Zipi sababu za wanaume kubambikiziwa watoto wa wanaume wenzao?

Frumence M Kyauke

JF-Expert Member
Joined
Aug 30, 2021
Posts
630
Reaction score
1,262
Ndugu zangu kila mmoja wetu achangie mada hii ili tupate kiini cha swala hili. Kuna baadhi ya wanaume wametunza watoto ambao si wao, kuanzia mimba mpaka ukubwani kwa kuwasomesha kwa gharama kubwa pasipokujua kuwa sio watoto wao.

Baadhi ya familia zinaishi na watoto wasiokuwa wa baba mwenye familia na hata kurizishwa mali huku baba mwenye familia akijuwa kuwa ni watoto wake.

Sababu kubwa ni ipi ukizingatia kuwa baba wa familia hiyo hana matatizo ya kutungisha mimba.
 
Kiafrika, mtoto ni Mtoto wa Kila MTU, Haya mambo ya biological father yameletwa kuharibu ustawi wa family tu.

Kuna makabila Tanza-nia Mtoto ni WA Mjomba, yaani usitarajie uende Kusini au Pwani umzalishe Binti Kisha udai Mtoto! Subutuuuuu, mtoto ni WA ujombani.....Ina logic Fulani Hivi
 
Huoni kuwa kuna utamu zaidi pale mtoto anapokuwa wako wa kumzaa?
 
Hili Ni suala mtambuka Sana
Sababu zinang'ata kote kote
Kwa sisi wanaume na wanawake pia
 
Mwanaume ukiwa
1. Huna hela, huna future
Huwezi bambikwa mimba Wala kusingiziwa mtoto.

2. Huna Ela, ila una future
Mimba utabambikwa, mtoto akizaliwa kadi za clinic zinakua mbili.

3. Ela unayo, na future unayo
Mimba utabambikwa, utalea mimba na kusomesha mtoto mpk chuo kikuu
 
Na ni Kati ya mambo yanayochangia kuwa na jamii yenye watu waliopungukiwa na karama, vipawa, baraka, kibali n.k

Asikudanganye mtu mtiririko wa baraka unaanzia kwa Mungu muumbaji kwenda kwa baba

Kumnyima mtoto connection na baba yake ni kumnyima baraka zake toka kwa Mungu. Unaweza kujisemea mbona mtoto yupo powa tuu lakini amini kipo kikubwa anachokikosa

Baba hubarikiwa na Mungu kadri ya neno lake na baba hubariki wanawe
 
Uzi ufungwe.

Ukiwa huna hela utanyang'anywa watoto hata wa damu yako kabisaaa
 
Ndugu zangu kila mmoja wetu achangie mada hii ili tupate kiini cha swala hili. Kuna baadhi ya wanaume wametunza watoto ambao si wao, kuanzia mimba mpaka ukubwani kwa kuwasomesha kwa gharama kubwa pasipokujua kuwa sio watoto wao.

Baadhi ya familia zinaishi na watoto wasiokuwa wa baba mwenye familia na hata kurizishwa mali huku baba mwenye familia akijuwa kuwa ni watoto wake.

Sababu kubwa ni ipi ukizingatia kuwa baba wa familia hiyo hana matatizo ya kutungisha mimba.
Kama mwanamke yuko ndani ya ndoa akibeba mimba na sio ya mme wake lazima ambambikizie mume ili kuepusha aibu

Kama hayuko ndani ya ndoa anaangalia wapi kuna manufaa ndo anakopeleka mtoto

Japo wapo wanaopeleka watoto kwa wanaume wanaowapenda bila kujali manufaa kama vile hali ya uchumi. Hii nimeishuhudia kwa ndugu yangu mmoja, ye aliniambia kabisa "jamaa mwenye huyu mtoto nilikuwa simpendi nilitaka apite tu aende zake ila ndo hivyo bahati mbaya imetokea, mi nampenda fulani na ndo nitamtaja kuwa baba wa mtoto". Siri tumeibeba moyoni mi na yeye.
 
Na ni Kati ya mambo yanayochangia kuwa na jamii yenye watu waliopungukiwa na karama, vipawa, baraka, kibali n.k

Asikudanganye mtu mtiririko wa baraka unaanzia kwa Mungu muumbaji kwenda kwa baba

Kumnyima mtoto connection na baba yake ni kumnyima baraka zake toka kwa Mungu. Unaweza kujisemea mbona mtoto yupo powa tuu lakini amini kipo kikubwa anachokikosa

Baba hubarikiwa na Mungu kadri ya neno lake na baba hubariki wanawe
Nakazia ✍️✍️
Jambo la msingi sana hili
 
Back
Top Bottom