Zipi ni alama za kuwa umefanikiwa kimaisha?

Zipi ni alama za kuwa umefanikiwa kimaisha?

Miaka miwili iliyopita huko Kigamboni,
Nilikuwa natoka kwangu na kwenda dukani kufuata mahitaji, wakati nipo njiani kuna vijana watano walikuwa kwenye mjadala juu ya kufanikiwa.

Ulikuwa mjadala wenye mabishano pia. Walitajwa watu maarufu wengi kama mfano wa watu wenye mafanikio.

Walitajwa : Diamond, Samatta, Dimpoz, Mwamposa, Kiba na wengineo wengi.

Nilisimama na kuwasikiliza ..
..nikachangia kwa kuuliza swali moja
"zipi ni alama kwamba mtu amefanikiwa kimaisha "

Nikawaambia mimi nitajiona nimefanikiwa kama :
  • Kipato changu kilichopo akiba kitaweza Kulisha familia yangu muda wa mwaka mzima bila kuterereka.
  • Nitakuwa na familia yenye amani na upendo.
Kuna tofauti kati ya "kufanikiwa kimaisha" na "kutajirika"

Binafsi yangu mafanikio ya kimaisha ni pale ambapo unayo amani na furaha thabiti ya moyo wako juu ya maisha yako
 
Kufanikiwa ni kutosheka yan we utafuti tena unatafutiwa ila kama unaendlea kutffuta bado hujafaikiwa
 
Kusalimiwa na watu wazima 😊
Angali ni bwana mdogo.

Just kidding ndo nilichofanikiwa Mimi kwasasa na kitendo Cha kupewa salamu na watu wakubwa Tena ya kipekee tofauti na wengine uliokuwa nao inakuongezea kujiamini na kujitafuta zaidi
 
Miaka miwili iliyopita huko Kigamboni,
Nilikuwa natoka kwangu na kwenda dukani kufuata mahitaji, wakati nipo njiani kuna vijana watano walikuwa kwenye mjadala juu ya kufanikiwa.

Ulikuwa mjadala wenye mabishano pia. Walitajwa watu maarufu wengi kama mfano wa watu wenye mafanikio.

Walitajwa : Diamond, Samatta, Dimpoz, Mwamposa, Kiba na wengineo wengi.

Nilisimama na kuwasikiliza ..
..nikachangia kwa kuuliza swali moja
"zipi ni alama kwamba mtu amefanikiwa kimaisha "

Nikawaambia mimi nitajiona nimefanikiwa kama :
  • Kipato changu kilichopo akiba kitaweza Kulisha familia yangu muda wa mwaka mzima bila kuterereka.
  • Nitakuwa na familia yenye amani na upendo.
Kama unaingiza kipato cha kukidhi mahitaji yako na familia, elimu Bora, nyumba, na unaweza ukaenda vacation hata zenj, wewe familia, MTU nne, tena kwa pipa, hata ukifikisha 70yrs, bado unakiapto kinakuja, aaaah wewe ni mwamba
 
Ngoja nijitutumue nitimize hayo.
 
Kufanikiwa hakuna maana inayojulikana moja kwa moja, hili swali litajibiwa Kutokana na mtazamo wa MTU binafsi.

Hii mada kuna watu watachanganya kati ya Kufanikiwa au mafanikio Success na kuwa na maendeleo development.

Mimi ntatoa mtazamo kuhusu kufanikiwa na sio Maendeleo.

Kuhusu Mimi kufanikiwa , huwa naangalia pale unapofika hatua ya kuwaathiri watu kwa njia chanya.

Mfano Una pesa au una kipawa fulani jinsi watu wanavyokuwa benefited kupitia ulichonacho tayari umefanikiwa.

Mfano, Diamond tunaona ametoa Sana Ajira kwa watu na hao watu wanaishi vizuri hayo sasa ndo mafanikio.

Hivyo yawezakana Mimi napesa Sana naishi vizuri Ila watu wakaribu yangu wakiwa hawaishi vizuri maana yake sijafanikiwa.

Huo ndo mtazamo wangu kuhusu mafanikio.

NB: Kujenga ghorofa, kuoa, kuolewa, kununua gari kuhamia kwako hayo ni maendeleo - development

Ila kusaidia ndugu aliyekwama Ada, kumuwezesha MTU kibiashara, kuwasapoti wazazi ndugu marafiki n.k hayo huitwa mafanikio. Success.
Kuna vitu vitatu hapa.

01. Mafanikio
02. Maendeleo
03. Utajiri
 
Mafanikio
- Ni kutimiza KUSUDI ambalo umeumbwa kwalo. Tunajua kuwa mbali na shughuli zetu za kila siku, Kila mtu ameumbwa ili kuja kuwa faida fulani kwa watu. Yaani KUSUDI la kuumbwa kwa mtu ni ili iwe faida kwa watu. Kama alibyosema DR HAYA LAND.
Tafsiri nyepesi "UMEKUJA KUFANYA NINI DUNIANI"

Maendeleo
- Ni kupiga Hatua fulani katika Maisha inaweza kuwa, kifedha (Kiuchumi), Kisaikologia (HISIA & AKILI), Kielimu (Kufikia level fulani ya maendeleo). Maendeleo yanaweza kuwa General (Kinchi, Kikanda, Kimkoa au kikabila), Personal (Kila mtu anajipima yeye kama yeye zidi ya Mipango/Malengo yake). KUMBUKA- Unaweza niona (Kunipima) kwa kuniangalia eneo la kifedha na ukasema sijafanikiwa ila ukiniuliza ntakwambia nimefanikiwa kielimu au kifedha maana ndoto yangu ilikuwa kuwa na nyumba (Hivyo nikijipima NTASEMA, Nimefanikiwa).

Utajiri.
Kama Neno jenyewe UTAJIRI. Hii tunaipima kifedha au UWEKEZAJI au umiliki wa vitu vya thamani.
  • Investment.
  • Businesses.
  • Possession (Gari, Nyumba, Viwanja)
Kiwango chako cha Umiliki, UWEKEZAJI na fedha ndio inaunda Tafsiri ya utajiri au umiliki wa vitu vya thamani.(Wealth/ Possession).

Hivyo kujibu swali lako ni kuwa.
Mafanikio ni kipimo cha kutimiza KUSUDI la kuumbwa kwako (Kipimo Binafsi, kwani wewe ndie unajua Nini ni KUSUDI lako). Kiufupi UMEKUJA DUNIAN KUFANYA NINI????

greater than
 
Back
Top Bottom