My brother, hapa bwana panataka akili kubwa wala sio majority participation hii inayoendelea sasa nchini juu ya masuala haya, kwa sisi watu wazima tuliopata neema ya kuuona utendaji wa serikali za awamu zote tano tunahofia historia isije ikajirudia kama ilivyokuwa wakati wa Mwl Nyerere na sera zake za Nationalization ya njia kuu za uchumi toka kwa wawekezaji hasa wa kigeni ambao wakati huo tuliwaita wanyonyaji na miradi ya uwekezaji wao tuliiita mirija, kwa kila aina ya mbwembwe tulifanikiwa ku-forfeit the so called mirija yote ya kiuchumi toka kwa makupe hao na kuifanya kuwa mali ya umma, baada ya zoezi hilo hao MABEBERU waliji-organize duniani kote na matokeo yake cha moto tulikiona hawa jamaa walitu-drill accordinglly mpaka uchumi wa nchi uka-paralyse na hivi ndivyo wanavyoipiga sindano za ganzi serikali ya Nicholas Madullo wa Venezuela tokana na sera za Marehemu Hugo Chaves. Hofu, tahadhari na maswali yako vina maantiki pana sana ktk mjadala huu tete isipokuwa inahitajika electromagnetic telescope kupambanua logic hiyo.