Lukonge
JF-Expert Member
- Jul 31, 2015
- 1,469
- 2,086
Salaam wanaJamiiForums na watanzania wote kwa ujumla wetu.
Ni ukweli usiopingika kwamba ndani ya wiki mbili zijazo, tunaenda kufanya uchaguzi wa viongozi mbali mbali kwenye Taifa letu.
Pamoja na mengi yaliyokwishaongelewa na kampeni zote zilizofanyika, kuna jambo moja ambalo halijapata mjadala mpana kwenye suala la upigaji kura.
Inawezekana limejadiliwa lakini si kwa kiasi cha kutosha. Hii ni kwa tume, vyama vya siasa, madhebu ya dini, wagombea na wadau wengine wa uchaguzi.
Pamoja na hasira, mihemko na chaguo lolote utakalolifanya wakati wa kupiga kura, tafadhali USIHARIBU KURA YAKO KWA KUJUA AU KUTOKUJUA.
Kuna mambo ambayo pamoja na nia yako nzuri ya kushiriki uchaguzi, ukiyafanya basi unakuwa umeharibu kura yako. Mambo hayo ni:
KUWEKA ALAMA YOYOTE ZAIDI YA TIKI DHIDI YA MGOMBEA UNAEMCHAGUA.
Hivyo, nawasihi ili kutokuharibu kura zetu:
1: Usiandike ujumbe/ maneno yoyote kwenye karatasi ya kupigia kura zaidi ya tiki.
2: Usiweke alama ya kosa kwa mgombea mwingine yeyote zaidi ya tiki kwa unaemchagua.
3: Usichole mchoro wowote kwenye karatasi ya mpiga kura.
4: Usitobie macho au kukoleza chochot kwa wino wa kalamu au wini wowote kwenye karatasi ya mpiga kura.
Zingatia, Ukifanya chochote zaidi ya kuweka tiki kwa unaemchagua, umeharibu kura yako.
Inahitaji uelewa na nidhamu ya hali ya juu na hasa pale ambapo maelekezo haya yatakuwa hayajatolewa kwa msisitizo sahihi.
Ukizingatia kuwa kwa kila kipindi kunakuwa na ingizo la wapiga kura wapya.
Tuwe na uchaguzi mwema na wenye Amani.
Amina