Zipi tamu na chungu za mimi kumiliki BMW X3

Sawa...wewe bmw yako unafanyia wapi service?
 
Vp wana ndugu,

Nafikiria kununua BMW x3, ningependa mniongoze faida na changamoto za kuwa na gaira aina kama hii.

Na mengine mengi mtakayoona yanafaa kuhusu gari hili tungependa kuyasoma yote na wana JF walioko concerned.

KARIBUNI
BMW X3 yenye engine ya DIESEL ni nzuri zaidi kama unapenda mbio na yenye nguvu kuna Cc 3000 itafaa lakini pia kuna yenye cc 2000 japo bajeti yake ni zaidi ya 30M hadi 40M

BMW X3 yenye Engine ya petrol ina Cc 2400 hii inafaa sana kwa bajeti yako kwa sababu bai yake inacheza kati ya 20M hadi 30M ila ina matumizi makubwa kidogo ya mafuta ukilinganisha na ile ya Diesel

Kama unawezakuwa na option ya kubadili mawazo kidogo ningekushauri uangalie na VolksWagen Tiguan yenye Engine ya Petrol (japo zipo aina nyingi) na Cc 2000 hii itakufaa sana ina matumizi mazuri ya mafuta na ni gari nzuri sana japo ni ndogo kidogo kwa ukubwa ukilinganisha na BMW X3

Wataalamu watajazia nyama kidogo
 
Kwa uzoefu wangu wa kuendesha BMW for 3 years now (ikiwa ndio gari yangu ya kwanza), achana na hii gari kama pesa yako ni ya mawazo. Most of hizi gari sisi tunanunua huku ni za below 2010, wachache sana wanunua up to 2015. Kwenye huu umri gari inahitaji replacement ya vitu vingi sana na hapo shida ndio inapoanzia. Na ndio maana BMW ni miongoni mwa gari ambazo ni rahisi sana kuzinunua. Mtu mwenye 13 M anapata 320i ya maana kabisa ila IST hupati.

BTW, ni chuma tamu sana. Ukizoea kuendesha hii then ukapewa toyota ya ajabu ajabu, utateseka sana.
 
Mkuu hizi BMW sikuhizi zipo nyingi Sana mtaani hasa 320i, X1,X3 na X5
Acha wanaonunua waendelee kununua Tu maana Ile kasumba ya kumiliki Toyota itapungua
 
Kodi vp Mkuu
 
Chagua gari ...ingia kwenye tra calculator. Utaona kodi jumlisha na ya clearing agen plus TPA.

MIMI nina BMW ya 2012 ....ukihitaji msaada wa lolote nicheki.
X5 natumia huku Perth nipo kikazi mpaka April 2025 nataka nirudi nayo bongo
 
2013 subaru engine SJ5 unaweza kuipata kwa 25m Max ( Kodi 10M, CIF 12-14M), kuliko kuchukua overpriced Toyotas
 
Hata toyota ukitaka plug original bei ni hiyo hiyo, engine kama ni synthetic pia kwa toyota bei ni hiyo hiyo. Nna bmw e60 toka 2019 sijawahi kuwa na major breakdown ila magari ya ulaya inabidi upende kusoma na kujua tatizo la gari uzuri forums zipo kibao ila magari ya kijapani forum zimeandikwa kijapani. Gari za ulaya zinataka owner anaejua gari na fundi anaejua au kuelezeka. Otherwise uwe na hela kupeleka garage nzuri kama kwa mlebanon, atlantic, dmag etc au DT Dobie
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…