Zingatia mambo haya ukiwa gerezani

Kabsaa
Mkuu

Umeambiwa ukiwa gerezani acha kuchunguza chunguza yaliyowapeleka wenzio
Ni kweli
 
Unatoka nduki risasi nyuma yako
Unatoka nduki kukimbilia wapi? Umeshaambiwa ukiwa mtii na kuacha fujo utaishi. Kutoroka ni Trial and Error - unaweza kufeli jaribio hilo au kuzua jambo baya zaidi kwako hata kilema cha maisha. (kama ukifa in action basi utakuwa umefanikisha lengo).
Yaani umeongea ki-raia sana. Ngoja ikitokea bahati umefika huko ukajaribu.😭
 
Kwenye hizo adhabu ya viboko hua wanachapa sehem gani ?
 
Mfungwa hana thamani
 
Kule hapafai tuwe makini ambao hatujafika huko, nina rafiki alipata msala akapelekwa huko mwaka mmoja butimba, alimpiga mtu akamuumiza ikawa kesi kubwa mpaka akahukumiwa.

Jamaa yangu sikumtenga nilikua naenda kwa mwez mara 2 kumpa moyo asijione kama ametengwa sana.
Mungu alisadia mwana alitoka baada ya kama miez 8 kama sikosei, nilichokiona mule ndani kila nilipokua naenda hakuna uhuru kabisa, kuna utulivu na watu wanaheshimiana , pale kwenye nyavu mnapoongelea dah!!!
hata sio sehem nzur ya kuongea na ndugu yako kumfariji maana kuna kelele kila mtu anataka kuongea na mtu wake.. kila nilipokua namuaga alikua anapenda kusema mwanangu mimi ndo kama hivi unavoona nipo jela
 
Samahan mkuu , umesema usipende kuchunguza au kuuliza wenzio yaliowapeleka jela unaweza kulezea sababu ili tufahamu maana kila mtu ni mfungwa matrajiwa
 
fanya michezo yako yote usiingie jela fulani fulani Mozambique.....au jela za Zambia...Kwa kiasi fulani Tanzania tumejitahidi kwa hizi jela kulinganisha na baadhi ya nchi za Africa...
Mkuu,

Tanzania tumejitahidi kwenye issue nyingi sana ukifananisha na mataifa mengi ya Africa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…