Zipi ni alama za kuwa umefanikiwa kimaisha?

"Mimi nimefanikiwa kung'oa pisi Moja matata hapa mtaani kwetu! Ilikuwa inanisumbua Kwa muda mrefu".

Tusipangiane maisha
 
"Mfalme Suleiman alipewa vitu vingi vizuri na alifanya mambo mengi mazuri ila mwisho wa siku alikiri kwamba yote ni ubatili na kujilisha upepo tu"
 

Philanthropist - ndo hatua nakuombea uifikie .

Ukiwa philanthropist utaweza kujiona vizuri
 
Mafanikio sio lazima pesa na mali.

Hata ukibadili mtazamo wako wa maisha tu nako ni kufanikiwa.
 
Kufanikiwa ni Kutimiza kusudi la Mungu aliloweka ndani Yangu, Na hatimaye baada ya kutimiza kusudi hilo niweze kufika kwake yeye aliyenileta.
 
Hata freemason na watoa kafara wenye vipato na matajiri wanalisha familia mwaka mzima bila kutetereka

Hata wanasiasa mafisadi na wezi wanafamilia zenye amani na upendo (kwa sababu ya pesa) mf. Nape
 
Watu wanamiliki viwanda vya kumwaga ila hawana uwezo wa kuzaa, wengine wana madonda yanayotoa funza, wengine wanafuga majoka n.k Nao wamefanikiwa kimaisha?
 
Watu wanamiliki viwanda vya kumwaga ila hawana uwezo wa kuzaa, wengine wana madonda yanayotoa funza, wengine wanafuga majoka n.k Nao wamefanikiwa kimaisha?
Wewe umesema nimesemaje ukiwa na Mara 3 au 4 ya kile ulichonacho km assets wewe tayari umefanikiwa mfano una mashamba Ekari 100 au Ekari 200 matatu au Manne na umepanda miti ya mbao ya kutosha wewe tayari umefanikiwa baada ya miaka Kumi unashika mabillion mkononi hapo tayari umeshafanikiwa
 
Unaweza kufanya hayo yote lakini bado ukawa haujafanikiwa, Mfano Mobutu Seseseko Alikuwa na mali nyingi na alisaidia ndugu zake, Je na yeye alifanikiwa? Tujifunze kutambua mafanikio ya Kimwili, Nafsi na Roho.
 
Kwangu mimi mafanikio ni kuwa na uwezo wa kufanya chochote unachotaka, na kuenda mahali popote unapotaka muda wowote unaotaka, ilimradi haumdhuru mtu wala hauvunji sheria za nchi
Yote hayo yana maana gani kama hauna mguu mmoja, hauna uwezo wa kuzaa, una masharti ya kafara n.k? Ukipewa sharti la kuhasiwa haumdhuru mtu wala kuvunja sheria ila nafsi yako haijafanikiwa
 
Unaweza kufanya hayo yote lakini bado ukawa haujafanikiwa, Mfano Mobutu Seseseko Alikuwa na mali nyingi na alisaidia ndugu zake, Je na yeye alifanikiwa? Tujifunze kutambua mafanikio ya Kimwili, Nafsi na Roho.


Mafanikio hayana definition ndo maana hapa kila MTU anakuwa subjective anatoa mtazamo wake


Usi-question utaharibu mada.

Wenzako wamezungumzia kiuchumi wengine kijamii sasa umezungumzia kiroho

Na ukizungumzia kiroho unakuwa upo subjective
 
Mafanikio ni ile level ambayo mtu humtegemei mtu mwingine kwenye basic need za kibinadam hapo tyr ushafanikiwa mana unaweza lea familia bila shida ss kama hata kula yako tu tabu hata kama una amani na upendo hujafanikiwa bado
Kama simtegemei mtu ila namtegemea Jini nyoka a.k.a Ndumba kwa sharti la kidonda, hapo nimefanikiwa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…