Zimebaki siku nne tu kwa mujibu wa katiba kumtangaza, kuthibitishwa na bunge na kuapishwa kwa Makamu wa Rais

Naona lukuvi akiwa ana ulinzi wa kificho sijajua atakua na post ipi.
 
Wakuu

Kuanzia tarehe 17/3/2021 mpaka leo ni siku kumi. Kwakuwa katiba inatamka ndani ya siku 14 makamu awe amepatikana, basi sasa rais na chama wamebakiwa na siku 4 kutuletea makamu.

Niwatakie kila la heri na watuletee mtu mwenye uwezo.
Katiba inamtaka Rais aliye apishwa kuteua makamu wake ndani ya siku 14 tangu alipo apishwa
 
🤣🤣 Nimecheka sana!!, Wizara ya afya inakoelekea kama hazitachukuliwa jitihada za haraka kuinusuru tunaenda kuipoteza. Gwajima+Mollel,, sijui jiwe alifikiriaga nini au ndio kutokushauriwa
Combination ya hovyo kupata kutokea.
Wapigwe chini mapema sana.
 
Ni kweli kabisa,hawapo kabisa kwenye ubashiri wa watu(kutajwa tajwa)
 
Hatutafut kiongoz wa chama tunatafuta kiongoz wa nchi izo cv za ccm hatuzitak
 
Kigezo cha dini kimefanyaje? Tangu lini Tanzania kukawa na kigezo cha dini kwenye teuzi?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Anaitwa Palamagamba John Aidan Mwaluko Kabudi, alizaliwa Kilimatinde, Manyoni, Singida. Baba yake (Mchungaji na Mwalimu) ni Mgogo na mama yake (Mwalimu) ni Mkaguru wa Kilosa.

Baadae wazazi wake walihamia Mvumi Makulu, Chamwino, Dodoma.
Mtashuhudia vituko..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…