Zingatia mambo haya ukiwa gerezani

Notorious thug ungetuambia nini sababu ya wewe kufungwa gerezani

Sababu ya yeye kufungwa sioni kama ni critical hapa maana kila mmoja kule hufikishwa kwa sababu ambazo hazifanani na za yule, kila mmoja ana lake kule, cha msingi nikuomba Mungu akuepushe na huko na hata ikitokea uko kule basi walau hizi A b c alizotoa jamaa angalau zitakuongoza japo nahisi hata hizi ni sawa na bure, uhuru tulionao huku inje nimeona kumbe ni mkubwa mnoo, kama wafungwa huku uraiani wanapaita Ulaya [emoji23][emoji23][emoji23], basi tutembee kifua mbele.
 
ungemuacha tu ajibu mwenyewe.
 
Mkuu embu naomba uniambie kuhusu adhabu ya mboko inayoambatana na kifungo kirefu.

Mfano mheshimiwa Sabaya amefungwa jela na kuhukumiwa kulambwa mboko kadhaa, sikumbuki idadi na wakati huo kakata rufaa.

Swali linakuja: je hizo mboko hutembea siku ya ngapi tangu uingie gerezani kuanza kutumikia kifungo?

Na je kwa mtu aliyekata rufaa hutembezewa mboko hata kabla ya rufaa yake kusikilizwa?
Ni hayo tu.
 
9-- usipende vya watu.
10- ukilala usilale matako juu.
 
Inaonekana unauzoefu na magereza ya tz
 
Ukihukumiwa miaka kadhaa jela na viboko mfano 12 wakat wa kuingia na 12 wakati wa kutoka kinacho fanyika kwanza hawakupigi Hadi uende kwa daktari upimwe afya athibitishe kuwa ni mzima wa afya na kwamba unaweza kumudu viboko baada ya hapo ndo unatembezewa kichapo

hizo 12 ni sawa na 24 maana inahesabiwa 2 ni moja alaf unaweza ukapigwa leo 4 kesho 4 keshokutwa 4 Mara nyingi hawapigi zote kwa siku 1 ila upigaji wake ni wa kimafya siyo kama stail za shule kule utakutana na stail za kibabe
 
Ni bora ukutane na Simba ukurarue ufe uishe kuliko uwe mtovu wa nidhamu gerezani.
Yani kwakifupi gerezani chunga heshima babangu,ukijitoa akili maji utatamka"bhaji"kama una mafua hivi.
Hahaha sana utapigwa rungu
 
KABISA
Maana mule ndani choo kichafu,joto sio poa,harufu nzito ,nguo hambadilishi.
Haujui saa ngapi.zaidi ya asubuhi ukiletewa chai unajua Sasa asubuhi.
Ukiletewa ugali au wali unajua hii mchana usiku Giza likiingia.
Ukitaka kujua NI usiku mzito utaona tu watu wamelala[emoji1787][emoji1787][emoji1787].
Ila kabla ya kulala uwa tunaambiana mwenye redio yake awashe.
Hapo wahuni wanaanza kuimba singeli.ila maisha ya mule Raha Sana mnaishi Kama familia
 
Gerezani ni lazima ufanye kazi ukishakua mfugwa tena kwa nguvu hata wanaoumwa mara nyingine wanafanya kazi wanaambiwa wanasingizia kuumwa kupga kazi ni amri
 
Ugopa kesi ya mauaji kwanza balaa linaanzia ukiwa kituo cha polisi pale ni msala utateswa hadi ufike mahabusu ya gerezani ushaiva
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…