ngongoti2000
JF-Expert Member
- Nov 20, 2017
- 2,236
- 2,142
Hello!
Kuajiri mtu akufanyie shughuli zako sasa hivi ni kitu kinachosumbua sana watu wengi, nikiwemo. Ukisema uajiri ndugu tegemea maumivu tu yasioelezeka.
Ukisema uajiri rafiki tegemea kabisa urafiki kuvunjika hakawii kukuzunguka. Nyie wenzangu mnatumia njia gani bora za kuajiri mtu MWAMINIFU? Yaani ile kazi unamwachia hela ndefu ukisubiria returns, maana huwezi fanya kila kitu mwenyewe.
Ipi ni njia sahihi ya kumpata mtu atleast mwaminifu. Au ulimpataje mtu mwaminifu?
Nawasilisha.
Ni changamoto sana.....watu hakuna kabisa...kuna kipindi nilikuwa natamani ili nimpe mtu kazi aache kiungo chake muhimu kwangu kama dhamana......ila njia ninayoitumia kwa sasa nikumpa mtu hisa (kama 5 - 10%) ya faida naye ajisikie kama mmiliki badala ya kumlipa kama kibarua...hii imenisaidia kidogo....Biashara nyingine ambayo hainiumizi kichwa kabisa mpaka sasa ni mobile money ambayo ni mjinga tu anaweza kudokoa sababu utamshika kirahisi...ripoti zote zinatumwa online