Zipi ni alama za kuwa umefanikiwa kimaisha?

Nilitaka uongee namna hiyo💪
 
Mafanikio ni ile level ambayo mtu humtegemei mtu mwingine kwenye basic need za kibinadam hapo tyr ushafanikiwa mana unaweza lea familia bila shida ss kama hata kula yako tu tabu hata kama una amani na upendo hujafanikiwa bado
 
Mafanikio ni ile level ambayo mtu humtegemei mtu mwingine kwenye basic need za kibinadam hapo tyr ushafanikiwa mana unaweza lea familia bila shida ss kama hata kula yako tu tabu hata kama una amani na upendo hujafanikiwa bado
Well,ndiyo mana nkasema nikiwa na kipato cha akiba cha kuweza kulisha familia mwaka mzima....

And binadamu kutegemeana ni jambo lisiloepukika,,,,
 
Kwangu mimi mafanikio ni kuwa na uwezo wa kufanya chochote unachotaka, na kuenda mahali popote unapotaka muda wowote unaotaka, ilimradi haumdhuru mtu wala hauvunji sheria za nchi
Nakubali, utajiitaje umefanikiwa ila hauna financial freedom..

Huwezi kula unachokitaka

Huwezi kuhimili medical bills kwenye hospitali zinazoeleweka

Huwezi kusafiri kwa usafiri unaoupenda

Savings zinawekwa ili ziliwe next month

Haya sio mafanikio Ila ni kupiga hatua tu kwenye maisha

Lakini pia kufanikiwa yaweza kumaanisha fullfillment inayotokana na mtu kufikia malengo aliyoyatamani. Maana kuna wengine wanapenda umaarufu, kusaidia watu au kuweza kuishi kutokana na vipaji vyao etc

Kwa hiyo wewe unaweza kumuona hajafanikiwa Ila amepata fullfillment aliyoitaka. So, hata hayo ni mafanikio
 
Maisha ni ubatili mtup
Only if it was Just a statement, but unfortunately it's not, that's the reality 🙂🙂
maisha ni ubatili mtupu- hii kauli huwa inaongelewa na WATU ambao hawajafika hatua inaitwa Self- actualization ambao hawajazigusa jamii zao kwa njia chanya


Ya duniani na mbinguni yote katoa Mungu hivyo every day is a gift from God. To say life is illusion inafikirisha.
 
Hapo kwenye maendeleo na mafanikio nimekuelewa.
 
Binadamu hawezi kuyafanikisha maisha mpaka anakufa
 
hili swali litajibiwa Kutokana na mtazamo wa MTU binafsi.
Na mazingira husika ya eneo

Kwa mfano mtu anayesema amefanikiwa kijijini ni wa tofauti na mjini

Mtu anayesema amefanikiwa Marekani ni tofauti na mafanikio ya mtu wa Tanzania

Mtazamo wa mtu binafsi na eneo analoishi vinaamua ikiwa mtu atajiona amefanikiwa au la
 
Kwangu mimi mafanikio ni kuwa na uwezo wa kufanya chochote unachotaka, na kuenda mahali popote unapotaka muda wowote unaotaka, ilimradi haumdhuru mtu wala hauvunji sheria za nchi
Kwa mantiki hii, rais wa Tz unaweza kusema amefanikiwa?
 
Yeah nakubaliana na wewe mkuu, ila kama nilivyosema huo ni mtazamo wangu binafsi na si maana ya moja kwa moja ya neno mafanikio, hili neno sidhani kama lina maana ya jumla kila mtu hutoa maana kulingana na mtazamo wake hivyo kubaki kuwa moja ya masuala mtambuka
 
Mkuu kusema maisha ni ubatili haimaanishi watu hawatakiwi kutafuta mafanikio na kuyafurahia maisha, wewe pambana na furahia maisha yako wazungu wanasema "enjoy it while it lasts" ila hiyo haibadili ukweli kuwa maisha ni ubatili, Mfalme Suleiman alipewa vitu vingi vizuri na alifanya mambo mengi mazuri ila mwisho wa siku alikiri kwamba yote ni ubatili na kujilisha upepo tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…