Zinedine Zidane kala shavu Qatar

Zinedine Zidane kala shavu Qatar

Hata hiyo milioni 110 kwa siku bado nyingi sana kwa siku kweli hawa waarabu wana hela za kuchezea.....

Sisi mbona haya mafuta na gesi huku kwetu hayatusaidii....

Kweli muafrika ni muafrika tu....

Wenzetu wametuzidi akili mkuu..tuna rasilimali nyingi sana kuliko huyo Qataar na hata nchi nyingi za europe..lakini hatujui kuitumia ipasavyo.
 
Qatar na mpira wa miguu wapi na wapi? Nadhani lengo lao ni kumtajirisha Zidane tu.

Khalifa-Stadium.jpg


Mkuu, nilidhani wewe pia wafuatilia habari za Qatar khasa hizi za michezo.

PSG inamilikiwa na Qtara Spos Investments waarabu kutoka Qatar.

Manchester City inamilikiwa na Abu Dhabi United Group ambayo ni ya kutoka Qatar.

Fainali za kombe la dunia mwaka 2022 zinagharimu kiasi cha dola bilioni 220 mara 60 zaidi ya fainali za Afrika Kusini mwaka 2010 (dola bilioni 3.5) na fainali za Brazil mwaka 2014 ambazo ziligharimu dola bilioni 12.

Hivyo inawezekana wanataka Zizzou ainoe timu ya taifa ya Qatar ili timu hiyo ije kufanya maajabu kutwaa kombe la dunia nchini mwao.
 
Fake news.
Kuna ukweli hapa. Hii habari itakuwa ya uongo. Nimeitafuta kwenye vyombo vikubwa vya habari sijaiona. Nimeenda bbc sports. Hamna kitu. Tumeingizwa chaka.
Hivi hii habari ilikua April fools?
Picha ya zamani Sana iliyotumika, alipiga Zidane akiwa balozi wakati Qatar inawania nafasi ya ku host world cup.
Kweli hii taarifa kweli tumepigwa changa la macho na mleta mada. Na tulivyokuwa mabwege hata source ya habari hamna tunachangia tu kama mazuzu.
 
Ila we mtoa mada unatuletea tetesi bhana mi mwenyewe nilitaka kushangaa aisee. Hii habari kwenye vyombo vya habari vikubwa haipo.
JamiiForums rekebisheni title isomeke kama tetesi ni fake news hii.
 
Ustazi mwepesi hajawahi kua star ata wa miaka mitatu kilichompa umaarufu ni mechi moja tu ya fainali 1998 pale state de france .....ambayo ilikua France Vs Brazil ila ni mwepesi sana ndio maana ata Perez hamkubali kwa kifupi ana kikosi bora ila si mtaalam wa mbinu za ukocha ata ilo shavu la quatar ni bahati na jina tu....kiufupi ata ikiangalia kina Maradona mara nyingi star kua kocha mzuri hua ni nadra sana

Hiki kikosi alikua nacho Mourinyo alichukua uefa? Kikosi hicho hicho alikua nacho Anceloti alitamba mwaka mmoja uliofuata akachemka, kikosi hico hicho alipewa Benites timu ilikua inaelekea kubaya akafukuzwa akaitwa Zidane, alipewa kikosi kikiwa kinasuasua akabeba ndoo ya CL, wenye chuki zao kama wewe wakasema hawezi kulichukua mara ya pili mfululizo akalichukua, msimu uliopita wenye chuki kama wewe wakasema hawezi kulichukua mara tatu mfululizo akalichukua mara ya tatu mfululizo na kuweka rekodi ya kua kocha wa kwanza kufanya hivo. Kuhusu uchezaji wake nadhani utakua mgeni katika soka kwa taarifa tu Zidane amestafu na kiwango chake ndio maana alistaafia madrid wakati wengine viwango vikishuka wanatafut timu ndogo za kuchezea.
 
Kuna ukweli hapa. Hii habari itakuwa ya uongo. Nimeitafuta kwenye vyombo vikubwa vya habari sijaiona. Nimeenda bbc sports. Hamna kitu. Tumeingizwa chaka.Kweli hii taarifa kweli tumepigwa changa la macho na mleta mada. Na tulivyokuwa mabwege hata source ya habari hamna tunachangia tu kama mazuzu.
Ndio hivyo Mkuu, uongo mtupu. Hata kwenye tetesi hamna. Picha ya zamani sana hiyo.
 
Hongera zidane! Uliona mbali..nenda ukale neema ya waQatar huko ndiyo kwenye pesa bwana achana na hizo za madafu..
 
Back
Top Bottom