Zipi ni alama za kuwa umefanikiwa kimaisha?

Zipi ni alama za kuwa umefanikiwa kimaisha?

greater than

JF-Expert Member
Joined
Sep 22, 2018
Posts
1,653
Reaction score
3,060
Miaka miwili iliyopita huko Kigamboni,
Nilikuwa natoka kwangu na kwenda dukani kufuata mahitaji, wakati nipo njiani kuna vijana watano walikuwa kwenye mjadala juu ya kufanikiwa.

Ulikuwa mjadala wenye mabishano pia. Walitajwa watu maarufu wengi kama mfano wa watu wenye mafanikio.

Walitajwa : Diamond, Samatta, Dimpoz, Mwamposa, Kiba na wengineo wengi.

Nilisimama na kuwasikiliza ..
..nikachangia kwa kuuliza swali moja
"zipi ni alama kwamba mtu amefanikiwa kimaisha "

Nikawaambia mimi nitajiona nimefanikiwa kama :
  • Kipato changu kilichopo akiba kitaweza Kulisha familia yangu muda wa mwaka mzima bila kuterereka.
  • Nitakuwa na familia yenye amani na upendo.
 
Miaka miwili iliyopita huko Kigamboni,
Nilikuwa natoka kwangu na kwenda dukani kufuata mahitaji,wakati nipo njiani kuna vijana watano walikuwa kwenye mjadala juu ya kufanikiwa.

Ulikuwa mjadala wenye mabishano pia.Walitajwa watu maarufu wengi kama mfano wa watu wenye mafanikio.
Walitajwa : Diamond,Samatta,Dimpoz,Mwamposa,Kiba na wengineo wengi.

Nilisimama na kuwasikiliza ..
..nikachangia kwa kuuliza swali moja
"zipi ni alama kwamba mtu amefanikiwa kimaisha "

Nikawaambia mimi nitajiona nimefanikiwa kama :
  • Kipato changu kilichopo akiba kitaweza Kulisha familia yangu mda wa mwaka mzima bila kuterereka.
  • nitakuwa na familia yenye amani na upendo.
Haya ni mafanikio halisi.
 
Haya ni mafanikio halisi.
Mafanikio ni kua na Mara 3 au 4 zaidi ya kile ulichonacho hapa nazungumzia assets, mifano ni mingi let say unamiliki viwanda zaidi ya vitatu au vinne na kuendelea wewe tayari ni umeshafanikiwa

SIO eti unamiliki kigari kimoja na kijumba kimoja n still bank inakudai Pesa kibao za Mkopo wenye riba za kufa mtu na unakatwa kila mara eti unajiona umefanikiwa hell no ukiteteleka kidogo tu kigari chako na kijumba bank inapiga mnada hajafanikiwa bado
 
Kufanikiwa hakuna maana inayojulikana moja kwa moja, hili swali litajibiwa Kutokana na mtazamo wa MTU binafsi.

Hii mada kuna watu watachanganya kati ya Kufanikiwa au mafanikio Success na kuwa na maendeleo development.

Mimi ntatoa mtazamo kuhusu kufanikiwa na sio Maendeleo.

Kuhusu Mimi kufanikiwa , huwa naangalia pale unapofika hatua ya kuwaathiri watu kwa njia chanya.

Mfano Una pesa au una kipawa fulani jinsi watu wanavyokuwa benefited kupitia ulichonacho tayari umefanikiwa.

Mfano, Diamond tunaona ametoa Sana Ajira kwa watu na hao watu wanaishi vizuri hayo sasa ndo mafanikio.

Hivyo yawezakana Mimi napesa Sana naishi vizuri Ila watu wakaribu yangu wakiwa hawaishi vizuri maana yake sijafanikiwa.

Huo ndo mtazamo wangu kuhusu mafanikio.

NB: Kujenga ghorofa, kuoa, kuolewa, kununua gari kuhamia kwako hayo ni maendeleo - development

Ila kusaidia ndugu aliyekwama Ada, kumuwezesha MTU kibiashara, kuwasapoti wazazi ndugu marafiki n.k hayo huitwa mafanikio. Success.
 
Kwangu mimi mafanikio ni kuwa na uwezo wa kufanya chochote unachotaka, na kuenda mahali popote unapotaka muda wowote unaotaka, ilimradi haumdhuru mtu wala hauvunji sheria za nchi
In which is impossible to any human being at all over around the world and actually an illusion 100%.

Ubinadamu ni kazi/The humanity is a work.
 
Ofcourse ila kwa angle ipi?
Kwa Angle nyingi tu,

Mfano mtu akiweka malengo ya kuacha pombe na akafanikiwa kuacha hayo ni mafanikio kwake coz ametimiza lengo lake,
Mtu akiwa na lengo la kununua Baiskeli na akainunua hayo ni mafanikio yake,ndio maana nikasema kua mafanikio ni kutimiza malengo uliojiwekea coz binadamu tuna malengo tofauti tofauti,

Donald Trump ni tajiri ila alikua na lengo la kugombea urais wa US,baada ya kushinda ikawa ametimiza lengo lake,so hapo amefanikiwa,ni mafanikio kwake kwa kutimiza lengo lake.
 
Ukianza kuwavimbia wenzako na kuwaona ni wabaya wako baada ya kupata ajira kubwa na yenye hadhi hasa serikalini. Na wenzako haohao mlikuwa mki-hangout pamoja na mkiwasiliana Ila saiv unawaona vidasi... Basi ujue umeshafanikiwa ila una Umasikini sugu wa kurithi na wa kimawazo.
Hii angle uliyofkiria ni hatari sana......yani ni kama mashairi ya chekacheka ambapo hakuna hata moja la kuchekesha.
 
Mimi nikiwa na uhakika wa kula dona na dagaa kauzu......nikibakiwa na mia mbili ya gahawa.......najiona tajiri kabisa......
 

Attachments

  • 1002138772.jpg
    1002138772.jpg
    51 KB · Views: 6
Back
Top Bottom