Zita Act Retroactively? Tutavunja Mikataba Yote Iliyopo? Can we Stand? Do we have the Guts?

Oya jadili mada basi
 
Yalipozuiwa makontena bandarini mwanasheria msomi Tundu Lissu,akatoa tamko kwa mbwembwe mpaka kuleta hizohizo story za MIGA etc,tungemsikiliza na kufuata mawazo yake hata hii hatua ya miswada ingefikiwa??,kama tumeamua kwenda front twende front ili mabadiliko yaonekane kwa maslahi ya taifa,na kwa taarifa dukuduku mnazoziletaga hapa washauri na wasomi walio kwenye nafasi husika serikalini huwa wameshajadili,yote hayo na matokeo yake,tatizo wengi humu JF mnaichukulia poa serikali hii.
 
jingalao,
Mchango wako unasadifu jina lako.
Ni wapi mleta hoja ametishia? Zaidi naona ameleta mjadala ili tujadiliane pamoja. Kwanini unataka kila mtu apige tu makofi na kupongeza?
 
Mapendekezo ya sheria ni mazuri lakini wasiwasi wangu mkubwa ni kufukuza wawekezaji wakubwa in the future kwa sababu inaondoa lee way ya wao kufanya watakavyo (disincetive)
Kwahiyo waendelee kuwa na hiyo incentives sisi tuendelee kula kwa macho siyo?
 
Kasome civics kwanza!
 
la


Huyu ajuza naye alikuwepo wakati mikataba hii mibovu inapitishwa!
Jenista hana uzalendo na hii nchi ni mwanamke ndumila kuwili.
Tumesahau yale ya NSSF na SHOGA yake?

JPM ni muda muafaka kusikiliza upande wa pili acheni itikadi zenu za kisiasa kwenye mambo ya msingi kama haya!

Walioharibu ni hawa hawa wanaopiga makofi na kuandaa maandanmano ya kumpongeza huyo "MWENYEZI NCHI WAO"!
 
Inasikitisha una umri wa kushuhudia marais wote watano ila nado mwoga, hiki kizazi chenu asilimia kubwa ndo gundu kwa hili taifa!
 
Kwahiyo waendelee kuwa na hiyo incentives sisi tuendelee kula kwa macho siyo?
Ni angalizo tu, kuwa kuna side effects pia. Wawekezaji wakubwa wa madini walikuja kwa sababu ya vivutio na unafuu (loopholes) zilizokuwepo. Of course kuna wawekezaji ambao hawatajali marekebisho haya.
 
Tatizo tumetanguliza Uoga mbele kuliko KujiaminiKujiamini,
Sisi kwa sisi tunatishiana
wengine wanaomba kabisa mambo tawe mabaya kana kwamba si mtanzania!!
Tuwe na imani tuungane
 
Mapendekezo ya sheria ni mazuri lakini wasiwasi wangu mkubwa ni kufukuza wawekezaji wakubwa in the future kwa sababu inaondoa lee way ya wao kufanya watakavyo (disincetive)
Hao siyo wawekezaji wakubwa Bali ni wanyonyaji wakubwa!
Acha waondoke! Wamekuwa balaa na si Baraka kwetu!
 
Hofi ni emotions.Sheria hizo ni nzuri
 
Wananchi tunatakiwa kufanya kitu ili kuweka kumbukumbu sawa.
 
Pascal Mayalla,

Pascal, kwa maoni yangu hakuna namna hii sheria inaweza ku-apply retrospectively kiasi cha kuathiri Mineral Development Agreements (MDAs) in force.

Kwa wale wanaokumbuka, mwaka 1984 ulipitishwa, tena kwa hati ya dharura sana, mswada wa sheria ya wahujumu uchumi (Economic Sabotage and Organised Crime Act) ambayo awali ilikuwa na kipengele cha kuiwezesha itumike retrospectively.

Baada ya Rais Nyerere kuusaini huo mswada kuwa sheria, wanasheria wakiongozwa na Jaji Mkuu Francis Nyalali wakamkumbusha rais kuwa the purpose of law is to cause justice to reign and therefore the application of the law retrospectively would defeat that purpose.

Nyerere alichokifanya baada ya kupata huo ushauri ilikuwa ni kurudisha hiyo sheria bungeni na kufanyiwa marekebisho ya kuiondolea hadhi ya kuwa "retrospective law".

Swali ni je, hii hatua iliyochukuliwa mwaka 1984 haikuweka precedent kwa sheria zingine zozote zitazazotungwa na bunge hilo hilo? Lakini swali la msingi ni je, hii sheria mpya ina kipengengele cha kuiwezesha kutumika kinyume kinyume (retrospectively)?

Kuhusu baadhi ya watu kushangilia tu kila kinachofanywa na watawala, tatizo ni kwamba political passions distort people's thinking and sense of reality.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…