Zipi ni njia bora za kumpata mfanyakazi mwaminifu

Zipi ni njia bora za kumpata mfanyakazi mwaminifu

Wangari Maathai

JF-Expert Member
Joined
Aug 13, 2018
Posts
34,962
Reaction score
70,576
Hello!

Kuajiri mtu akufanyie shughuli zako sasa hivi ni kitu kinachosumbua sana watu wengi, nikiwemo. Ukisema uajiri ndugu tegemea maumivu tu yasioelezeka.

Ukisema uajiri rafiki tegemea kabisa urafiki kuvunjika hakawii kukuzunguka. Nyie wenzangu mnatumia njia gani bora za kuajiri mtu MWAMINIFU? Yaani ile kazi unamwachia hela ndefu ukisubiria returns, maana huwezi fanya kila kitu mwenyewe.

Ipi ni njia sahihi ya kumpata mtu atleast mwaminifu. Au ulimpataje mtu mwaminifu?

Nawasilisha.
 
Ili kumpata mfanyakazi muaminifu, mlipe vizuri. Mpe ahadi za kumsaidia endapo atafikisha lengo.

Kuwa karibu naye na umjali. Muambie kuwa unaona kila sababu ya kumuamini. Kwamba nafsi yako inamtuma kumuamini.

Upande wa pili mtie hofu ila siyo wewe mwenyewe. Watafute watu kadhaa watakaoenda kumpeleleza na kumuambia kuwa wewe unapenda watu waaminifu. Kwamba kila aliyejaribu kukufanyia hila, cha mtema kuni alikiona.

Lakini kabla ya kuyafanyia kazi yote hayo, mchunguze na kumjua kabla ya kumuamini.
 
Kuna wakat I unapaswa kujua kuwa kumiliki pesa ni raisi kuliko kuzizalisha ziongezeke

MI nilitumia njia ya kumpa posho kila siku na mshahara ukiwa pale pale

Na alikuwa akiuza vizur posho iliongezeka Zaid

Kuiba ataiba ila atajikuta nae anakosa posho

Sasa mwingine unampa hizo ofa lakini bado akawa hajitambui!
 
Pole sana...

Ni ngumu sana... Wengi ukiwaajiri wanakua na big expectations bile kujali kama wanafilisi...

It's really sad, kupata muaminifu asilimia zote ni ngumu, ila tafuta yule ambae utaweza kumthibiti...

Cc: mahondaw
 
Rasimisheni biashara zenu.

Hiyo ndio tiba.

Kila mfanyakazi apewe Mkataba, Job Description na Responsibilities.

Afanye Kazi na Kutoa Report Kwa Seniors !

Acheni Kuji-embed Kwenye Biashara. Yaani Biashara Ndio Ninyi Na Ninyi Ndio Biashara

!
 
Ili kumpata mfanyakazi muaminifu, mlipe vizuri. Mpe ahadi za kumsaidia endapo atafikisha lengo.

Kuwa karibu naye na umjali. Muambie kuwa unaona kila sababu ya kumuamini. Kwamba nafsi yako inamtuma kumuamini.

Upande wa pili mtie hofu ila siyo wewe mwenyewe. Watafute watu kadhaa watakaoenda kumpeleleza na kumuambia kuwa wewe unapenda watu waaminifu. Kwamba kila aliyejaribu kukufanyia hila, cha mtema kuni alikiona.

Lakini kabla ya kuyafanyia kazi yote hayo, mchunguze na kumjua kabla ya kumuamini.
Hii ni manipulation....
Kama wewe sio wa moyo huo ipo siku utateleza tu na ndipo sura yako halisi itakapoonekana, Omba sana huyo mtu utakaemfanyia hivyo awe mstaarabu ila kama haramia utakuwa umemuumiza kwa kumfanya mjinga.

Pay back yake hata shetani huwa anakaa pembeni kuchukua lessons..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ili kumpata mfanyakazi muaminifu, mlipe vizuri. Mpe ahadi za kumsaidia endapo atafikisha lengo.

Kuwa karibu naye na umjali. Muambie kuwa unaona kila sababu ya kumuamini. Kwamba nafsi yako inamtuma kumuamini.

Upande wa pili mtie hofu ila siyo wewe mwenyewe. Watafute watu kadhaa watakaoenda kumpeleleza na kumuambia kuwa wewe unapenda watu waaminifu. Kwamba kila aliyejaribu kukufanyia hila, cha mtema kuni alikiona.

Lakini kabla ya kuyafanyia kazi yote hayo, mchunguze na kumjua kabla ya kumuamini.
HHii mm imefeli kbs mkuu!
 
Unapotafuta kwanza zingatia umri mfano vijana 18-23 wachache hapo kati wanakuwa ndio wanaanza maisha na hawana experience kubwa ya maisha ukiwa nae utaweza kumcontrol na yeye huwa muoga . Ukikuta ni mwizi Basi toka utoto wake

Pili pendelea wafanyakazi ambao sii wajanja kivilee , washamba washamba Kama kazi unamfundisha wewe

Yote kwa pamoja huku mshahara wake mpe kwa wakati ule mliokubaliana na viposho vya hapa na pale .
 
Kwa mtanzania hiyo sahau, mtu atakuja na shida analialia unampa kazi, unamlipa vizuri anafanya kazi kwa uaminifu uliotukuka baada ya muda anasahau alipotoka wizi unaanza ukichelewa anakufilisi mpk shilingi ya mwisho ndio moyo wake utasuuzika, anarudi tena kwenye maisha ya tabu anapata sehemu nyingine anatulia kwa muda anarudia yale yale

Suluhisho, kwanza hakikisha upo eneo la kazi mwenyewe kila siku au baada ya siku 2/3

Rejea mwanzo, tambua nature ya mfanyakazi ni kuharibu hapa, anarukia pale na pale kwahiyo mtumie vizuri kipindi ni asset yaani muaminifu baada ya muda ukinusa tu harufu ya wizi muondoe haraka tafuta mwingine na yeye hivyo hivyo.

Usidanganyike na mikataba ya kazi nimeshuhudia hili mfanyakazi mwingine akikaa wiki anaanza matatizo na huwa wanakuwa na kiburi akiamini mkataba unamlinda na huna la kumfanya, pia utashindwa kufanya mabadiliko ya haraka akizingua. Weka mkataba wa kulinda mali zako tu usiweke mkataba wa ajira

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom