Wiki hii habari inayotrend Afrika ni Comment ya mtandao wa X(twitter) ya mwanadada Susan Mutami alitabiri kifo cha Mfanyabiashara wa Zimbabwe Wicknell-Chivayo kufariki kwa ajali ya Helicopter hakutaja siku wala tarehe ila aliandika kwa kujiamini ili kutuakikishia utabiri wake utatimia na akaomba post yake itunzwe kama ushahidi. Susan alipost Comment hiyo May 28, 2025
September 30, 2026 Vyombo vya habari nchini Zimbabwe viliripoti kifo cha Chivayo pamoja na mkewe kilichosababishwa na ajali ya helicopter iliyodondoka na kusambaratika baada ya kupata hitilafu ikiwa angani, Utabiri wa Susan kuhusu kifo cha Chivayo kwa ajali ya helicopter ulitimia ikiwa imepita miezi 14
Watu walikuwa na madai tofauti kuhusiana na utabiri wa Susan wapo waliosema ni mchawi wengine Time traveller yaani kila mtu aliongea lake lakini kwa mimi ntakuwa tofauti na mawazo ya watu wengi katika hii ishu
Susan sio mchawi au Time Traveller bali kakutana na hali inayoitwa "Deja Vu"
Deja Vu ni hali ambayo unakutana na matukio uliyowahi kuyaota ndotoni na huwa yanatokea kama marudio na unajua muda flani kitatokea kitu flani na kweli huwa kinatokea kama ulivyotabiri, Hata neno Deja-Vu asili yake ni kifaransa likiwa na maana ya "kimeshaonekana"
Watu wengi ni mashahidi wa kukutana na hali ya "Deja-Vu" kama nilivyoielezea na mimi ni miongoni mwao nimekuwa nikikutana na Deja-Vu mara kwa mara nikaingia katika maswali ili kupata jawabu la hali hii lakini nilikosa majibu ya kueleweka
Nimesoma hali ya Deja-vu katika sayansi na imani, kila utafiti majibu yake yametofautiana kuelezea hali hiyo
Sayansi inaelezea Deja Vu inatokea katika sehemu ya ubongo iitwayo Hippocampus ambayo hushughulika kuhifadhi kumbukumbu badala ya ubongo kuhifadhi tukio la sasa katika kumbukumbu za muda mfupi huchanganya mafaili na kulihifadhi katika kumbukumbu ya muda mrefu na kusababisha tukio kuonekana kama ni la wakati uliopita
Ila katika Imani Deja-Vu imeelezewa kwa namna tofauti kulingana na kila imani
Katika Imani ya kihindu na buddha wanaamini Deja-Vu ni kuzaliwa upya kwa roho hali hiyo huitwa Reincarnation inaaminika roho iliyozaliwa mara ya pili inakutana na hali ya Deja-Vu kwa sababu iliwahi kuishi katika mazingira hayo
Imani nyingine za dini hutafsiri Deja-vu ni ndoto yenye maono huonesha mambo yatakayotokea wakati ujao Wakiamini yakiwa yamepangwa na Mungu
#babusisu