSS)......atakununulia gari, atakujengea nyumba....sasa unajuta(BITCHUKA NA HOMA IMENIZIDIA) Usilie unalia nini......na wewe ulisema umempata bwana (HUGO/OSS)sisi tulia nyumba hiyo ni chambo tu......hiyo miziki sio mchezo BAlantanda inaelezea visa vya kweli kabisa
 
Mkuu Balantanda,Homa imenizidia ni wimbo alioimba Bitchuka akiwa OSS, na kisa hasa ni kuwa wakati Hugo Kisima anawachukua kutoka Nginde (Bitchuka, Ngurumo,Bartazar nk) aliwaahidi kuwapa fedha, nyumba, gari na vitu vingine na ndio kisa cha kutimukia humo huku wakimwacha Chidumule kama ndio mwimbaji kiongozi akiwa na Bushoke Max Ngindesasa walipofika (Bitchuka na wenzie) kule wakakuta yale yote waliyoahidiwa hakuna hata moja ni la kweli, hivyo Bitchuka ndio akaingia hewani kutoa hicho kibao,sasa angalia zamani watu walivyokuwa wanapanga mashairi, yaani huwezi kujua kabisa story hasa ni niniHoma imenizidia mie (Bitchuka na wenzie)............kisa alichonitenda rehani (HUGO)...alinishawishi nimuaache mume wangu (DDC) ili niishi nae (OSS)nikaachana na mume wangu (DDC), nikaenda kwa rehani (OSS)..Mama yamenikuta..ndugu zangu mlioolewa.....sasa baada ya Bitchuka kutoka hivyo, Mzee mzima Chidumule akaingia hewani na mtoto akililia wembeMtoto (Bitchuka, ngurumo nk) akililia wembe wacha Umkate...dada (Bitchuka na wenzie) yetu ee we ulishaolewa (na DDC), lakini kwa tamaa yako ulikubali kumwacha mumeo (DDC) ....... na kwenda kwa bwana mwenye pesa (HUGO/OSS)......atakununulia gari, atakujengea nyumba....sasa unajuta(BITCHUKA NA HOMA IMENIZIDIA) Usilie unalia nini......na wewe ulisema umempata bwana (HUGO/OSS) sisi tulijua nyumba hiyo ni chambo tu......hiyo Chidumule na MAx Bushoke hawakuishia hapo, wakaja na Nimekubali maneno yangu.....kuwa uzuri wa mtu, sio sura ni tabia, Hapa chidumule na Max kwanza walichukua nafasi ya Bitchuka na wenzie kama analalamika kwa wazazi wake na kisha wakawa wazazi kumshauri binti yao (Bitchuka na wenzie)Nimekubali maneno yenu wazazi wangu.........Huyu mume (HUGO/OSS) niliyemkubali kanishinda hila, Hata kama mimi (DDC wakimwakilisha Bitchuka na wenzie) sio arudi.......Kwa hiyo wazazi wangu (DDC walimwakilisha dede na wenzie) tabia hiyo.....bora nirudi kwetu (DDC)sasa Chidumule na Max wakaingiaMwanetu (Bitchuka na wenzie) kaza moyo uishi na mumeo (HUGO/OSS), ..... ni wewe mwenyewe ulimpendamiziki sio mchezo BAlantanda inaelezea visa vya kweli kabisa
 
du nimeandika kwa para, lakini hapa imeunganisha kila kitu na kila niki edit inashindwa kusave
 
Nyimbo za zamani mistari yake imetulia, inabidi utumie miwani kuichambua maana yake asili. Shukran mdau

Sent from my NOKIA 3310 using Tapatalk HD
 
Salama wakuu.....Ni wikiendi nyingine baada ya muda mrefu wa kuwa kimya.....Leo nimewakumbuka TANCUT Almas Band, wana Fimbo Lugoda....Kinye kinye kisonzi,tisa kumi mangala...Musendemule......Mangala Dansi

tancut.jpg

Baba_na_nduguze8.jpg

Leo ngoja tujikumbushe na baadhi ya vibao vyao vilivyotamba enzi hizo,kwa kuanzia tuanze na kitu Jejee Lutandila

E wasaa.......

Ujumbe wangu kama umeupata Jejee,
ujumbe wangu kama umeupata fanya haraka Jejee,
Jejee Lutandila rudi nyumbani baba,
Nimetuma barua hata majibu wala sipati mamaa,
Sasa ni miaka kumi na mbili Jejee Lutandila aaa..

Jejee.......Lutandila...

Jejee Jejee Lutandila,mwanangu Jejee Jejee Lutandila,
Mimi mama yako sina wa kunitunza,baba yako amekwishafariki mama,
Ninayemtegemea kwa sasa ni wewe Jejee,ewawaa..

Jejee Jejee Lutandila,mwanangu Jejee Jejee Lutandila,
Mimi mama yako sina wa kunitunza,baba yako amekwishafariki mama,
Ninayemtegemea kwa sasa ni wewe Jejee,ewawaa..

Maisha magumu kila kitu ni pesa Jejee,nimekuwa na ukiwa kama vile sijazaa,
Nakuwa ombaomba na watoto ninao, e wawaa Jejee Lutandila aaaaa, ewawaa

Maisha magumu kila kitu ni pesa Jejee,nimekuwa na ukiwa kama vile sijazaa,
Nakuwa ombaomba na watoto ninao, e wawaa Jejee Lutandila aaaaa, ewawaa....

Bridge...

Wanyalukolo eeeee

Musendemule....Musekuwine......E mangala......Musendemule....Musekuwine......E mangala

Chegela.....chegela...chegela e wasawasa....Chegela.....chegela...chegela e wasawasaaa....

E wasaaaaaaaaaaaaaaaaaa
 
Mama - Tancut Almas

Aaa mama aaa.......Aa mama aa......

Miezi tisa ya uchungu tumboni mwako,yote uliyavumilia mamaa,
Uchungu mwingi umeupata aa mama aa, hurumaaa......

Miezi tisa ya uchungu tumboni mwako,yote uliyavumilia mamaa,
Uchungu mwingi umeupata aa mama aa, hurumaaa......

Aa mama aaa, aa mama aa......Aa mama aaa, aa mama aa....

Miezi tisa ya uchungu tumboni mwako,yote uliyavumilia mamaa,
Uchungu mwingi umeupata aa mama aa, hurumaaa......

Miezi tisa ya uchungu tumboni mwako,yote uliyavumilia mamaa,
Uchungu mwingi umeupata aa mama aa, hurumaaa......

Chorus.

Sina cha kukupa mama aa mama aa,zaidi ya asante mama aa mama..
Sina cha kukupa mama aa mama aa,bali shukrani mama aa mama..

Miezi tisa ya uchungu tumboni mwako umenivumilia,matatizo ya utotoni mama umeyavumilia,shule nimesoma mikononi mwako katika shida na raha,hukunitupa mama katika shida na raha,hukunitupa mama sasa nimeoa,nimetoka mikononi mwako mama najitegemea,nimetoka mikononi mwako mama,najitegemea,nikupe nini mama ee,nikufanyie nini mama,asante sana mama,asante sana mama...

Chorus..
Sina cha kukupa mama aa mama aa(mama iyolele),zaidi ya asante mama aa mama..
Sina cha kukupa mama aa mama aa,bali shukrani mama aa mama..

Asante sana mama,shukrani kwako mama, Asante sana mama,shukrani kwako mama , sema nikupe nini mama ee,sema nikupe nini mama nikufanyie nini mama, zawadi gani nikupe kulingana na wema wako,zawadi gani nikupe kulingana na wema wako,sina cha kukupa ee mama,sina cha kukupa,zaidi ya asante...

Chorus.

Sina cha kukupa mama aa mama aa,zaidi ya asante mama aa mama..
Sina cha kukupa mama aa mama aa,bali shukrani mama aa mama..

Bridge...

Mama huyo mama huyo katoka shambani na Mkungu wa ndizi(Mama huyo mama huyo katoka shambani na Mkungu wa ndizi).....

Chorus.

Sina cha kukupa mama aa mama aa,zaidi ya asante mama aa mama..
Sina cha kukupa mama aa mama aa(mama iyolele),bali shukrani mama aa mama..
 
Wifi - Tancut Almas...

Ewe binti uliyeamua kuolewa,na kaka yanguuuu, nakupa pongeziiiiii,
Inadhihirisha wazi,kuwa wewe nana kaka yanguuuuuu mmependanaaa kwa dhati,
Mmejizuia vishawishi vingiiii,mpaka kufikia uamuzi huooo,
Wenzenu wote, twawapa pongezi,hongera dada, hongera kaka....

Mmejizuia vishawishi vingiiii,mpaka kufikia uamuzi huooo,
Wenzenu wote, twawapa pongezi,hongera dada, hongera kaka....

Chorus..

Wifii twende nyumbanii,wifi twende nyumbanii,wifii twende nyumbanii...
Wifi yetu karibu mama,karibu sana hapa ndipo nyumbani kwetu karibu mama...
Wifi yetu karibu mama,karibu sana hapa ndipo nyumbani kwetu karibu mama

Mtunzane na kaka yangu katika maisha yenu,shida yako iwe yake na yake iwe yako,Mheshimiane nyumbani kwenu muzae watoto,muwatunze,muwalee wawe mfano bora...

Wifi yetu karibu mama,karibu sana hapa ndipo nyumbani kwetu karibu mama...
Wifi yetu karibu mama,karibu sana hapa ndipo nyumbani kwetu karibu mama

Muwe wa karimu kwa ndugu na jirani,msiache kuwaheshimu wazazi wenu wote,msisikie maneno ya nje kuhusu maisha yenu,mtakuja kutengana mbaki mnachekwa....

Wifi yetu karibu mama,karibu sana hapa ndipo nyumbani kwetu karibu mama...
Wifi yetu karibu mama,karibu sana hapa ndipo nyumbani kwetu karibu mama....
Iye iye iye iyeeee....
Wifi yetu karibu mama,karibu sana hapa ndipo nyumbani kwetu karibu mama...
Wifi yetu karibu mama,karibu sana hapa ndipo nyumbani kwetu karibu mama....
 
Habari Mr. Balantanda
Naitwa Benson. Mimi ni mwanzilishi wa mradi unaoitwa Tanzania Heritage Project ambao lengo lake kuu ni kuboresha na kukuza nyimbo zilizorekodiwa na Bendi zetu za zamani na im impressed na uchambuzi wako wa hizi bendi.Ningependa kuwasiliana na wewe ili tuweze kuongea ni namna gani tunaweza kufanya kazi pamoja.naomba unitumie email brukantabula@gmail.com ili tuongee vizuri
Shukrani
 
Leo tumalizie na kitu Ashura kutoka kwao Magereza Jazz( wana Mkote ngoma)...Muimbaji ni Nanah Njige

Ashura mimi najuta,mwenzenu kweli najuta sasa,
Ashura mimi najuta,mwenzenu kweli najuta sasa..

Visa ninavyofanyiwa na bwana huyu(bwana huyu),
Nimeamini methali isemwayo(isemwayo) mkataa pema,pabaya panamwita....

Leo hii mwenzenu, Kusema hivi mimi, Nina maana yangu, nilidanganyika,
Kumuacha mume wangu, kumfuata bwana mwingine,
Kumbe ni mwizi baba, kumbe ni muongo.

Visa ninavyofanyiwa na bwana huyu(we Kunyatta),
Nimeamini methali isemwayo(isemwayo) mkataa pema,pabaya panamwita....

Kibwagizo;

Nawausia wanawake wenzangu wote eeh, Muheshimu ndoa zenu zisijevunjika,
Nawausia wanawake wenzangu wote eeh, Muheshimu ndoa zenu zisijevunjika.

Muachane na mabwana wadanganyifu eeeh, Atakupenda wakati una mumeo ooh,
Ukishaachika wala hana habari nawe [Hana habari nawe]

Atakudanganya kwa curl na relaxer, Atakudanganya kwa khanga za Mombasa,
Atakudanganya kwa vitenge vya Zaire, Atakudanganya kwa chips na mayai,
Na starehe za muda hazina mwisho sikia.

Nawausia wanawake wenzangu wote eeh, Muheshimu ndoa zenu zisijevunjika,
Nawausia wanawake wenzangu wote eeh, Muheshimu ndoa zenu zisijevunjika.

Muachane na mabwana wadanganyifu Ashura, Atakupenda wakati una mumeo ooh,
Ukishaachika wala hana habari nawe (hana habari nawe),

Atakudanganya kwa curl na relaxer, Atakudanganya kwa khanga za Mombasa,
Atakudanganya kwa vitenge vya Zaire, Atakudanganya kwa chips na mayai,
Na starehe za muda hazina mwisho Ashura.

Shakaza....

Sehemu ya kwanza iliimbwa na Washirika Tanzania Stars(Watunjatanjata) na sehemu ya pili iliimbwa na Bima Lee Orchestra(Wana Magnet 'Ndele' Tingisha)....Mtunzi ni Hayati Eddy Sheggy 'Mzee Shakaza'

Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom