Zingatia mambo haya ukiwa gerezani

Zingatia mambo haya ukiwa gerezani

Gerezani ni sehemu ngumu sana na isiyoelezeka kwa mambo yaliyopo kule ili kupunguza makali ya gerezani unaweza fanya haya mambo.

1-Mfungwa hachagui gereza ni kweli ila unaeza kuchagua gereza wengi wanapohukumiwa huingia gerezani hapa unaeza kutambua gereza ulilopo ni la kilimo au vipi kama ni la kilimo fanya juu chini wewe na ndugu zako uhamishwe hapa ni wewe kusuka mipango na mabwana wakubwa toa fungu ndugu yangu utafia shambani. Bora ukae gereza la mjini huku kazi ni ndogo ndogo magereza ya kilimo ni mateso kazi ni ngumu vifaa butu askari wakali nyapara hawana huruma mbele bunduki nyuma fimbo.

2-Hela ya kula. Gerezani mlo ni mmoja saa nane achana na uji mlo wa gerezani ni kukufanya usife njaa ila sio mlo wa kula mwanadamu wakuu sasa hapa unaweza kuacha hela kwa mapai kwa mwez ukawa unapata msosi kutoka kwa wake za wadau wa pale ongea na ndugu zako angalau waache laki kwa mwezi kama inawezekana usijepata vidonda vya tumbo.

3-Nidhamu. Gerezani nidhamu unafundishwa kwa lazima ila watu sugu wapo pia epuka makundi gerezani utapata shida sana kuna wafugwa wao ni watata labda kuzaliwa au makabila kuna mfugwa alikua ni Mmasai kabila huyu alikua si mwelewa anaeza akaanza kkushambulia muda wowote kutokana na msongo wa mawazo na namba aliyokula kutoka ni 2035 watu kama hawa usijenge urafiki nao akili hua zinafyatuka.

4-Uongozi. Hapa namaanisha upate kitengo kizuri jikoni hua ni ngumu ila unaweza kupata uongozi wa kuongoza wenzako mnapokua kazini simaanishi uwe nyapara hapana unyapara unapewa kwa kuangalia muda uliokaa gerezani na nidhamu yako, hapa nazungumzia kusimamia genge mnapokua kazini kumbuka gerezani kazi ni nyingi na watu ni wengi muhimu ni wewe upatee nafasi ya kuwasimamia vinginevyo mikono itaota sugu na ngozi itapigwa jua kama la mbarali.

5- Marafiki. Anzisha urafiki na askari gereza ambaye labda ni kabila lako lafudhi hazipotei utaweza kumgundua huyu atakusaidia utakapokua mgonjwa au kwenye mambo mengine madogomadogo, askari mara nyingi hua wakali sana ila hamna mwanadamu anayekosa chembe chembe ya huruma atakusaidia kwa kujua huyu ni wa nyumbani. Pia kuna viongozi wa dini ambao ni wafugwa pia hawa watakusaidia kiroho na kukushauri ni watu muhimu pia.

6-Punguza mawazo. Hamna jambo gumu kama kuishi mbali na familia baba,mama,dada,kaka,mke na watoto utakua unawaza sana kuhusu maisha yao na pengo lako jipe moyo sana na jione bado wewe ni mtu kwenye jamiii. Unapokua na kifungo cha chini ya miaka30 ina maana bado una nafasi ya siku moja kutoka gerezani na kuendelea na maisha yako kma zamani usiangalie mwaka utakao toka utakata tamaa wewe amini tyu nitatoka siku si

7-Jifanyie usafi, linda afya yako. Ngozi yako epuka kushare share baadhi ya vitu unapokua kule ndani namaanisha sabuni na vitu vingine unavyokua navyo kwa siri. Jipende usijisuse ni hali ya muda soon utarudi ulaya(uraiani)

8- Usipende kudadisi wenzako
mambo yao au kesi zao acha wao wakuambie vinginevyo wewe pambana na yako,wakili wako endelea kua na mawasiliano nae kupitia ndugu zako kuandaa mikakati ya rufaa na mambo mengine.

N:b. Ni haya machache wadau najua mna mengi karibuni tuendelee kupeana uzoefu na mbinu kwa waliokaa na ambao hawajakaa kila mtu ni mfugwa mtarajiwa tumekaa tumetokaa huenda tukarudi WHO KNOWS!!
Nakuona afisa wa magereza unajipigia chapuo la ulaji [emoji23][emoji23]haya tumekusikia tunakuja kuwapeni hizo laki
 
fanya michezo yako yote usiingie jela fulani fulani Mozambique.....au jela za Zambia...Kwa kiasi fulani Tanzania tumejitahidi kwa hizi jela kulinganisha na baadhi ya nchi za Africa...
naskia kuna jela mnalala wima..chini kote mimaji..Sijui nilinyweshwa kahawa au la
 
Umesema kwa dhati sana ya moyo wako, Mungu yupo na wewe, maana dhamira yako ya utii bila shuruti itakulinda na kukuongoza daima siku zote za mausha yako.
Jela na hospital ni mtakuja hizi place hazina wenyewe.
Sabaya alikuwa akiwapeleka wenzake akitoka akipewa uongozi atothubutu kuwatia ndani watu.Bado bashite
 
images.jpeg.jpg
 
Kwa maelezo haya ni dhahiri Magufuli yupo motoni, maana pamoja na dhahama zote hizi yeye alikuwa anaona hazitoshi aliwasema Askari magereza wawatese kwelikweli wafungwa.

Sijawahi kuona Mtanzania katili kama huyo mwendakuzimu.
Let the dead man rest... kuendelea kumtuhumu mtu aliyekwisha tangulia mbele ya haki haiwezi kutibu majeraha yako.
 
Back
Top Bottom