Zipo taarifa kwamba walioshirikiana na Naibu waziri wa Sheria kufanya ukatili wamekimbilia nchini Kenya kujificha kupoteza ushahidi

Resilience

JF-Expert Member
Joined
Jan 4, 2023
Posts
1,096
Reaction score
4,948
Nimeona taarifa kutoka mitandaoni zikieleza kwamba walioshirikiana na Mbunge wa Babati kwemwekea kijana wa Kitanzania chupa Makalioni wamekimbia na kwenda kujificha nje ya nchi kwa maelekezo ya Naibu waziri.

Lengo la watuhumiwa kutoroka nikukwepa kuhojiwa kwa madai kwamba kesi inayofuatiliwa sasa inapanga kumtenga Mhe. Naibu waziri na tuhuma hizo badala yake wasaidizi wake wabebeshwe huo mzigo.

Jeshi la polisi fuatilieni njama Hii mapema kwani hakuna ajuaye kesho Maelekezo yatakuwa upande wa Mbunge au yatakuwa upande wa Jamii? Endapo yatakuwa upande wa jamii je wanasiasa watashindwa kuwatoa kafara polisi na kuwawajibisha kwa kutochukua hatua au kutorosha watuhumiwa?

Akili za kuambiwa changanyeni na zenu......RPC timiza wajibu wako jambo hili halipo sawa kama ilivyoonekana hapo awali. Barua ya utengezi na audio ya mdogo wa mtuhumiwa akijinadi hakuna wa kumkamata ana anaweza akaua vimechochea kasi.

DPP sidhani kama atachukua hatua kwa sababu huyu aliyefanya haya ni bosi wake. Ila kama ni kutoa ushauri basi aachane na ubosi achukue hatua.


Kuhusu chama cha mapinduzi, sidhani kama ni sahihi kama chama kukaa kimya kwenye tuhuma hizi za mwanachama wao. Ukimya utakinzana na misingi ya haki na kwamba kukemea kuna tija zaidi kuliko kukaa kimya kikatili
 
Msemaji wa Chama Cha Mapinduzi,anasemaje kuhusu hili,au anasubiri mpaka Kamati Kuu au Halmashauri Kuu ikutane?, Mbona mambo mengine Chama kilikuwa kinatoa Maagizo huko Kanda ya Ziwa
Hahahaa anawatembelea wastaafu kwanza . Chama kinaagiza
 
Shahidi namba moja aka dogo atatueleza na kumtambua mtoa bastola na mtoa amri ambaye bila shaka yupo na baada ya hapo huyo ndio atatafuta na kuwataja wenzie.

La msingi ni sheria kufuata mkondo wake, na ikigundulika ni kweli basi mhusika mkuu na wenzie wawajibike japo ni vyema kwa sasa awe mahabusu akisubiri uchunguzi ukamilike kama mahabusu wengine...
 
shida yetu watanzania nasisi wanyonge sana, ingekuwa nchi nyingine kwasasa hapo babati hapakaliki mpaka mhusika akamatwe.

Raia sasa tujifunze kujitetea hasa pale tunapoona sheria inataka kupindishwa kumfavor fulani.
 
Bora dogo asije potezwa kiaina
 
Leo mchana vijana walienda kuzuia gari ya serikali iliyokuwa inahamisha mizigo na vitu mbalimbali vya Gekul , mashaka ya vijana hawa walikuwa wanadai kuwa kuna mkakati wa kumtorosha mbunge huyo kipitia mpaka wa Kenya na Tanzania
 
Pride comes before failure, gekul kiburi tu ndio kimemponza kwa kuibiwa kiasi gani hadi afanye yote yale kama sio kiburi na wapo wengi wenye tabia kama yake
 
shida yetu watanzania nasisi wanyonge sana, ingekuwa nchi nyingine kwasasa hapo babati hapakaliki mpaka mhusika akamatwe.

Raia sasa tujifunze kujitetea hasa pale tunapoona sheria inataka kupindishwa kumfavor fulani.
Ukute anazurura tuu hapo babati kama vile ana spareroho!
Bangi za kaskazin kumbe hazina tija
 
shida yetu watanzania nasisi wanyonge sana, ingekuwa nchi nyingine kwasasa hapo babati hapakaliki mpaka mhusika akamatwe.

Raia sasa tujifunze kujitetea hasa pale tunapoona sheria inataka kupindishwa kumfavor fulani.
Hamia huko. Sheria ifuate mkondo wake.

Sent from my Infinix X656 using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…